Makamu wa Rais, Dkt. Mpango Aielekeza Wizara ya Madini Kusimamia Madini Mkakati kwa Manufaa ya Watanzania

Makamu wa Rais, Dkt. Mpango Aielekeza Wizara ya Madini Kusimamia Madini Mkakati kwa Manufaa ya Watanzania

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

DKT. MPANGO AILEKEZA WIZARA YA MADINI KUSIMAMIA MADINI MKAKATI KWA MANUFAA YA WATANZANIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango ameitaka Wizara ya Madini kuhakisha inasimamia vyema uvunaji wa madini ya kimkakati ili nchi iweze kunufaika nayo.

Mh. Dkt. Mpango ameyasema hayo leo Katika eneo La Mpwayungu,Wilaya ya Chamwino-Dodoma wakati akihitimisha ziara ya siku 4 ya Mkoa wa Dodoma.

“Mwenyezi Mungu ametujaalia rasilimalo hii ya madini mkakati yenye mahitaji makubwa sana Duniani.

Mkoa wa Dodoma umebarikiwa kuwa na madini haya mkakati kwa uwingi na aina tofauti tofauti,lazima rasilimali hii ikatafsirike katika maendeleo ya wananchi wa Dodoma na Tanzania kwa ujumla.

Wizara ya Madini hakikisheni mnaweka mpango mzuri wa usimamizi wa rasilimali hii kwa manufaa ya Taifa na kwa manufaa ya vizazi vijavyo”Alisema Dkt. Mpango

Akiwasilisha salamu za Wizara,Waziri wa Madini * Mh. Anthony Mavunde* amemuahidi Dkt. Mpango kuyafanyia kazi maelekezo yote na kwasasa Wizara inakamilisha andiko la mkakati wa usimamizi na uvunaji wa madini haya ili yalete faida kwa nchi kwa kuchochea uchumi na kuendeleza sekta ya madini.

Mh. Mavunde alitumia fursa hiyo kutoa maelekezo kwa Afisa Madini Wakazi(RMOs) kuhakikisha wanasimamia ipasavyo maeneo yenye uchimbaji wa madini mkakati ili manufaa yake yaonekane kwa Taifa.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-08-22 at 15.04.19.jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-22 at 15.04.19.jpeg
    170 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-08-22 at 15.04.20.jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-22 at 15.04.20.jpeg
    164.4 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-08-22 at 15.04.24.jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-22 at 15.04.24.jpeg
    168.1 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-08-22 at 15.04.25.jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-22 at 15.04.25.jpeg
    106.6 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-08-22 at 15.04.25(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-22 at 15.04.25(1).jpeg
    176.1 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-08-22 at 15.04.26.jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-22 at 15.04.26.jpeg
    100.1 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-08-22 at 15.04.26(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-22 at 15.04.26(1).jpeg
    191 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-08-22 at 15.04.28.jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-22 at 15.04.28.jpeg
    157.5 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-08-22 at 15.04.29.jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-22 at 15.04.29.jpeg
    148.2 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-08-22 at 15.04.29(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-08-22 at 15.04.29(1).jpeg
    164 KB · Views: 1
Back
Top Bottom