Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Heri ya Mwaka Mpya wanajukwaa!
Tuje hapa. Kumbe zile kelele nyingi za kudai kwamba kero za Muungano zimeanza kutatuliwa kwa kasi kumbe ilikuwa danganya toto. Mbona hii sasa ni tabu tupu!
=========================
“Kwa upande wa kero za Muungano, hakuna hata kero moja ya maana iliyotatuliwa. Aidha, waliojipa mamlaka Zanzibar hawaonekani na shauku ya kudai kutatuliwa kwa kero za muda mrefu na hata zile zinazoathiri maisha ya watu kila siku.
Soma Pia: - Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?
Ni dhahiri kwamba kama Zanzibar itaachwa iendelee na mfumo na hali ya sasa ya uendeshaji wa nchi, haitokuwa na mustakbal mwema na inaweza kufikia kuirithisha Zanzibar kwa kizazi kijacho ikiwa imekosa misingi madhubuti ya kiuchumi, utawala mwema na uzalendo kwa watu wake. Zanzibar inaweza kurithishwa mfumo uliojaa ufisadi na kukosa weledi wa uendeshaji Serikali na hivyo kuhatarisha mustakbal wake. Ni kwa sababu hizo ndio maana nasema, Zanzibar inahitaji kunusuriwa”- Othman.
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, na Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa, Othman Masoud Othman akitoa salamu za Mwaka Mpya 2025.