Makamu wa Rais Dkt. Mpango, kuna Hospitali nyingine zaidi ya Benjamin Mkapa zinazohitaji kusikilizwa changamoto

Makamu wa Rais Dkt. Mpango, kuna Hospitali nyingine zaidi ya Benjamin Mkapa zinazohitaji kusikilizwa changamoto

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
20,834
Reaction score
26,217
Wanabodi...

Tunaelewa baada ya Mh Philip Mpango kupitiwa na lile tatizo la Upumuaji na hatimaye akavuka salama baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma wakati akiwa bado Waziri wa Fedha na Mipango.

Ni hakika alishukuru kwa namna wafanyakazi wa Benjamin Mkapa hospital walivyomsaidia mbele ya kamera huku akimwaga machozi na aliahidi kwenda kuishauri Serikali namna ya kuboresha huduma za afya zaidi katika hospitali zetu.

Cha ajabu toka wakati huo mpaka sasa ni zaidi ya mara mbili ameshaitembelea hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma lengo likiwa ni kwenda kuwasalimia wafanyakazi.

Hilo halina shida lakini kuna hospitali nyingi nchini ambazo yeye kama Makamu wa Rais anawiwa kuzifuatilia hata kwa salamu na kusikiliza chamgamoto zao hata kama hajawahi kupatiwa matibabu katika hizo hospitali.
 
Wanabodi...


Tunaelewa baada ya Mh Philip Mpango kupitiwa na lile tatizo la Upumuaji na hatimaye akavuka salama baada ya kupatiwa matibabu katika hospitali ya Uhuru iliyopo Dodoma wakati akiwa bado waziri wa fedha na mipango.

Ni hakika alishukuru kwa namna wafanyakazi wa Uhuru hosp walivyomsaidia mbele ya kamera huku akimwaga machozi na aliahidi kwenda kuishauri serikali namna ya kuboresha huduma za afya zaidi katika hosp zetu.


Cha ajabu toka wakati huo mpaka sasa ni zaidi ya mara mbili ameshaitembelea hosp ya Uhuru iliyopo Dodoma lengo likiwa ni kwenda kuwasalimia wafanyakazi.


Hilo halina shida lakini kuna hosp nyingi nchini ambazo yeye kama Makamu wa Rais anawiwa kuzifuatilia hata kwa salamu na kusikiliza chamgamoto zao hata kama hajawahi kupatiwa matibabu katika hizo hosp.
Hivi alilazwa hospitali ya Uhuru au Benjamin Mkapa?
 
Back
Top Bottom