- Thread starter
- #21
Ibada hiyo pia imehudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Mawaziri pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiagana na na Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Mbeya Mhashamu Gervas Nyaisonga pamoja na Mapadre mbalimbali mara baada ya kushiriki Ibada ya kumuombea Baba wa Taifa Hayati Mwalimu. Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Francisko wa Asizi, Mwanjelwa Mkoani Mbeya leo tarehe 14 Oktoba 2025