Green Beret
JF-Expert Member
- Apr 22, 2022
- 631
- 991
Wanafanya hivi kwa sababu wanaume zao hawamjui Mungu.Wahanga ni Wanawake wanahisi hao ma Pastor ni Mungu wengine wanapika wanawapelekea msosi.
Adamu ndie alipewa neno halisi na Mungu akaambiwa amfundishe Eva. Mwanaume ndie kichwa ila wengi wanatumia kichwa kidogo kuliko kikubwa.
Biblia inasema haya juu ya Ibrahim. Alibarikiwa na Mungu kwa sababu hii:
Mwanzo 18:17 Bwana akanena, Je! Nimfiche Ibrahimu jambo nilifanyalo,
18 akiwa Ibrahimu atakuwa taifa kuu, hodari, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa?
19 Kwa maana nimemjua ya kwamba atawaamuru wanawe, na nyumba yake baada yake waishike njia ya Bwana, wafanye haki na hukumu, ili kwamba Bwana naye akamtimizie Ibrahimu ahadi zake.
Wababa wangapi hapa JF wanakaa chini kujifunza Neno la Mungu na kumfundisha mke wake na watoto wake??? Kama hufanyi hivyo lazima mke akimbilie huko makanisani maana sketi za mtaa zitakupepeta kama ngano
Wanawake wengi wanaenda huko maana wanaume wao wana vimada wanawatesa kuwatukana na kuwanyanyasa na kutelekeza familia baada ya kuwarubuni na kuwatumia!!!
Hii ni failure ya wanaume. Wanaume wakimjua Mungu watatiisha familia yao katika kumcha Mungu na hii kimbia kimbia ya wanawake makanisani itaisha.