Makamu wa Rais Dkt. Phillip Isdor Mpango amefungua Barabara ya Loliondo–Mto wa Mbu (km 217) Sehemu ya Wasso-Sale (km 49)

Makamu wa Rais Dkt. Phillip Isdor Mpango amefungua Barabara ya Loliondo–Mto wa Mbu (km 217) Sehemu ya Wasso-Sale (km 49)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
1684373453376.jpg
Makamu wa Rais Dkt Phillip Isdor Mpango amefungua Barabara ya Loliondo–Mto Wa Mbu (km 217) Sehemu ya Wasso-Sale (km 49) ambayo imekamilishwa na Serikali kupitia TANROADS kwa kiwango cha lami wilayani Loliondo mkoani Arusha.

Akizungumza na wananchi waliojitokeza kushuhudia barabara hiyo, leo tarehe 17Mei 2023 Makamu wa Rais Dkt Mpango amesema pamoja na kwamba gharama za ujenzi wa barabara ni kubwa Serikali inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan itahakikisha inajenga kipande cha barabara kilichobaki kwenda Mto wa Mbu.

Kwa kuanzia Makamu wa Rais Dkt Mpango ameiagiza Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuhakikisha kuwa inaweka kwenye Bajeti ya Wizara hiyo itakayosomwa Jumatatu 22 Mei, 2023 na kuomba fedha kwa ajili ya ujenzi wa kipande kingine korofi cha barabara chenye kilometa 24 kutoka Ngaresero kwenda Engaruka wakati Serikali kupitia TANROADS ikiendelea na mchakato Ujenzi wa sehemu nyingine ya barabara hiyo.

Naye Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Geoffrey Kasekenya amesema barabara hiyo ni muhimu kwa wananchi wa mkoa wa Arusha, wilaya ya Ngorongoro, Loliondo na vijiji vyote ambavyo barabara hiyo inapita na kwamba inahitajika sana na watalii wanaokwenda Mbuga ya Serengeti, lengo likiwa ni hadi kufikia mwaka 2025 mikoa yote iwe imeunganishwa na barabara nzuri kwa kiwango cha lami.

"Naomba niwape Wananchi hawa taarifa, Rais ametoa maelekezo, kipande cha kilometa 10 kutoka Wasso kwenda Makao Makuu Loliondo nacho kipo kwenye hatua ya manunuzi ili kijengwe kwa kiwango cha lami, Mtu akitoka Makamo Makuu ya Wilaya anakuja Wasso anaendelea na lami" ameongeza Naibu Waziri Kasekenya.

Screenshot_20230518-040151.png
Screenshot_20230518-040126.png
Screenshot_20230518-040213.png
Muonekano wa Barabara ya Mto wa Mbu - Loliondo:Sehemu ya Wasso-Sale yenye urefu wa kilometa 49 wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha iliyofunguliwa rasmi leo tarehe 17 Mei 2023.

1684371889423.jpg
1684371888139.jpg
1684371887773.jpg
1684371886136.jpg
1684371863925.jpg
1684371885976.jpg
Wakazi wa eneo la Sale wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango wakati wa Ufunguzi Rasmi wa Barabara ya Wasso hadi Sale yenye urefu wa kilometa 49 wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha mapema leo.

1684373173973.jpg
1684373171210.jpg
1684373171408.jpg
1684373167363.jpg
1684373167510.jpg
 
Hii nzuri 🎦naona sasa tuangalie tena km nyingine kama hizi, usiishie hapa tukaze mwendo.
 
Kwan kikombe kimerejea? Watu wa loliondo na wamchague mtoto wa mwaisapile kuwa mbunge wao! The late babu wa loliondo waz veri krietivu! And smart upstairs
 
Back
Top Bottom