Sol de Mayo
JF-Expert Member
- Sep 10, 2016
- 6,515
- 6,230
Sijui una laaana au stress za maisha kila kona tanzania kuna bar zinapiga mziki wa makelele na kukesha tuache bar misikiti inatoa hazana kila baada ya muda tena kwa kipaza sauti wew umeona makanisa tu.
Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Ulie ili iwejeAcha tu. Unaweza kulia.
Naitafuta nitaiweka hapaREJEA?
Natanguliza shukrani.Naitafuta nitaiweka hapa
Hah hah haha....Kuna kanisa mtaa mmoja huku nilipo, Sijajua hawa ni walokole ama! Mtaa mzima hapa ni kelele kwenda mbele. Miziki inapigwa kama wako disco mazee! Aise wanakera mno na makelele yao, serikali naomba muwashugulikie hawa watu, tembeeni mikoa yote mpaka vijijini.
NashangaaHaya madisco kwenye kumbi za starehe na bar zinakera kwelikweli. Watu miaka nenda miaka rudi hakuna anayelalamika , watu wameridhika. Lakini linalohusu Mungu malalamiko ni mengi!!
Hah hah haha....
Huzijui bar zenye kupiga makelele, magari ya matangazo, misikiti, kumbi za sherehe , kumbi za madisco nk.
Nchi yetu haina sheria ya kudhibiti mijikelele
Naomba kuuliza hivi haya mafundisho aliyafundisha Yesu ? Yaani vinanda,kuimba na yale yote yanayo patikana katika miziko hiyo iitwayo "Miziki ya Injili".Kuna kanisa mtaa mmoja huku nilipo, Sijajua hawa ni walokole ama! Mtaa mzima hapa ni kelele kwenda mbele. Miziki inapigwa kama wako disco mazee! Aise wanakera mno na makelele yao, serikali naomba muwashugulikie hawa watu, tembeeni mikoa yote mpaka vijijini.
Naomba kuuliza hivi haya mafundisho aliyafundisha Yesu ? Yaani vinanda,kuimba na yale yote yanayo patikana katika miziko hiyo iitwayo "Miziki ya Injili".
Shukrani.Yesu hajafundisha haya maujinga.
UNAKUTA HUMO NDANI WAMO WATU 20 TU WASIOHITAJI SPIKA KUELEWANA!
Shukrani.
Kazini kufanya nn Sasa na wanahudumu kwa bwana?!Wanaserebuka kwa Bwana Yesu, sema kila kitu lazima kiwe na limit, nadhani serikali pia inapaswa kuwawekea mipaka hawa watu maana wakati mwingine ni dico 24/7 mpaka huwa najiuliza hao waumini huwa wanaenda makazini saa ngapi
Naamini kanisa linatakiwa lifanye mambo ambayo yanavuta watu kwa Yesu, siyo yanayokera watu.Kuna kanisa mtaa mmoja huku nilipo, Sijajua hawa ni walokole ama! Mtaa mzima hapa ni kelele kwenda mbele. Miziki inapigwa kama wako disco mazee! Aise wanakera mno na makelele yao, serikali naomba muwashugulikie hawa watu, tembeeni mikoa yote mpaka vijijini.
Fikiria wagonjwa, watoto na wazee.Anayekereka na sauti za hayo makanisa azibe masikio ikiwezekana na tigo kabisa.
Hii dunia hatuwezi kufanana tuvumiliane tu.))
Kwangu wapo hao walokole na mikesha yao huku wakiliankwankutumia microphone....kuomba kwa kunena, na siku ya J2 usiombe....saa 12 asubuhi unaamshwa na mziki wao wa kelele.....mbaya zaidi wamejenga kwa mjumbe wetu wa nyumba kumi....kila tukilalamika hakuna kitu....nilichofanya nami ni kununua speaker zangu mbili na amplifier ya ukweli.....wakianza tu nami nalianzisha mara nne yao.....inabidi wazime kabosa.....sasa tunalala na kwa amani....tunaheshimiana.....Hili ni janga la taifa kwakweli,,,
Mwanzoni wakati sijapata hadha ya jambo hili nilikuwa naona watu wanaolalamika kuhusu kelele za makanisa ya kilokole kama ni watu wenye chuki za kidini. Mimi ni mkristo tena mpentecoste, fpct,
Lakini tangu mwezi wa tatu mwaka huu na Mimi nimeanza kuonja adha na madhila ya kuishi karibu na makanisa ya kilokole yenye makelele kupita kiasi.
Nimejenga karibu na kanisa la EAGT (Evangelist Assembles of God Tanzania) , mwanzoni wakati wa mchungaji wa zamani marehemu, walikuwa wanaabudu kwa ustaarabu bila makelele mengi au adha kwa majirani, hata wakipiga makelele basi ni jumapili tu au siku ya ijumaa ambapo ufanya mkesha basi.
Lakini tangu mchungaji huyo afariki dunia, kulitokea mabadiriko ya utawala na kugombania uongozi, waumini wengi walilihama kanisa hilo nawamekuja waumini wapya, sasa tangu hapo hatulali, kila siku ni kelele kubwa kupita kiasi mpaka huwezi kupumzika nyumbani kwako tena nikila Siku 24/7.
Mbaya zaidi wameanzisha utaratibu wa kuanza kufanya ibada usiku wa manane kuanzia saa kumi usiku (alfajiri) mpaka saa kumi na mbili na nusu asubuhi wakiita ibada ya "Morning glory" tena kwa makelele makubwa sana kiasi cha kufanya watu tunashindwa kulala usiku ukizingatia tuna watoto wadogo , wazee na wagonjwa! Tumeshawafuata na kuwaomba wafanye ibada zao kwa sauti ya wastani lakini wapi, ndio kwanza wanafungulia maspeakers mpaka mwisho!
Kiukweli hili jambo linaumiza sana akili na afya.mpaka wengine tulio na nyumba za kupangisha tunakimbiwa na wapangaji kwasababu ya kukwepa kelele za ibada!! yaani nyumba yako lakini unatamani kuhama kukwepa kelele!! Hata ningekuwa na uwezo wa kuibeba nyumba yangu nikaiweke eneo lingine ningefanya hivyo kukwepa makelele kupita kiasi!! Unaamka umechoka, una usingizi na kichwa kinauma kwa kelele za hao jamaa waliokesha usiku mzima!!
Kwanini haya madhehebu yanayotumia utaratibu huu wa ibada yasifungulie sauti ya wastani ili kutowabughudhi wakazi wanaozunguka kanisa husika?! Au watumie sound proof kupunguza kelele, hatukatazi wala hatuwezi kuzuia watu wasiabudu kwa imani yao lakini wasiwe kero kwa jamii inayozunguza nyumba zao za ibada, mbona wakatoliki, walutheri, waanglican na waorthodox hawasumbui watu kwa makelele kupita kiasi wanafanya ibada zao kistaarabu tu?! Kwani bila makelele kupita kiasi Mungu hasikii ibada yao?! Ajabu zaidi waumini wanakuwa humo ndani ni wanne tu! Lakini makelele ya maspeakers utadhani kuna mkutano wa adhara na watu laki mbili.
Jamanii eeh Uhuru wako unapoishia ndipo uhuru wa wenzako unapoanzia, tuheshimu faragha ya kupumzika kwa wenzetu, au tuwe kama Rwanda ambapo kagame alizuia kelele za aina hii?! Au wajenge mbali na makazi ya watu ili wapige kelele zao masaa 24/7 bila kuwasumbua watu hasa usiku wakati watu wamepumzika!
Hao wagonjwa wanaumwa nin? Icho ambacho awataki kusikia sauti au wazee wamezeeka nini? Icho acheni ushetani wa namuna iyo wafe ili wasisikie saut.Fikiria wagonjwa, watoto na wazee.