Makapuku Forum

[emoji599] Mambo ni moto. Manchester United na Arsenal huenda zikapangwa kwenye makundi magumu zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambapo droo ya upangaji wa hatua hiyo ya makundi utafanyika leo Alhamisi Monaco, Ufaransa.
.
Utaratibu wa upangaji wa makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya unakuwa na vyungu vinne (Pot), ambapo zinawekwa timu na kuchaguliwa mojamoja na kupata kundi lenye timu nne. Kwa ujumla wake timu zipo 32, hivyo zitaunda jumla ya makundi nane.
.
Arsenal na Man United zote zimepangwa kwenye Pot 2, hivyo zitakuwa na kibarua cha kumenyana na mwamba yeyote aliyewekwa kwenye Pot 1 isipokuwa Man City tu ambayo wanacheza kwenye ligi moja, Ligi Kuu England na hatua hii ya makundi timu za ligi moja haziruhusiwi kukutana.
.
Hali ilivyo, kwenye Pot 1, kutakuwa na timu mabingwa wa ligi za ndani pamoja na bingwa wa Europa League kwa msimu uliopita, hivyo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu wa 2023-24, chungu hicho kitakuwa na timu za Manchester City, Sevilla, Bayern Munich, PSG, Barcelona, Napoli, Benfica na Feyenoord.
 
Manchester united imedhamiria kuwa na Sofyan Amrabati lakini kikwazo ni Financial Fair Play hivyo inawalazimu kuomba wampate kwa mkopo kitu ambacho Fiorentina hawataki ,mchezaji mwenyewe anahitaji kusajiliwa moja kwa moja .

Saga bado gumu
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa imemuhukumu Cyprian Kasuva kifungo cha miaka 80 jela kwa kosa la kukutwa na makosa matatu, kosa la kwanza kukutwa na nyara za Serikali (kichwa cha Tembo na meno yake), kosa la pili kukutwa na silaha (Magobole matatu) na kosa la tatu kukutwa na risasi 35.

Cyprian(44) Mkazi wa Kalenga Iringa Vijijini inadaiwa alitenda kosa hilo May 09, 2022 katika eneo la Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambapo akiwa anabanika nyama ya Tembo, Askari wa Wanyama Pori wakafanikiwa kumkamata.

Kosa la kukutwa na kichwa cha Tembo na meno yake hukumu yake ni kifungo cha miaka 30 au faini ya shilingi milioni 348, kosa la kukutwa silaha (Magobole matatu) hukumu yake ni kifungo miaka 25 na kukutwa na risasi 35 hukumu yake ni kifungo miaka 25 na hivyo kufanya jumla ya makosa yote kupewa hukumu ya kifungo cha miaka 80 ( anaitumikia kwa pamoja )

Kesi hiyo imesomwa na Hakim Mkazi Mkuu Said Ally Mkasiwa na ilikuwa na Mashahidi 6 huku ikisimamiwa na Mwendedha mashtaka wa Serikali Barton Mayage, Mahakama ilipompa nafasi ya kujitetea Cyprian aliiomba kupunguziwa adhabu kwasababu ni kosa lake la Kwanza na ana Watoto watatu wanamtegemea lakini hata hivyo akahukumiwa miaka 80.
 
Mkazi wa Dar es salaam aliyejitambulisha kwa jina la Mussa Mawa amekamatwa katika maeneo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili akituhumiwa kutapeli Wananchi wanaopata huduma akijifanya Daktari.

Mkuu wa Idara ya Ulinzi Alfred Mwaluko amesema kuwa wana usalama walimbaini Mtu huyo akiwa kwenye harakati za kuwatapeli Watu wanaouguza ndugu yao aliyelazwa jengo la Mwaisela.

Tukio hili limemfanya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano Muhimbili Aminiel Aligaesha kutoa rai kwa Watu wote wanaojihusisha na kutapeli Wananchi katika eneo la Hospitali kwamba kwa sasa ulinzi umeimarishwa na wakijaribu kufanya hivyo watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya usalama.
 
Rais Samia amefanya uteuzi wa Watanzania wanne kuwa waajumbe wa Tume ya Mipango.

Wajumbe walioteuliwa ni Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu, Balozi Ombeni Sefue, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanesco na Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandela, Omar Issa.

Wengine ni Balozi na Mjasiriamali Ami Ramadhan Mpungwe, na Meneja Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Cambodia Maryam Salim.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…