Makamu wa Rais Dkt. Mpango ziara yako Manyara imeleta hasara na Usumbufu mkubwa kwa wananchi

Viongozi huwa wanakera sana kwa hii tabia...mpaka inafika mahali mtu unatamani wapite usiku!!
 
Tiba ni katiba mpya, Blue lights ni kwa top 3leaders only na wao pia watahakikisha misafara yao haina athari sana,President HH ana msafara wa gari 3 tu(inayosafisha njia..polisi;ya kwake;protection unit yake)na mara chache wanatumia Blue lights, nimeshuhudia mno hii ndani ya Cairo road, Lusaka
 
Acha upotoshaji

 
Kwa nini wasiwe wanatumia Helicopter??
 
Mbona tuliambiwa ni ziara ya Riziwani Kikwete!?
 
Niliwahi msindikiza bibi airport ikatokea Samia anarudi kutoka sijui wapi ile alifika usiku. Yani tulisubirishwa masaa mawili ile Nyerere road. Kuna wazungu maskini walikuwa wanawahi walibidi waburuze mabegi kwenye lami. Walilaani sana lazima walitumia shit hole country. Ile siku nina uhakika kabisa kuna watu waliachwa
 
Ulitumwa ukanunue mabasi kwa mkopo?
Rejesho linakusumbua.
 
Pamoja na kwamba huna uandishi mzuri. Ila hata mimi huwa nashangaa hii tabia ya kufunga barabara muda Mrefu eti kusubiri kiongozi apite na ujuha wa hali ya juu. Mtu yuko madarakani kwa wizi wa kura, ila anataka asujudiwe.
Mkuu Tindo huo ujuha wa kiwango cha juu sana, unaotokana na fungate la kijuha kati ya majizi ya kura CCM na vikaragosi vyao vilivyopo ndani ya vyombo vya dola. Na kwa hakika hiki ndicho chanzo halisi cha maamuzi ya kijuha.

Maamuzi haya yanayoathiri shughuli nyingi za kawaida za watu wengi, na tena kwa muda mrefu ni ya kipuuzi sana. Upuuzi wa kuusubiri na kuupisha msafara wa kiongozi mmoja ili apite na kuonekana kwa hao anaowaudhi, huku akionyesha kero zake za dhahiri kwao, kea kuzidi kuwachelewesha katika mishemishe zao huku akiwatambia na kufanya msafara wenye mbwembwe na anasa nyingi.
 
R.C Makongoro Nyerere,ujumbe umefika...Wangekusikiliza tu....Ila..'Karibu Nyumbani Mkuu'..Wakizingua
 
Pamoja na kwamba huna uandishi mzuri. Ila hata mimi huwa nashangaa hii tabia ya kufunga barabara muda Mrefu eti kusubiri kiongozi apite na ujuha wa hali ya juu. Mtu yuko madarakani kwa wizi wa kura, ila anataka asujudiwe.
Huo ndio utaratibu na LAZIMA uheshimiwe kama mnavyoheshimu kila neno la Mbowe.
 
Thubutu, wameshatoka kwenye huo upuuzi boss. Labda sio Marekani tuliyofika na kuishi.
Kwani ninachosema ni siri. Ebu nitumia msafara wa Joe Biden ukiwa barabarani ukipishana na magari ya wananchi. Usiponitumia utakuwa huna tofauti na Mungu wa Zumaridi wa huko kwenu Mwanza.
 
Viongozi huwa wanakera sana kwa hii tabia...mpaka inafika mahali mtu unatamani wapite usiku!!
Teh teh teh 😂😂...huo usiku watakua wanafanya shughuli gani sasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…