Makanisa yazingatie umuhimu wa Sunday Schools kwa watoto wa umri mdogo na wa kati

Makanisa yazingatie umuhimu wa Sunday Schools kwa watoto wa umri mdogo na wa kati

Mr Pixel3a

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2021
Posts
5,710
Reaction score
8,579
Baadhi ya makanisa kupuuzia Sunday schools kwa watoto na kuwa na utamaduni wa kuwachanganya watoto na watu wazima haimjengi mtoto kimaadili, kidini, kisaikolojia na kiufahamu pia. Maana kuna mahubiri mengine yanaleta matokeo hasi kwenye ubongo wa mtoto.

Mtoto lazma afundishwe katika ranks na apate walimu wazuri wa kidini kila Jumapili ama siku za ibada.
 
Watoto wana mafundisho yao kulingana makuzi yao, kuwachanganya na watu wazima hawataelewa kitu, haya mafunzo husaidia sana kukua ki maadili wanapokuwa watu wazima wanakuwa na hofu ya kutenda dhambi. Watu wazima ambao hawakupitia huko kuwafundisha imani mpaka wakue kiimani ni shughuli pevu kwa wachungaji.
 
Mmetoka kwenye makanisa ya msingi mmeenda kwa wapigaji halafu mnawapangia?? Katoliki, Lutheran,Anglican, morovian sunday school zipo na mafundisho ya kipaimara kwa watoto. Huko kwingine pambaneni na hali zenu
 
Back
Top Bottom