TANZIA Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad afariki dunia

Huyu jamaa wachache walokuwa wanapendelea nafsi zao na wanafaidika na udhulumati walihakikisha hawampi nchi mana angeleta mabadiliko makubwa. Alikusudia hasa kuikomboa Zanzibar na Wazanzibar. Hakuchoka na alikua very patient akiamini ipo siku kusudio lake litafanikiwa. Makatili wachache hawakutaka kumpa nafasi.Rest easy legend. Atazaliwa tu kama yeye. ....one day yes.... mapinduzi ya ukombozi wa Mzanzibari yatapatikana tu.
 
Bwana alitwaa, bwana ametwaa sifa na jina vihimidiwe milele!
 
..kuna corona ya kukaa nyumbani, na kuna corona ya kukimbilia hospitali.

..kuna watu vijana kuliko Maalim Seif lakini corona imewasumbua zaidi ya mwezi hawajakaa sawa.
Huenda pia kuna corona ya kuambukizwa kwa kukaa na mwenye nayo na ipo inayowapata watu kwa kuikumbuka moyoni tu. Hii aina ya mwanzo wengi huipata na haina nguvu sana.Tatizo hii ya kujitengeneza kwa kuiwaza wakati uko peke yako ndiyo mbaya kwani haianzii puani wala kooni bali kwenye mapafu moja kwa moja.
 
Mkuu umeandika maneno makaliii
Lkn hamna haja kuporomosha maneno makaali kiasi icho kumbuka hakunanmkamilifu mwingoni mwa sie wana damu
 
Sawa shihata
 
Pumzika Kwa upole tulipenda harakati zako ila mungu kazipenda zaidi
 
Dah!
Mwamba ndio umelala milele.
Ni huzuni kubwa kwa wazanzibar.

Kuanzia uchaguzi wa 1995, 2000, 2005, 2010, 2015 na 2020 wazanzibar tunaamini kwa 100% kuwa Maalim Seif Sharif Hamad ndio alikuwa mshindi wa kiti cha urais wa Zanzibar. Wazanzibar tulimchagua yeye. Mara zote alidhulumiwa ushindi wake. CCM na watawala walipora kinguvu ushindi wake.
Ipo siku hiyo dhuluma itawatafuna pia hawa watawala katili wa CCM.
 
Nasikia Bakhressa katoa Meli kesho kupeleka watu pemba Buuure!

Jamani Jamani! Najua umma utakuwa mkubwa sana utakaokwenda Pemba kumsindikiza Kipenzi cha watu. Muhimmu watu wachukue tahadhari
 
Nasikia Bakhressa katoa Meli kesho kupeleka watu pemba Buuure!

Jamani Jamani! Najua umma utakuwa mkubwa sana utakaokwenda Pemba kumsindikiza Kipenzi cha watu. Muhimmu watu wachukue tahadhari
ishu si usafiri wa meli, changamoto ninayoiona mimi ni usafiri wa barabarani utakuwa wa tabu sanaaa na vurugu huko Pemba.
 
ishu si usafiri wa meli, changamoto ninayoiona mimi ni usafiri wa barabarani utakuwa wa tabu sanaaa na vurugu huko Pemba.
ninahisi huenda pasiwe na gari kabisa na watu wakausindikiza kwa miguu kutoka Airport mpaka Gombani kusaliwa na kutoka hapo mpaka kijijini kwake. Huu Mkusanyika utakuwa mkubwa kupita maelekezo na watu hawatakuwa na tahadhari yoyote. Na tunajua kuwa kuna watu wanabeba hivi virusi, kwenye umma huo watakuja kuumwa wengi mno ambao wengi wao watakuwa wazee na kuanza kuona idadi ya vifo ikikuwa kwa kasi ya ajabu sana. Kutokana na udogo wa visiwa hivi na watu kuwa karibu karibu bila tahadhari, haitoshangaza ikawa 80% ya wazanzibari wakajikuta wanaumwa na hii kitu.

Zanzibar ina Wizara yake ya Afya, wangefanya mazungumzo na S.A wakatupatia tu hio chanjo ilofeli kwao.
 
Hamphrey Polepole kwa jinsi alivyokuwa anamtusi huyu mzee sijui anajisikiaje huko alipo
 
Wewe ndo huna analysis Kwa waislamu ni kawaida hawana ujinga to hold too long an empty body .... Hata isingekuwa corona ,... Serikali haina dini Ila inaheshimu taratibu za kidini za mhusika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…