BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amewasili Jijini New York nchini Marekani ambapo anatarajia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Baraza Kuu la 77 la Umoja wa Mataifa (UNGA).
Makamu wa Rais anatarajiwa kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika Ukumbi wa Mikutano wa Umoja wa Mataifa Jijini New York nchini Marekani tarehe 22 Septemba 2022.
Aidha Makamu wa Rais ataongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mikutano mbalimbali inayohusu Uchumi, Elimu, Afya, Demokrasia na Malengo ya Maendeleo Endelevu ambayo Tanzania imealikwa na nchi washirika, Taasisi za kimataifa na Asasi binafsi.