Makanisa Nchini Mjitafakari

Hao mruki wametumwa kuuchafua ukristo..sadaka tangu lini ikamfanya mtu awe masikini..mana unatoa kadri ya uwezo wako na ulivyobarikiwa..hakuna mtu anayekushikia bunduki ili utoe..mana sio lazima.

Huyo ni mamruki tu..wakupuuza.

#MaendeleoHayanaChama
Mtakuja Kukumbuka Kwamba Mlikuwa Mnawanufaisha Watu au Taasisi za Watu. Ndipo Mtakumbka

Hamtoi sadaka Tu ila Mnatoa Sadaka.. Shukrani...Harambee..Mnajenga...Michango kibao.. acha Kuudanganya Ubongo wako kwamba Eti natoa Sadaka Peke yake

Halafu kwa Vile Mshakuwa Brain Washed mnaambiwa Mnamtolea Mungu.
 
Utaratibu wa kurudisha zaka na sadaka ni Mungu mwenyewe kauweka kwa ustawi wa kazi Jambo la msingi ambalo ninalo ona hapa viongozi wa kidini waache kujitukuza wao wenyewebad
 
Mbona Hasira Lete Hoja yako. Ni Lazima Kwako na Familia yako Ili mmpigwe zaidi na Zaidi. Si mnadanganywa Zinaenda Kwa Mungu. Endeleeni kutoa Na Muwajemgee na Wachungaji wenu Nyumba na Magari Mnunue Ambayo yatakuwa Urithi kwa Watoto wao na Si Wewe
Wewe shida yako nini wakitoa hizo sadaka na zaka..walishakuja kwako kuomba chakula.

Wewe tunakupuuza tu...mana ni mamruki.

#MaendeleoHayanaChama
 
Wewe unamtolea shetani ama?..mambo ya imani kwako hayana maana..ila kwa wengine yana maana.

Hoja zako dhaifu sana na inaonekana umetawaliwa na chuki ama husuda dhidi ya ukristo...haitokusaidia kitu.

Hizo nguvu wekeza kukuza kipato na kusaidia familia yako.

#MaendeleoHayanaChama
 
Utaratibu wa kurudisha zaka na sadaka ni Mungu mwenyewe kauweka kwa ustawi wa kazi Jambo la msingi ambalo ninalo ona hapa viongozi wa kidini waache kujitukuza wao wenyewebad
Aliuweka lini huo utaratibu! Taratibu hizo zimewekwa na Sisi Binadamu ili tupige pesa. Hakuna Sehemu Mungu kkaandika Chochote kile wala kutoa masharti ya Zaka wala Sadaka
 
Ukifa Huwezi jua Ukweli.

Unakuwa Mfu na Kwenye Biblia si wameandika Wafu hawaongei wala Wasikii jambo Lolote kwahiyo huwezi Jua Ukweli ukifa. Utajua Ukweli ukiwa Hapa unaona na Kusikia
Sasa mbona na wewe mwenzetu hueleweki, hiyo biblia uliyo rejea hapa, ndio hiyo hiyo inazungumzia juu ya sadaka na mengine mengi! kwanini baadhi ya mistari ya bible uiamini na mingine usiiamini?
 
[Soma malaki 3:8-12 lakini pamoja na yote, haya ni mambo ya kiimani hakuna mtu atakulazisha kutoa ndio maana Mungu anasema tumjaribu whatever the case kama utaona kumtolea Mungu ni katika kuwasaidia wahitaji it is
ok maana neno lunasema anafurahishwa na wanaotoa kwa hiari .Broblem ambayo inafanya wengi wawe wanavunjwa moyo kutoa ni kuona viongozi wa makinisa wakijiabudu kwa kununua vitu vya anasa na huku wanajigamba kwa pesa ambazo sio malengo yake
QUOTE="FabNXTzqEtcgazfbjjfo, post: 41663093, member: 534375"]
Aliuweka lini huo utaratibu! Taratibu hizo zimewekwa na Sisi Binadamu ili tupige pesa. Hakuna Sehemu Mungu kkaandika Chochote kile wala kutoa masharti ya Zaka wala Sadaka
[/QUOTE]
 
Sasa mbona na wewe mwenzetu hueleweki, hiyo biblia uliyo rejea hapa, ndio hiyo hiyo inazungumzia juu ya sadaka na mengine mengi! kwanini baadhi ya mistari ya bible uiamini na mingine usiiamini?
Nimemrejea Biblia kwa Sababu ndio kitabu anachokiamini ili aweze elewa.
 
[Soma malaki 3:8-12 lakini pamoja na yote, haya ni mambo ya kiimani hakuna mtu atakulazisha kutoa
Huwa Unaenda Kanisani Ndugu!? Sadaka/Michango/Zaka/Bahasha/Harambee Siku hizi ni Za Lazima usipotoa Unakutana na Haya

1. Kususiwa Wewe na Familia yako
2. Watoto wako Kutobatizwa
3. Katika Jumuiya zao Watakutenga
4. Utaonekana mtu wa Hovyo

kama Sadaka zako unazipeleka Kwwa Binadamu mwenzako wahitaji wewe utaonekana Mbaya. Hautoi Sadaka Kwa Miungu ya Kanisani

ndio maana Mungu anasema tumjaribu
Ngoja Nikupe Mfano Kwenye Hiyo Hiyo Biblia. Aliyesema MSIMJARIBU NDIO HUYO HUYO ANASEMA MMJARIBU

Kumbuka hata Yesu Alipojaribiwa na Shetani Alisema Maneno hayo Kwamba USIMJARIBU BWANA MUNGU WAKO

Sasa Hamuoni Hapo Kwamba Mnachanganywa Ndugu zangu ma Mnapigwa. Maana Huyo huyo anasema Mmjaribu kwa Sadaka kwanini Aseme tena Mmjaribu wakati keshasema MSIMJARIBU




Kwanza Unatakiwa kuelewa kwamba Mungu hatolewi chochote kile. Unapotoa Kitu Mfano msaada Haumpi Mungu unampa Binadamu mwenzako. Na ndip Kitu Mungu ametuwekea Akilini Tusaidiane sisi kwa Sisi.

Unaposema Nimemtolea Mungu Maana Yake Mungu ni Dhaifu anahitaji Kitu ndio akamilike. Yaani Usipompa Kitu Hakubariki anakupa Ma laana . Hizo ni Tabia za Kibinadamu si Mungu.


Mungu wa Kweli haitaji Sadaka Wala Zaka.
 
Wewe shida yako nini wakitoa hizo sadaka na zaka..walishakuja kwako kuomba chakula.


Tunaishi nao na Ndio Walishawahi kuja Kuomba. Na Wakitafuta Wao wenyewe Wanazipeleka kwa Wachungaji wao Kama Sadaka. Ni Upungufu wa Akili Timamu

Wewe tunakupuuza tu...mana ni mamruki.

#MaendeleoHayanaChama

Unaona Hivyo kwa Sababu kuna Kitu Kinakuuma Sana watu wasipoleta hizo Sadaka huko mliko. Maana Hadi Mmejiandikia Kwenye Biblia kuwa Mnakula Madhabahuni ili Mzidi wapotosha Waumini watoe zaidi wakidhani wanamtolea Mungu kumbe wanatolewa Viumbe Wa roho wa Mali
 
Jinsi ya Kuishi Kibinadamu na Kuishi Kama Mungu alivyokuumba. Moja Ya Viongozi Amepost hiki Kitu. Watu wanaweza Kukichukulia Poa. Ila Ujumbe wake ndani Una Maana Kubwa Sana Ya Kwanini Binadamu Tumeumbwa Hapa Duniani.

Mungu Alituumba Si Tumpe Vitu(Sadaka,Zaka,Matoleo,Mbuzi, Ng'ombe) hapana. Alituumba Na Akili na Yeye Haitaji Kitu Chochote kile kutoka Kwako
 
Alafu na wale homeless kwanini wasingekuwa wanalala makanisani nauliza tuu. !!
 
Unalalamika kutoa kwa Mungu mbona kwa shetani mnatoa zaidi. Hakuna ibada bila sadaka, hata kwa shetani Ili upate utajiri ni lazima utoe sadaka
 
Tutumie Akili Timamu na Tumwabudu Mungu asiyetaka Vitu bali Aliyeumba Vitu vyote bila Yeye Kukutaka Kitu Chochote kile kutoka Kwako.
Umeongea Point kabisa.

Mimi nipo Ughaibuni; Ila nikiona information za watumish mabali mbali wa Africa especially my country Tz; Majority ya hao watumish hawawezi kufanya Kazi nje ya Africa? Mfano US, Europe maana Kuna mahali mtu anakila Kitu gari nzuri, nyumba, kazi nzuri, watoto etc Unafikiri utampelekea preaching za Utapata mali, utapata gari etc? mtu ana kila kitu? hapo inaonyesha inabidi wabadilike,

Mambo ya Mali mtu yoyote mwenye mipango thabiti anaweza kupata, wajikite kufundisha Kiini cha imani wanazohubiri.
 
Ungeweza eleza Mada hii kwa kurejea biblia huenda ningekuamini... Mimi ni muumini na najua ninachotoa ni kwa Mungu hata kama mchungaji atakula au atahonga, kazi yangu ni kumtii Mungu nibarikiwe. Ufalme wa Mungu unaongozwa na kanuni.. MALAKI 3:8 Mungu anasema tumtolee ili atubariki period. Hapa hamaanishi anashida na Mali au fedha zetu.. Hapa a nataka utii wetu hata katika mambo aliyotubariki.. Ili tusijivune na kutumia kuharibu Jina lake.. Bali tuwe tayari kumtumikia kwa Mali zetu kuujenga Ufalme. Watu wa Mungu hawawezi barikiwa kwa kutoa zaka kwa yatima tu.. Bali katika kila eneo tulioagizwa na Mungu.

Mungu hawezi bariki watu bila kupitia watu. Ukitoa kwa yatima utabarikiwa kwa utii wako ktk Hilo.. Bali Ukitoa katika madhabau hama zaka na sadaka.. I po Baraka yake pia kama alivosema ktk MALAKI 3.8.
Kumbuja ibada kamili ni Ile inayofanyika mbele ya Madhabau, inayoongozwa na kuhani na yeye kutolewa sadaka.
Mfumo huu uko hata kwa wachawi na waganga, mganga ndio kuhani, kilinge ndio madhabau na sadaka ndio kuku, njiwa au hela unayotoa ili upate tiba. Kama unataka maombi yajibiwe na Mungu.. Lazima ukamilishe ibada.. Sadaka ni lazima.. Uwe na njaa, una kazi shauri yako.. But kanuni lazima ifuatwe ili ukutane na Mungu ktk ibada.

Soma neno ujue kweli, utakua huru na chiki na wachungaji na mafanikio Yao acha a navyo.. Maana hata wao watatoa hesabu ya sadaka mbele za Mungu, usipoteze muda kudhibiti sadaka.. Sio kazi yako.

Neno, Neno la kristo ndio taa!! Barikiwa Sana mwana WA Mungu!
 
Mistari yako ni sawa, kwahiyo Mungu ni ni hao wachungaji wanaopokea sadaka?
 
Haya ni mapokeo ambayo binafsi sijui mwisho wake utakuwaje, nimekuwa nikijiuliza hizo sadaka Mungu huwa ana fanyia nini? kama anauhitaji nazo yeye anashindwaje kuzipata wakati yeye ndiye amekuumba na kukuwezesha kuzipata? yeye ninini kimemshinda mpaka akusubiri mvuja jasho wewe umtafutie ndiyo umpelekee! Na kuna baadhi ya Manabii wanawaaminisha waumini wao kununua bidhaa wanazo wauzia kwa kuwaaminisha kwamba ni za upako na ulinzi kwao, wakati Nabii mwenyewe halindwi na hizo bidhaa? akiumwa anaenda Hospitali na kuhusu ulinzi kutwa anazunguka na ma bouncers!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…