Makamu wa rais Ndejembi aagiza saruji kushuka bei

Makamu wa rais Ndejembi aagiza saruji kushuka bei

Hapana hakutaka Kuingilia mifumo alya wataalam, ndio Maana ameagiza waziri wa viwanda na biashara pamoja na Kamishina wa TRA hawa ni wadau Muhimu kwenye mchakato wa kushusha bei
..kwa hiyo jibu pekee ni kushusha bei, na wewe akili yako ndio imeishia hapo vile km unaona hilo ndio jibu..
 
Wangeruhusu tu sement itoke China na India tuuziwe shs 15,000 Kwa mfuko.
Kule china na India mfuko wa sement reja reja unauzwa kwenye shs 10,000 hivi za kitanzania.
Akili za matakoni ziko hivi..huyu anaweza jiuza ili ale maharage yaani tatizo alilo nalo anayemuona kwanza kulitatua ni jirani wakati yeye amelala usingizi..peculiar!
 
Kiongozi angesema yafanyike moja mbili tatu na angesema kuanzia kesho cement iuzwe shilingi fulani na ingeuzwa, kusema fulani na fulani wakae wazungumze washushe bei ni siasa.
..mwambie afanye hivyo kwa vifaa vyote vya ujenzi km unadhani ishu ni kutamka bei.
 
Hapana hakutaka Kuingilia mifumo alya wataalam, ndio Maana ameagiza waziri wa viwanda na biashara pamoja na Kamishina wa TRA hawa ni wadau Muhimu kwenye mchakato wa kushusha bei
Hakutaka kuingilia kwann sasa anasema ishuke. Hao mawaziri wa biashara si wapo na wanaona tu tangu inapanda hadi sasa?
 
Tatizo ni kodi lukuki kwa wawekezaji ndiyo inapandisha bei.Hapo njia ni kupunguza kodi na siyo kutamka matamko.Kipindi cha magufuli cement ilifika 8000 lakini alipoingia huyu mama imepanda hadi 25000
 
Makamu wa Rais wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ameitaka Wizara ya Viwanda na Biashara kukaa meza moja na wazalishaji wa saruji nchini ili kuweka mikakati ya haraka itakayohakikisha bidhaa hiyo inapatikana kwa wingi na kurejea katika bei nafuu ya awali.

Ndejembi ametoa agizo hilo jana jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utoaji wa Tuzo za Rais kwa Mzalishaji Bora Viwandani (President’s Manufacturer of the Year Awards - PMAYA), zinazoratibiwa na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI).

Katika tuzo hizo, Kampuni ya SILAFRICA Tanzania Limited imeibuka mshindi wa kwanza wa jumla, ikifuatiwa na Alliance One kama mshindi wa pili, huku Tanzania Cigarette PLC ikitwaa ushindi wa tatu.

Akieleza kero ya wananchi kuhusu gharama za ujenzi, Makamu wa Rais amebainisha kuwa Watanzania wanalazimika kununua saruji kwa bei kubwa kutokana na usimamizi na uratibu dhaifu wa uzalishaji viwandani, jambo ambalo linaenda kinyume na maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Sasa nakuagiza Waziri wa Viwanda na Biashara namwona hapa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kaeni pamoja mmalize hili suala ili Mtanzania apate saruji kwa bei iliyokuwepo. Nataka kupata ripoti ya suala hilo baada ya kikao hiki, mjadili na mwandike ripoti tumkabidhi Rais,” amesisitiza Ndejembi.

Akiangazia mwenendo wa uchumi, Makamu wa Rais ameeleza kuwa sekta ya viwanda imeendelea kukua, ambapo mwaka 2025 ilikua kwa asilimia 5.2 ikilinganishwa na asilimia 4.2 ya mwaka 2024, huku mchango wake katika Pato la Taifa ukifikia asilimia 5.9 na kuchangia takribani asilimia 12 ya ajira rasmi nchini.

Hata hivyo, ametoa rai kwa wamiliki wa viwanda kutojiridhisha na soko la ndani pekee, bali kuongeza ubora na tija ili bidhaa za Tanzania ziweze kushindana katika masoko ya Afrika Mashariki na duniani kote.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa CTI, Leodegar Tenga, ameeleza kuwa tuzo za PMAYA zinalenga kutambua mchango wa sekta ya viwanda na kuchochea ubunifu. Pia amesisitiza utekelezaji wa misingi ya uzalishaji endelevu unaozingatia mazingira, jamii na utawala bora (ESG), akitangaza kuanzishwa kwa Mabalozi 10 wa ESG watakaopimwa kwa mwaka mmoja.

Kwan majukum ya makam wa rais yalishabadilishwa? Najua alikuwa anashughulikia mazingira na mambo ya muungano.. hii ya sukari alikuwa waziri wa viwqnda na biashara pamoja na waziri mkuu.. au m ndo nmejivulugha?
 
Asijisahau sana, yeye kazi yake kubwa ni kukata utepe tu.
 
Makamu atazungumia vyote ila siku akibugi akazungumzia utekaji ameisha
 
Aagize pia na hela ziongezeke mifukoni, na simu ziite🐼
 
  • Kicheko
Reactions: Lax
Kwan majukum ya makam wa rais yalishabadilishwa? Najua alikuwa anashughulikia mazingira na mambo ya muungano.. hii ya sukari alikuwa waziri wa viwqnda na biashara pamoja na waziri mkuu.. au m ndo nmejivulugha?
Amesema "amelichomeka chomeka jambo hilo" kutokana na agenda iliyopo
 
Duh wanaona Watanzania wajinga sana.
 
Hiiiiii
 

Attachments

  • 1000024076.jpg
    1000024076.jpg
    45.1 KB · Views: 10
kheeee yani na yeye anaagiza loh kweli bongo bahati mbaya .alooooo.
 
Back
Top Bottom