Buenos Aires
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 1,894
- 1,622
Acha tu. Unaweza kulia.
Haya madisco kwenye kumbi za starehe na bar zinakera kwelikweli. Watu miaka nenda miaka rudi hakuna anayelalamika , watu wameridhika. Lakini linalohusu Mungu malalamiko ni mengi!!Kuna kanisa mtaa mmoja huku nilipo, Sijajua hawa ni walokole ama! Mtaa mzima hapa ni kelele kwenda mbele. Miziki inapigwa kama wako disco mazee! Aise wanakera mno na makelele yao, serikali naomba muwashugulikie hawa watu, tembeeni mikoa yote mpaka vijijini.
"serikali itembee mikoa yote hadi vijijini", unahisi kama serikali ni kikundi fulani cha watu kinachokaa sehemu fulani.Kuna kanisa mtaa mmoja huku nilipo, Sijajua hawa ni walokole ama! Mtaa mzima hapa ni kelele kwenda mbele. Miziki inapigwa kama wako disco mazee! Aise wanakera mno na makelele yao, serikali naomba muwashugulikie hawa watu, tembeeni mikoa yote mpaka vijijini.
Zile siku za mikesha sasa ndo unaweza kuweuka. Kila ukitafta usingizi hauji labda uwe umetoka job umechoka hasa kiasi ukipanda tu kitandani una kata moto ndo utaweza kulalaKwakweli kuna wakati wa ibada na kuna wakati wa kufanya mambo mengine, hii ya makanisa especially ya kilokole ni tatizo kubwa.
Hatukatai watu wasali, waabudu, waimbe na wamsujudie Mungu wanayemuamini Ila iwe na wakati maalum Ila wenzetu walokole wao hawana muda
REJEA?Kuna study ulifanyika Mwaka juzi watoto vijana na wazee wanaosali kwenye makanisa ya kipentecost walionekana Wana tatizo la masikio. Ngoma zao za masikio zimekakamaa na kupelekea kutosikia vizuri au kushindwa kunong'onezana.
Hii ni kwa sababu ya kiwango Cha sauti kuwa kikubwa zaidi 45db kwa muda mrefu hasa wakati wa ibada.
Hivyo kupelekea watu wengi kwenye kwenye makanisa hayo kuwa na tatizo la afya ya masikio.
Tuchukue tahadhari na haya makanisa yenye kufungulia sauti kubwa wawapo kwenye ibada.
Study hiyo ilionesha matokeo tofauti kwa makanisa ya Roman (RC), Lutheran (KKKT) Orthodox n.k
Aidha watu wanaoishi mazingira kuzunguka makanisa hayo ya kipentecost hasa watoto walionekana kuathirika pia hata wale wasiosali kwenye makanisa hayo.
Chukua hatua