Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar - Public interest, wadau wa maendeleo, mukutano ya ndani ..

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
03 September 2021



Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mh. Othman Masoud, ofisi ya DPP lazima iwe inachunguzwa kama wenzetu huko Uingereza Ofisi ya Crown Prosecution yaani DPP huchunguzwa inavyofanya kazi

Umuhimu wa katiba Mpya upo. Kasoro za kikatiba zipo katika nyaraka za kikatiba inavyofahamika kama Tume ya Warioba. Katiba mpya iliyopendekezwa na Tume ya Warioba ilionesha wananchi waliona katiba iliyopo ina matatizo.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar anaongeza tunadhani kunaweza kuishi kwa kutumia mambo ya kizamani au kanuni za dunia iliyopita na serikali ya CCM kukataa suala la Katiba Mpya.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar azungumzia kinga ya viongozi kutoshitakiwa, viongozi wakumbuke kinga hiyo haikuzuii kushitakiwa nje. Bora kiongozi ushtakiwe halafu usamehewe badala ya kujiwekea kinga.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar atoa ushauri kuhusu upande mmoja wa Tanzania mikutano ya ndani kuzuiwa huku Zanzibar mikutano ya ndani ya vyama vya siasa Zanzibar inaruhusiwa.

Makamu wa Kwanza wa Rais Mh. Othman Masoud anakumbushia Nchi hii ina Wa(M)sajili wengi mfano msajili wa makampuni anachangia mchango mkubwa katika uchumi wa nchi kuliko msajili wa vyama vya siasa ambaye amepewa madaraka makubwa lakini hana mchango wowote kiuchumi lakini anauwezo wa kutoa kauli ikapelekea serikali ya nchi kupinduliwa kwa kusema Rais siyo mwanachama halali wa chama cha siasa . Msajili wa Vyama vya Ushirika, Msajili wa Makampuni, Msajili wa Vyama vya Siasa n.k

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar maoni yake kuhusu Mkutano wa Msajili na IGP kuhusu mikutano ya ndani ya Vyama vya kisiasa hauna afya kisiasa.
N.k

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar maoni yake ni kuwa Ma IGP waliopita kama Saidi Mwema na DCI Adadi walianzisha mageuzi ndani ya jeshi Polisi mazuri, lakini kwa sasa jeshi la Polisi limerudi nyuma katika kufanya mabadiliko yalitokuwa yameanza kwa jeshi la Polisi kujiondoa katika kutumika kisiasa.

Jeshi la Polisi linatakiwa kuelekea katika kazi za msingi yaani kupambana na uhalifu badala ya kuhangaika na vyama mikutano ya ndani ya vyama vya kisiasa.

Source : mubashara studio
Video Courtesy of StarTV Habari
 
Jamaa watajuta kumfahamu kwanza alishataka ugali umwagike ni vile tu watu wanaogopa vimisaada kuisha maana zanzibar nao umasikinmi mkubwa sana ni vile wanabebwa tu na bara
 
Mwanasheria asiyehendekeza Njaa utamjua tu.

Hongera sana Mh Makamu wa Rais.

Mtoto wa Mwinyi atanuna kwa kauli hizi za ukweli
 
Jamaa watajuta kumfahamu kwanza alishataka ugali umwagike ni vile tu watu wanaogopa vimisaada kuisha maana zanzibar nao umasikinmi mkubwa sana ni vile wanabebwa tu na bara
Zanzibar hakuna umaskini kuna rushwa na ubadhilifu uliokithiri na hutokaa usikie tetesi za ufisadi mahali popote.
 
Rais Samia anajua jama Msajili wa Vyama anaweza kumpindua?? Au anadhani waathirika ni wapinzani tu?
 
Naunga mkono hoja. Wakati mwingine uluwa huwa unalevya. Waache wajisahau, wataona baadae. Kwa kawaida mbuyu unaanza kama mchicha.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Samia aache kuvaa sare za ACT wazalendo japo ni Raisi wa vyama vyote.

CCM oyee !
 
Sema zinamkaa vizuri sana kuliko ile langi ya kijani inamzeesha tu,ona hiyo ya ACT kichuna kabisa.

Inamtoa kuonekana kizere.
 
Mawazo na fikra huru toka kwa kiongozi wa juu, hakika anastahili pongezi Makamu wa Kwanza wa Rais serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mh. Othman Masoud kwa kujibu na kuelezea hali halisi ya kisiasa na uongozi ilivyo nchini mwetu Tanzania.
 
Naunga mkono hoja. Wakati mwingine uluwa huwa unalevya. Waache wajisahau, wataona baadae. Kwa kawaida mbuyu unaanza kama mchicha.

Kabisa wanasahau msajili na jeshi la Polisi kutumika kisiasa ni jambo la kizamani

Toka maktaba:

4 October 2021
CHADEMA WAWAKA VIKALI JUU YA KAMATA KAMATA YA WAFUASI WAKE, POLISI SASA WAJISAJILI KUWA CHAMA CHA SIASA


Source : mubashara studio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…