Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Leo nimemsikia mubashara mheshimiwa Makamu wa Rais ndugu Philp Mpango alipokuwa anahutubia viwanja vya Mnazi Mmoja kwenye kilele cha kumbukizi ya kuzaliwa chama chetu CCM.
Nilidhani kwenye hotuba yake ataainisha mikakati ya serikali kudhibiti mfumuko na kuboresha ugumu wa maisha unaowakabili wananchi.
Makamu wa Rais alisimama na kusema kuwa balaa la bei kupanda linavumilika kwa sababu mfumuko wetu upo asilimia 4 tangu mwaka jana hadi leo. Hapo awali nilishasema kwenye threads zangu kuwa Mungu wa Mbinguni ameondoa kauli katika viongozi wa serikali wanaotoka CCM.
Tulimsikia Rais akisema kuwa wanaolalamimia mabehewa used ya SGR ni watoto wa miaka ya 90 hivyo aliwabeza watanzania kuwa kulalamika lalamika ni utoto.
Juzi tumemsikia TULIA akisema CCM hata iweje hawatompisha mshindi yeyote madarakani. Kauli yake haikuzingatia utawala bora.
Leo Makamu wa Rais anawahadaa Watanzania kuwa mfumuko wa bei ni mdogo na stahimilivu kwa kulinganisha na mataifa jirani zetu yaani Kenya na Uganda.
Je, Mhe. Philip Mpango amejiridhisha kuwa bei ya mahitaji muhimu iliyopanda zaidi ya mara mbili ni himilivu huku akijua kipato cha wafanyakazi kimeendelea kuwa kidogo kwa raise ndogo sana ya mishahara.
CCM ilmechoka na kupoteza dira na mwelekeo kwa sababu hata viongozi wake wakuu hawana tena ari na dhamana ya kusimamia nchi badala yake wanasimamia CHAMA KUSHIKA DOLA
Tuendelee kuomba, watakuja wakombozi kutuweka katika reli tena.