Miluzi mingi naambiwa humpoteza mbwa. Kimya cha wahusika kuhusu hali ya jiwe kikichanganywa na miluzi inayopigwa kwa mfano hapa JF inatufanya hata ambao hatukutaka kufikiria nini kinaendelea tuanze kuwa na hofu. Jinsi siku zinavyokwenda na hakuna taarifa isiyo na shaka ni hali inayo ongeza wasiwasi. Si kawaida ya mheshimiwa "kupotea" kwa siku kadha, wanasema kuna ambao amewatumbua-lakini ajabu hujasikia wateule wana apishwa lini. Sasa kunakuja huu mkutano ambao yeye angehusika kama Mwalikwa mkuu na unafanyika hapa Dar badala yake Mama ndiye atakaemuakilisha. Kila moja la hayo niliyo yataja linaweza kuwa na jibu la kueleweka lakini ukiyaweka pamoja yanaleta shaka. Ukweli wanaujua wahusika lakini kama watanzania ni vizuri kukawa na uwazi vinginevyo wapiga miluzi watazidi kuwachanganya watanzania.