Makamu wa Rais, Dkt Mpango anasafiri kwenda Singapore leo Novemba 14

Makamu wa Rais, Dkt Mpango anasafiri kwenda Singapore leo Novemba 14

Nakutakia safari njema Mh. Mpango, nchi inaendeshwa kwa mipango makini na wala mtu huwezi kujifungia ndani eti kwa kisingizio cha kubana matumizi. Hiyo ni safari ya kikazi na yenye manufaa makubwa hapo baadaye kwa nchi yetu.

Natarajia hapo baadaye kuwa utatembelea nchi nyingine kama vile za Scandinavia, Amerika Kaskazini na Kusini, Umoja wa BRICS, Umoja wa Ulaya huku ukiambatana na ujumbe mzito wenye wataalamu mbalimbali ili wapate kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwa wenzetu.
Hawa wanahudhuria mikutano ambayo ni open kwa viongpzi wa nchi zote, lakini ni kazi sana kupata mialiko ya nchi za Ulaya Magharibi na Amerika ya Kaskazini. Samia alijaribu sana alipokuwa Marekani ilishindikana.

Mataifa ya Ulaya na America yana ethics. Samia alitaka akutane na Biden, huku nchini kwake akiwa amewafungia kwenye mahabusu za polisi wanaomkosoa. Wakamkatalia. Mpaka sasa mialiko ya nchi ategemee zaidi ya mataifa ya Afrika ambayo hayana ethics.
 
Naona Wanapishana tu angani, huyu akirudi utasikia Chifu nae amepata mwaliko tena
 
Makamu wa Rais Dkt. @dr_philip_isdor_mpango leo [emoji1001]Nov 14,2021 anatarajia kuondoka Nchini kuelekea Sentosa Island Nchini [emoji1215]Singapore kushiriki mkutano wa Jukwaa la Majadiliano ya Kiuchumi (Bloomberg New Economy Forum 2021 ), Wenye lengo la kujadili masuala mbalimbali ikiwemo muelekeo mpya wa kiuchumi baada ya athari za Uviko19.

Aidha Makamu wa Rais anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na Viongozi wa nchi mbalimbali, Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa
Wafanyabiashara pamoja na Wakuu wa Taasisi mbalimbali kwa lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya 🇹Tanzania na nchi hizo pamoja na Taasisi zao.Mkutano huo unatarajia kufanyika kuanzia Novemba 16 hadi November 19, 2021

View attachment 2010128
Akitoka huko apitie Ethiopia kuona wenzetu wanavyojengwa bwawa la kufua umeme

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom