Nadhani Mwanza ni ideal kuwa mako makuu, sababu ni nyingi sana.
1. Hari ya hewa inaridhisha si baridi wala joto, moderate unaweza vaa suti yako mwaka mzima
2. Uzuri wa jiji lenyewe kwa uwepo wa miundo mbinu yote ya mji mkuu na maarufu.
3. Maji siyo shida kama Dsm, Dodoma, Tanga au Arusha, kwa maana ya maji ya ziwa victoria.
4. Uwepo wa hospitali kubwa ya rufaa tangu siku nyingi a next hosp to Muhimbili.
5. Ukarimu na upole wa wakazi wa mwanza, yani Wasukuma, wakerewe na wakara.
6. Uwepo wa uwanja wa ndege unaofanyakazi miaka yote
7. Mji uliopambwa na vilima na mawe
8. Uwepo wa ziwa victoria kutoa maji, samaki, usafiri na pia beach za kupumzika baada ya kazi
9. Jiji ambalo lina eneo la kukuwa(expansion) na jiji ambalo lina maeneo prime ya kukaa viongozi kama Isamilo na Capripoint ( maeneo ya kihistoria kukaa viongozi)
10. Maeneo ya utalii kama bujora na visiwa vya sanane, serengeti n.k
11. Uwepo na mahotel ya kisasa yamesheheni mwanza.
Nadhani Mwanza inajitosheleza haiitaji kujengwa upya kama ilivyokuwa kwa Dodoma au miji mingine
Nawasilisha Wakuu