Makamu wa Rais Ndejembi atembelea ubalozi wa Tanzania, Vienna

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433
Tarehe 16 Septemba 2026 Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius John Ndejembi alitembelea Ubalozi na Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Vienna. Wakati wa ziara hiyo, Mhe. Makamu wa Rais alisaini kitabu cha wageni, kupitishwa kwenye Ofisi za watumishi wa Ubalozi, na kuzungumza na maafisa Ubalozi.

Ziara ya Mheshimiwa Makamu wa Rais imefanyika pembezoni mwa Jukwaa la Kisayansi la Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomu (The IAEA Scientific Forum) lililofanyika tarehe 15 & 16 Septemba 2026 jijini Vienna ambapo Mheshimiwa Makamu wa Rais alimwakilisha Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Makamu wa Rais aliambatana na Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na wasaidizi wake.

Mheshimiwa Makamu wa Rais alipokelewa na Mheshimiwa Naimi S.H. Aziz, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Vienna na maafisa Ubalozi.

Tarehe 16 Septemba 2026 Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius.jpg

Tarehe 16 Septemba 2026 Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deograti...jpg

​
 
Tarehe 16 Septemba 2026 Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius John Ndejembi alitembelea Ubalozi na Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Vienna. Wakati wa ziara hiyo, Mhe. Makamu wa Rais alisaini kitabu cha wageni, kupitishwa kwenye Ofisi za watumishi wa Ubalozi, na kuzungumza na maafisa Ubalozi.

Ziara ya Mheshimiwa Makamu wa Rais imefanyika pembezoni mwa Jukwaa la Kisayansi la Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomu (The IAEA Scientific Forum) lililofanyika tarehe 15 & 16 Septemba 2026 jijini Vienna ambapo Mheshimiwa Makamu wa Rais alimwakilisha Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Makamu wa Rais aliambatana na Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na wasaidizi wake.

Mheshimiwa Makamu wa Rais alipokelewa na Mheshimiwa Naimi S.H. Aziz, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Vienna na maafisa Ubalozi.

well done Makamu wa Rais Deo Ndenjembi 🐒
 
Back
Top Bottom