Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
- Thread starter
- #21
Umeongea tafakuri nzito.Mkuu, kwa maoni yangu naona kama tumo kwenye mpito. Uwe wa majaribu au mgumu, tutapita.
CCM bado imejizatiti pamoja na 'wachumia' tumbo kukithiri. Nafikiri hii itakuwa mara ya kwanza katika muda ninavyoijua historia ya Chama na uongozi wake, kuona wamelewa madaraka maradufu....
Madaraka hulevya, hauepukiki, lakini kwa sasa ni kufuru...kwa sababu hela imekuwa nje nje na ukichanganya kilevi cha madaraka, wanahisi au kudhani hawashikiki. Joking aside, Mh. Tundu Lissu atawatikisa wale watakao tikitishwa na matoroli yake ya taarifa, watajirudi They will sober up. Wajitathmini. Wajipange.
Ni kweli Wananchi maisha ni magumu kwa mtu wa kima cha chini, lakini ndio ubepari waliokuwa wanalilia. Hakuna kukwepa
kastori kafupi ka kweli.
Miaka ya nyuma nilimsii jamaa yangu asiuze shamba lake alikiwa analima michicha, nyanya vitunguu bilinganya yaani mahitaji yake yalikuwa sio makubwa zaidi ya ku attend shamba, pia, shamba lake lliikuwa na mbaazi mihogo, miti yake mitatu ya korosho, mti mmoja wa machungwa na mchenza na mkungu nyumba yake ya udongo na mabati na palikuwa na kisima cha maji. oooh na wanyama wachache kuku, bata, mbuzi na kondoo
Alikuwa analalamika kutokuwa na sembe, mchele n.k na baada ya wanawe kuhama walimletea Luninga wakaunganisha solar. Baadae mzee yule akaniambia maisha ni magumu, sikumwelewa??? Nilimwambia Mwaka huo , ulikuwa 2008 ukiwa na elfu 30,000 sasa hivi mzee uko tajiri kuliko Mtu wa Ulaya, mzee huna deni shamba lako, nyumba yako....hakunielewa anadai anavaa mitumba! Namkejeli Ebbo basi 2012 mwishoni akauza shamba akapata mshiko mzuri tuu akapanga, baadae fedha ikakatika, 2017 madeni juu stori shoti ikabidi arudi kwenye banda lake pembezoni mwa shamba ambalo aliliuza, mabati wamesha ondoa na sio hivyo tu yani ikabidi awe analima kwenye shamba alilouza, kukata michongoma n.k ukumbuke
keshazeeka lakini inabidi awe na hela za kugharamia kila kitu....kuanzia matunda mpaka mchicha, mihogo n.k
Nafikiri amenikumbuka, nafikiri
sasa huyo ndie anasikia mfumuko wa bei.na.kuelewa bila hata shule!
Aisee
Lakini unaposema CCM wapo makini and put maana yake umeshashiba propaganda kuwa nchi hii bila CCM tutayumba.
Tusiwajaze hofu wasomaji