Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 441
- 1,065
Kwa sehemu kubwa mahubiri ya viongozi wa haya makanisa hawakemei dhambi, hawasisitizi maadili wala kukemea mmomonyoko wa maadili unaolitafuna Taifa kwasasa
Injili yao ni ya miujiza, utajiri, kupiga wachawi, na zaidi zaidi "mahubiri yamekuwa ya kisela" na kueneza utamaduni wa "kisela"
Tofauti na madhehebu kongwe kama RC, KKKT, ADVENTIST, ISLAMIC, Anglican hata viongozi binafsi wa zamani kama kina Kakobe, Mwingira na Mwakasege, hawa wa siku hizi hautowasikia wanakemea dhambi, kusisitiza heshima wala kuogopa uovu.
Mahubiri yao yanawapa ujasiri watenda maovu (tumekatazwa kuhukumu ila nimekosa neno sahihi la kutumia hapa) kwamba wanaweza kuendelea na uovu wao na bado wakafanikiwa tofauti na tulivyohubiriwa zamani kwamba kamwe huwezi kuwa mtenda maovu na ukakubaliwa kwenye ufalme wa Mungu
Leo Makahaba, mashoga, mafisadi, wachawi, na kila aina ya takataka zote zinakimbilia huko na wamekuwa waumini wa makanisa hayo kwasababu huko hakuna anayewagasi gasi kwa kukemea matendo yao. Kinachoangaliwa ni ada za viingilio kwenye maombi na kuelezea unataka nini sio kiongozi anataka uache nini
Kwa kiasi kikubwa waumini wa haya makanisa hawaogopi dhambi tena. Hawana hofu na Mungu hataki nini tena bali mawazo na akili zao zinawaza mafanikio yao ya kimwili sio ya kiroho tena na hata viongozi wao msisitizo wao ni kutafuta pesa tu bila kujalisha njia utakayotumia kuzipata
Kuna kila sababu Makanisa haya kongwe ikiwemo na dini ya Kiislamu (kwani waumini wanaoenda huko wametoka humu) kukemea mambo haya na kuishinikiza serikali kuingilia kati usajili wa haya makanisa
Nachojiuliza ni kitu kimoja tu, kwani makanisa na misikiti iliyopo haitoshi? Kuna haja gani ya mengine kuongezeka?
Nadhani ili kurudisha hadhi ya Taifa, kuna haja ya kuangalia upya sheria za usajili wa haya makanisa. Mwenzetu Kagame amefanikiwa, huwezi kukuta upuuzi kama huu kwake, sisi tunashindwa nini?