Pre GE2025 Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amewataka wananchi mkoani Kigoma kuutambua na kuuthamini mchango wa Serikali katika maendeleo ya huduma za kijamii

Pre GE2025 Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amewataka wananchi mkoani Kigoma kuutambua na kuuthamini mchango wa Serikali katika maendeleo ya huduma za kijamii

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

the guardian 17

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
395
Reaction score
570
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amewataka wananchi wa Kijiji cha Kasumo wilayani Buhigwe mkoani Kigoma kuutambua na kuuthamini mchango wa Serikali katika maendeleo ya huduma za kijamii wilayani humo.

1741086468802.png


Makamu wa Rais amesema hayo alipotembelea ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Kahimba iliyopo katika kijiji hicho, na kuongeza kuwa kwa muda mrefu Wanakasumo na maeneo jirani walikuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma za kijamii, lakini sasa huduma hizo zimesogezwa karibu zaidi na wananchi.

Dkt. Mpango amesema ujenzi wa barabara za lami, madaraja, zahanati, shule na huduma za maji ni jitihada za Serikali katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, hivyo wananchi wanapaswa kushukuru kwa kumpigia kura za ndio katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
1741086507207.png


Kwa wanafunzi walioanza kusoma katika shule hiyo ya sekondari ya Wasichana Kahimba, Dkt. Mpango amewataka kutumia vizuri nafasi waliyopata kwa kusoma kwa bidii ili shule hiyo iweze kutoa wataalamu wazuri kama ilivyo kwa shule nyingine kubwa nchini.

Makamu wa Rais ameahidi kutoa zawadi shuleni hapo kwa wanafunzi watano wa kwanza katika mitihani ya mwisho ya kila mwaka pamoja na kwa walimu watakaofaulisha vema masomo yao, ikiwa ni motisha ya wanafunzi hao kusoma kwa bidii.

Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Source: TBC Digital
 
Back
Top Bottom