Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman: Mtanzania yeyote mwenye akili hakuna atakayelalamika namna Muungano unavyoendeshwa

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
276
Reaction score
473
Akizindua maonesho ya biashara ya Miaka 60 ya Muungano, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman amesema wananchi wanatakiwa kuendelea kutambua umuhimu na tija za Muungano, ambapo amewahasa wanaofahamu vyema manufuaa yaliyopo kuendelea kuwaelimisha wengine hususani vijana ili waweze kuelewa vyema.

Amedai kuwa Mtanzania anayepinga Muungano unavyoendeshwa atakuwa na matatizo ya afya ya akili hivyo anatakiwa kufanyiwa uchunguzi.
WhatsApp Image 2024-04-19 at 19.34.14_3c1c009d.jpg
"Leo hii Mtanzania mwenye akili hawezi kuwa na maneno mabaya dhidi ya Muungano huu, na mimi nawaambieni vijana mpo hapa na wananchi mnanisikia Mtanzania yeyote mwenye akili hakuna atakayelalamika namna Muungano huu unavyoendeshwa," amesema Hemed Suleiman.
WhatsApp Image 2024-04-19 at 19.34.14_f3163ff3.jpg

WhatsApp Image 2024-04-19 at 19.34.14_bf3d42e7.jpg
Ameongeza kuwa "Ukimuona Mtu analalamika muangalie kwenye mambo mawili, kwanza mtazame kama akili yake ipo timamu ukiona mambo sio balabala mwambie Mh. Ummy Mwalimu (Waziri wa Afya) shughulika na huyu Mtu, na kule tunaye Mh. Mazrui (Waziri wa Afya Zanzibar) tutamwambia shughulika na huyu Mtu akili yake haipo sawa.

Ameyasema hayo April 19, 2024 wakati akihutubia kwenye uzinduzi huo ambao umefanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam akiwa mgeni rasmi kwenye hafla iliyowakutanisha wadau mbalimbali kutoka kwenye taasisi zinazohusika na masuala ya Muungano.

Aifha awali Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Khamis Hamza Khamis amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) mpaka sasa zimefanikiwa kutatua hoja 22 za Muungano kati ya 25 zilizokuwepo awali, huku akidai kuwa utatuzi unaenedelea kwenye hoja nyingine.

Ambapo katika hotuba yake amesema taasisi za Muungano ambazo zipo Tanzania bara zimefungua ofisi Zanzibar ikiwa ni kukuza usawa katika utoaji huduma.

"Katika kuhakikisha usawa wa utoaji huduma kwa wananchi wa pande zote mbili, taasisi za Muungano zilizopo Tanzania bara hadi sasa taasisi 33 zimefungua ofisi Zanzibar kati ya taasisi 39 za Muungano"amesema Naibu Waziri huyo

Sanjari na hayo Naibu Waziri huyo ametoa rai kwa wananchi kuendelea kutunza vyanzo vya maji ili kuepuka athari za mabadiliko ya tabia ya Nchi, huku akisisitiza kuwa maono Rais Samia Suluhu Hassan ni kuona inapofikia 2030 watanzania wawe wanatumia nishati mbadala, hali ambayo amedai itasaidia kulinda mazingira.

Maadhimisho hayo yanatarajiwa kuhitimishwa April 25, 2024 ambapo wananchi watapata fursa ya kujifunza masuala mbalimbali kupitia taasisi zinazoshiriki maadhimisho hayo, pamoja na kupokea ushauri na huduma mbalimbali.
 
LIKEWISE MTANZANIA ANAYEONA MUUNGANO HAUNA KASORO HANA AKILI TIMAMU
 
Nilitarajia azitaje hizo fursa za muungano hasa kwa upande wa Watanganyika, yeye anaongea blah blah😡😡
 
Kila uchao tunasikia kina Jafo wametatua kero za muungano, lakini kero hizo sisi wanànchi hatuzijui na sijui wamezitatua vipi. Isije ikawa CCM Wana create tatizo halafu wanalitatua kwa kutumia fedha za Uma.
Mwenye uelewa tafadhali.
Lucas Mwashambwa
@€twege
ChoiceVariable
 
Imagine neema na heri zilivyotamalaki Zanzibar wakati huu.

Hakuna Wakati Mzuri kuwa Mzanzibari kama Wakati huu.

Kule hakuna kuuzwa Bandari wala Hifadhi za Taifa.

Kule hakuna kufukuza Wakaazi wa Asili (kwa mfano Wanakijiji wa Kizimkazi) kutoka katika Ardhi yao kama walivyofukuzwa Ngorongoro, na watakavyofukuzwa tena baada ya Uchafuzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchafuzi Mkuu kushinza Uchafuzi wowote, 2025.

Zanzibar huwezi kusikia mtu kutekwa, kupotezwa kwa namna yoyote ile, ama kushushwa kutokea kwenye Jahazi na kudhulumiwa Uhai wake.

Zanzibar haiwezekani Mgeni afike akayatenda yote maovu na bado akawafokea wenye nchi yao kwa masimango na kudemka.

Zanzibar hadi Kizimkazi ni heri tupu na Matamasha kila kukicha.

Hakika hakuna wakati mzuri kula matunda ya Muungano ya kuwacheka Wadanganyika(Machogo) kama wakati huu.

SALAMALEKO Wadanganyika

Hadi Mseme kudadeki, na Mtasema🚮
 
Zanzibar deni la umeme likiwa kubwa wanasamehewa/linalipiwa na Tanganyika hadi raha

Wazenji ni kama malaika vile wanamiliki ardhi kwao na Tanganyika hadi raha.
 
Back
Top Bottom