Kushiriki utiaji saini wa makubaliano ya ufufuaji wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania – Zambia (TAZARA)
Makamu wa Rais wa Tanzania, John Nchimbi, amewasili nchini Zambia kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Vyombo vya habari vinaripoti kuwa Dk Emmanuel Nchimbi aliwasili kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda, kwa ndege ya Air Tanzania.
Alipokelewa na Waziri wa Afya, Elijah Muchima, sambamba na Meya wa Lusaka Chilando Chitangala, Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Ltuteni Jenerali Matthew Mkingule na viongozi wengine waandamizi wa serikali ya Zambia na Tanzania.
Dk Nchimbi anatarajiwa kushiriki utiaji saini wa makubaliano ya ufufuaji wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania – Zambia (TAZARA) unaotarajiwa kufanyika kesho mjini Lusaka.
Waziri Mkuu wa China Li Qiang Awasili Zambia kwa Ziara Muhimu
View: https://m.youtube.com/watch?v=uL70HKs7hTMWaziri Mkuu wa Baraza la Serikali ya China Bw. Li Qiang amewasili nchini Zambia jioni ya leo kwa ziara ya siku mbili ya ngazi ya juu kwa mwaliko wa Rais Hakainde Hichilema.
Katika ziara hiyo, Bw. Li atafanya mazungumzo baina ya nchi hizo mbili na Rais Hichilema na kushuhudia uanzishwaji wa mradi wa ufufuaji wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA).
Safari yake inafuatia ziara ya kitaifa ya Rais Hichilema nchini China mwezi Septemba 2023, ambapo Zambia na China ziliboresha uhusiano wao wa muda mrefu na kuwa Ushirikiano wa Kimkakati wa Ushirika wa Kimkakati.
Ziara hiyo inatarajiwa kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika maendeleo ya miundombinu, biashara na uwekezaji.