TANZIA Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad afariki dunia

TANZIA Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad afariki dunia

Aisee ni kweli jamaa historia yake ni balaa, namsikiliza Abdulkarim Atik hapa TBC 1 anamuelezea Maalim hakika mimi mwenyewe najilaumu kwanini sikufatilia historia ya huyu jamaa

Mzee Atik anasema Maalim alikwenda Brunei akaonana na mfalme na alipewa dollar za kutosha lakini aliporudi Znz akakabidhi zile Pesa zote japo alikabidhiwa yeye kama yeye kwa matumizi yake binafsi.

Mzee Atik anasema kama ingekuwa ni Kenya bac Maalim angekuwa mwanasiasa Billionaire na kumbuka yy ndio muasisi wa baraza la wawakilishi in short kafanya mengi ndani ya Znz
Huyu jamaa wachache walokuwa wanapendelea nafsi zao na wanafaidika na udhulumati walihakikisha hawampi nchi mana angeleta mabadiliko makubwa. Alikusudia hasa kuikomboa Zanzibar na Wazanzibar. Hakuchoka na alikua very patient akiamini ipo siku kusudio lake litafanikiwa. Makatili wachache hawakutaka kumpa nafasi.Rest easy legend. Atazaliwa tu kama yeye. ....one day yes.... mapinduzi ya ukombozi wa Mzanzibari yatapatikana tu.
20210217_213458.jpg
20210217_212600.jpg
 
Bwana alitwaa, bwana ametwaa sifa na jina vihimidiwe milele!
 
..kuna corona ya kukaa nyumbani, na kuna corona ya kukimbilia hospitali.

..kuna watu vijana kuliko Maalim Seif lakini corona imewasumbua zaidi ya mwezi hawajakaa sawa.
Huenda pia kuna corona ya kuambukizwa kwa kukaa na mwenye nayo na ipo inayowapata watu kwa kuikumbuka moyoni tu. Hii aina ya mwanzo wengi huipata na haina nguvu sana.Tatizo hii ya kujitengeneza kwa kuiwaza wakati uko peke yako ndiyo mbaya kwani haianzii puani wala kooni bali kwenye mapafu moja kwa moja.
 
Huyu jamaa wachache walokuwa wanapendelea nafsi zao na wanafaidika na udhulumati walihakikisha hawampi nchi mana angeleta mabadiliko makubwa. Alikusudia hasa kuikomboa Zanzibar na Wazanzibar. Hakuchoka na alikua very patient akiamini ipo siku kusudio lake litafanikiwa. Makatili wachache hawakutaka kumpa nafasi.Rest easy legend. Atazaliwa tu kama yeye. ....one day yes.... mapinduzi ya ukombozi wa Mzanzibari yatapatikana tu.View attachment 1704936View attachment 1704938
Mkuu umeandika maneno makaliii
Lkn hamna haja kuporomosha maneno makaali kiasi icho kumbuka hakunanmkamilifu mwingoni mwa sie wana damu
 
Ofisi ya makamu wa pili wa Rais Zanzibar imesema maalimu Seif rip atazikwa kesho kijijini kwao huko Pemba.

Mwili wa maalimu Seif utaondolewa hospitali ya Lugalo kesho saa 4 asubuhi na kuswaliwa katika msikiti wa Upanga kabla ya kusafirishwa kwenda Unguja saa 5 asubuhi.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Sawa shihata
 
Pumzika Kwa upole tulipenda harakati zako ila mungu kazipenda zaidi
 
Dah!
Mwamba ndio umelala milele.
Ni huzuni kubwa kwa wazanzibar.

Kuanzia uchaguzi wa 1995, 2000, 2005, 2010, 2015 na 2020 wazanzibar tunaamini kwa 100% kuwa Maalim Seif Sharif Hamad ndio alikuwa mshindi wa kiti cha urais wa Zanzibar. Wazanzibar tulimchagua yeye. Mara zote alidhulumiwa ushindi wake. CCM na watawala walipora kinguvu ushindi wake.
Ipo siku hiyo dhuluma itawatafuna pia hawa watawala katili wa CCM.
 
Nasikia Bakhressa katoa Meli kesho kupeleka watu pemba Buuure!

Jamani Jamani! Najua umma utakuwa mkubwa sana utakaokwenda Pemba kumsindikiza Kipenzi cha watu. Muhimmu watu wachukue tahadhari
 
Nasikia Bakhressa katoa Meli kesho kupeleka watu pemba Buuure!

Jamani Jamani! Najua umma utakuwa mkubwa sana utakaokwenda Pemba kumsindikiza Kipenzi cha watu. Muhimmu watu wachukue tahadhari
ishu si usafiri wa meli, changamoto ninayoiona mimi ni usafiri wa barabarani utakuwa wa tabu sanaaa na vurugu huko Pemba.
 
ishu si usafiri wa meli, changamoto ninayoiona mimi ni usafiri wa barabarani utakuwa wa tabu sanaaa na vurugu huko Pemba.
ninahisi huenda pasiwe na gari kabisa na watu wakausindikiza kwa miguu kutoka Airport mpaka Gombani kusaliwa na kutoka hapo mpaka kijijini kwake. Huu Mkusanyika utakuwa mkubwa kupita maelekezo na watu hawatakuwa na tahadhari yoyote. Na tunajua kuwa kuna watu wanabeba hivi virusi, kwenye umma huo watakuja kuumwa wengi mno ambao wengi wao watakuwa wazee na kuanza kuona idadi ya vifo ikikuwa kwa kasi ya ajabu sana. Kutokana na udogo wa visiwa hivi na watu kuwa karibu karibu bila tahadhari, haitoshangaza ikawa 80% ya wazanzibari wakajikuta wanaumwa na hii kitu.

Zanzibar ina Wizara yake ya Afya, wangefanya mazungumzo na S.A wakatupatia tu hio chanjo ilofeli kwao.
 
Hamphrey Polepole kwa jinsi alivyokuwa anamtusi huyu mzee sijui anajisikiaje huko alipo
 
Ulichoongea akina analysis yoyote, Azikwi kesho kwa sababu ya uislamu. Bali kwa sababu amefariki kwa korona, kama una kumbukumbu Selfu alitangaza kua anaumwa korona.
Hata kama ni muislam isingewezakana kumzika kesho makamu wa kwanza wa serikali ya Zanzibar kwa mtu aliyefariki Leo.
Afu unatakiwa ujue kua ratiba za maxishi ya kiongozi wa serikali yanaratibiwa na serikali.
Tuache kuleta hisia kwenye jambo bila kua na analysisi vizr
Wewe ndo huna analysis Kwa waislamu ni kawaida hawana ujinga to hold too long an empty body .... Hata isingekuwa corona ,... Serikali haina dini Ila inaheshimu taratibu za kidini za mhusika
 
Back
Top Bottom