Makamu wa Rais Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi: Taifa limepata pengo kuondokewa na Jenista Mhagama

Makamu wa Rais Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi: Taifa limepata pengo kuondokewa na Jenista Mhagama

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema Taifa limepata pengo kuondokewa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma, marehemu Jenista Mhagama ambaye alikuwa kiongozi aliyeheshimika na kutumikia nchi katika majukumu mbalimbali ya kitaifa.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati akitoa salamu za rambirambi alipowasili kuhani msiba nyumbani kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, marehemu Jenista Mhagama eneo la Itega Jijini Dodoma. Amesema marehemu Mhagama licha ya kuwa ni alikuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, lakini pia alitoa mchango wake katika Chama Cha Mapinduzi na kusimamia maendeleo ya Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.

Makamu wa Rais ametoa pole kwa familia na waombolezaji na kuwaombea watoto wa marehemu na ndugu wa karibu, Mungu awape ujasiri wa kukubali jambo hilo na kutambua ni njia ya watu wote.

IMG-20251211-WA0091.jpg
IMG-20251211-WA0092.jpg
 

Attachments

  • IMG-20251211-WA0088.jpg
    IMG-20251211-WA0088.jpg
    428.3 KB · Views: 27
Ndugu zangu Watanzania,

Makamu wa Rais Mheshimiwa Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi amefika nyumbani kwa Marehemu Jenista Mhagama na kutoa salamu za pole.
Screenshot_20251211-205048_1.jpg
 
Msiba pekee wa kitaifa tunaoutambua ni wa watanganyika waliouwawa tarehe 29-31 October na muuaji kibibi wa Kizimkazi na hadi leo kuna familia hazijapata maiti za ndugu zao wazike.

Bibi yake Soka hadi leo hajui mjukuu wake alipo aliomba hata nywele akazike hajapewa.

Mama yake Polepole kazunguka mahakamani na polisi kuomba mwanae arudishwe hata kama wamemuua wampe akamzike mwenyewe ila bado wamemnyima fursa hiyo.
20251126_161405.jpg
 
Back
Top Bottom