Makapuku Forum

Makapuku Forum

Viongozi wa kijeshi waliochukua madaraka nchini Gabon wamemtangaza Mkuu wa Kitengo cha Walinzi wa Rais, Brice Clotaire Oligui Nguema kuwa Kiongozi wa mpito nchini humo, kwa mujibu wa ripoti za Vyombo vya Habari, Nguema ni Binamu wa Rais aliyeondolewa madarakani Ali Bongo.

@DWKiswahili_ imeripoti kuwa saa chache baada ya Viongozi wa kijeshi kutwaa mamlaka, Rais Ali Bongo alionekana kwenye ukanda wa video akiomba kusaidiwa ambapo amewataka Raia wa Gabon "kupiga kelele" na kueleza kuwa amezuiliwa kinyume cha sheria katika maakazi yake.

Jeshi la Gabon limesema Bongo anatuhumiwa kwa uhaini mkubwa.
Screenshot_20230831_180401_Instagram.jpg
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewahukumu aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Dk John Pima na wenzake wawili kifungo cha miaka 20 jela baada ya kukutwa na makosa ya uhujumu uchumi.

Hukumu hiyo imetolewa leo Alhamisi Agost 31, 2023 na Hakimu Seraphin Nsana, katika kesi namba 5/2023 ya uhujumu uchumi, iliyokuwa inawakabili Dk. Pima, aliyekuwa Mweka Hazina wa jiji la Arusha, Mariam Mshana na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji, Innocent Maduhu.

Akisoma hukumu hiyo ya kesi namba 5/2023, mbele ya mahakama hiyo, Hakima Nsana amesema kuwa baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili, mahakama imewatia hatiani washtakiwa katika kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inawakabili.

"Kwa kuzingatia maombi ya mawakili wa upande wa washtakiwa, ikiwemo kutokuwa na rekodi ya makosa ya nyuma, utegemezi wa familia na ushirikiano mlioutoa katika kipindi chote cha uendeshaji wa kesi hii, mahakama inawapa adhabu ya kutumikia miaka 20 jela huku miezi 14 mliokuwa kizuizini ukizingatiwa," amesema

Mbali na hilo, washtakiwa wana haki na nafasi ya kukata rufaa katika Mahakama Kuu endapo hawajaridhika na hukumu hiyo.

Screenshot_20230831_180514_Instagram.jpg
 
Moto uliozuka katika jengo la ghorofa tano katika jiji la Johannesburg, Afrika Kusini, umesababisha vifo vya zaidi ya watu 70, huku wengine wengi wakijeruhiwa.

Kwa mujibu wa mtandao wa DW, moto huo umetokea katika jengo lililopo katika eneo lenye shughuli nyingi za kibiashara la jiji hilo kubwa la Johannesburg.

DW imeripoti kuwa taarifa ya msemaji wa Kitengo cha Huduma za Dharura cha jiji hilo, Robert Mulaudzi, amesema moto huo pia umesababisha watu wengine takriban 52 kujeruhiwa.

Hata hivyo Mulaudzi amesema idadi ya vifo inaweza kuongezeka zaidi kwa kuwa jitihada ya kutafuta miili ya watu kutoka ghorofa moja kwenda nyingine inaendelea.

Hata hivyo pamoja na hiyo, msemaji huyo amenukuliwa na vyombo tofauti vya habari nchini Afrika Kusini, ambapo amesikika akisema jengo hilo lililowaka moto, lilikuwa limetelekezwa ila limefanywa makazi kwa wasio na malazi.

Msemaji Mulaudzi amenukuliwa akisema wanaendelea na shughuli za uokoaji katika jengo hilo.

"Mara tu tunapomaliza, tunakabidhi eneo la tukio, kwa polisi kuendelea na kazi yao," alisema Mulaudz.

Eneo hilo la kati la Johannesburg limekuwa na majengo yaliyotelekezwa au kuanza kubomoka na mara nyingi yanatumiwa kama makazi na watu wenye shida ya malazi.
Mamlaka ya jiji huyataja aina hiyo ya majengo kama "majengo yaliyotekwa nyara," duru zinaeleza jengo hilo lilikuwa na wakazi takribani watu 200.

Shuhuda mmoja ambae anaishi karibu na jengo hilo amekiambia kituo kimoja cha televisheni nchini Afrika Kusini kuwa wakati moto ulipoanza, alisikia sauti ya vilio vya watu vya kuomba msaada, wakisema "wanakufa".

Hadi wakati huu chanzo rasmi cha moto huo, bado hakijajulikana na maafisa wanaendelea na uchunguzi wao.

Lakini Afisa mmoja wa Serikali za mitaa katika eneo hilo, Mgcini Tshwaku, amesema inaonekana kama kuna mkazi mmoja aliwasha moto kwa lengo la kupasha joto makazi yake ili kujikinga na hali ya baridi kali.

Screenshot_20230831_180616_Instagram.jpg
 
Baraza la Madiwani, Halmshauri ya Siha, mkoani Kilimanjaro, limeomba taarifa mbali mbali zinazoletwa kwenye baraza hilo zije kwa lugha ya Kiswahili, ili wajumbe waweze kuchangia kwa mapana yake bila kukwama.

Hatua hiyo imekuja baada Diwani wa Viti Maalumu, Lilian Mollel, kutaka kufahamu ni lini taarifa zinazokwenda kwenye baraza hilo, zitapelekwa kwa lugha ya Kiswahili, ili kila mjumbe wa baraza hilo, aweze kuchangia bila kukwama kutokana na kutokuwa na uelewa wa lugha inayotumika.

Wakizungumza kwenye baraza hilo maalumu ambalo linajadili ufungaji wa hesabu za halmshauri kwa mwaka 2022 na 2023, wamesema ni muhimu taarifa kuwa katika lugha ya Kiswahili ambayo madiwani wengi wanauelewa nayo na kimsingi ndiyo wanaendeshea vikao vyao.

Wamesema Serikali kila siku inapigia debe kuhusu kukua kwa lugha ya kiswahili duniani na kwamba baadhi ya nchi wameaanza kufundisha lugha hiyo, hivyo wanadhani siyo jambo jema kwa taarifa kuendelea kupelekwa katika baraza hilo zikiwa zimeandikwa kwa kiingereza.

“...sasa bado wanatuleta taarifa kwa lugha ya kiingereza jambo linaleta usumbufu usio wa lazima, kwa muda mrefu taarifa zimekuwa zikija kwa lugha ya kiingereza hata leo, kitu ambacho wakati mwingine imekuwa kikwazo kusoma taarifa na kuilewa hivyo wakati mwingine kikao kushindwa kufikia malengo ya kikao,” amesema na kuongeza;

"Ni kweli...hii lugha wakati mwingine inaleta sintofahamu, tuletewe lugha ambayo kila mtu anaweza kusoma na kuelewa," amesema Diwani Lilian.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo, Dancani Urasa, amesema: “Nafikiri taarifa zije kwa mfumo wa lugha ya kiswahili, hata kipindi cha nyuma tulishasema taarifa zije kwa lugha hiyo ya Kiswahili, hii inarahisisha kazi.”

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji (DED) wa Halmashauri hiyo, Naomi Swai amesema jambo hilo litfanyiwa kazi.

"Mawasiliano ni pale ambapo anayetoa taarifa na anayepokea taarifa wanaelewana, na sasa nchi yetu na nchi nyingine Duniani, kiswahili kinashika kasi sana, na sisi lazima tuendelee kukikuza na kukitangaza," amesema Naomi.
Screenshot_20230831_180713_Instagram.jpg
 
Unaweza kusema Baraza la Mawaziri nchini Burkina Faso, ni kama limewasha taa ya kijani ambayo inairuhusu Serikali ya nchi hiyo, kupeleka wanajeshi wake Niger, ili kusaidia masuala mazima ya ulinzi na usalama nchini humo.

Hatua hii pia inatizamwa kama njia ya kuimalisha usalama wa Burkna Faso, ambao ni majirani na Niger, nchi ambayo jeshi lilimwondoa madarakani Rais Mohamed Bazoum takriban mwezi mmoja uliopita.

Mtandao wa AA umeandika kuwa, taarifa ya Baraza la Mawaziri Jumatano jioni imesema, “kutokana na mipango ya kimkakati ya nchi yetu," Serikali imeruhusiwa kupeleka kikosi cha kijeshi nchini Niger.

"Bila ya kuchochea vita, ni lazima ieleweke kwamba jambo hili lifanyika kwa kuwa ni wajibu wetu kuzuia, na kwa maslahi bora ya mapambano yetu dhidi ya ugaidi, na haya ndiyo matarajio makubwa ya watu wa Burkinabe," amesema Waziri wa Ulinzi Kanali Meja Kassoum Coulibaly, na kuongeza;

"Kinachoathiri usalama wa Niger kimsingi kinaathiri usalama wa Burkina Faso."

Wiki iliyopita, utawala wa kijeshi wa Niger uliidhinisha wanajeshi kutoka nchi jirani za Mali na Burkina Faso kuunda jeshi moja la Niger iwapo kutatokea uvamizi wa kijeshi.

Vitisho hivyo, vilikuwa vimetolewa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (Ecowas), kwamba ingetuma vikosi vyake iwapo wanajeshi hao hawatarejesha utawala wa kiraia wa Rais aliyepinduliwa Mohamed Bazoum.

Niger ilitumbukia katika machafuko Julai 26 wakati Jenerali Abdourahamane Tchiani, kamanda wa zamani wa walinzi wa Rais, alipoongoza mapinduzi ya kijeshi yaliyomwondoa Rais Bazoum.

Wanajeshi wa Burkina Faso na Mali wametangaza kuungaji mkono utawala wa kijeshi nchini Niger.

Screenshot_20230831_180802_Instagram.jpg
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema mkoa huo upo kwenye mpango wa kuziondoa shule za sekondari za kutwa ili kuongeza ufanisi kwenye elimu.

Akizungumza leo Alhamisi Agosti 31, 2023 wakati wa hafla ya kutambua mchango wa wadau kwenye sekta ya elimu Chalamila amesema suala hilo lipo kwenye vipaumbele vya elimu vya mkoa.

“Vipaumbele vyetu katika mkoa ni kufuta shule za kutwa kwa sekondari ili wanafunzi waweze kufundishwa katika mazingira mazuri.

“Tunataka wanafunzi wote wawe kwenye shule za bweni na hili tutalifanya taratibu tukiamini kwamba tukifanikisha hilo wanafunzi watakuwa katika mazingira mazuri ya kujifunza na kufundishika,” amesema Chamalamila.

Mkuu huyo wa mkoa amebainisha kuwa kwa sasa mkoa wake unatakeleza miradi ya elimu yenye thamani ya Sh85 bilioni kwa shule za msingi na sekondari.
Screenshot_20230831_180909_Instagram.jpg
 
Mkazi wa Mtaa wa Kivukoni mjini hapa, Lockman Abubakar (21) ameuawa kwa kuchomwa kisu kifuani na kijana mwenzake walipokuwa wakidaiana Sh5,000 ambayo ni malipo ya mgawo wa kuchuna ngozi mifugo katika machinjio ya Serikali yaliyopo Mpomvu.

Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Safia Jongo akizungumzia tukio hilo jana, alisema lililotokea Agosti 27, 2023 katika eneo la machinjio wakati vijana hao wakifanya kazi ya kuchuna ngozi mifugo.

“Saa nne asubuhi kwenye machinjio ya Serikali yaliyopo Mpomvu kata ya Mtakuja, mwanamume wa miaka 21 alifariki dunia baada ya kuchomwa kisu kifuani upande wa kushoto na kijana mwenziye mwenye miaka 21 pia, mkazi wa Tambukareli,” alidai Kamanda Jongo.

Alidai kuwa chanzo cha mauaji hayo kilitokana na Abubakar kumdai mwenzake amlipe Sh5,000 zake baada ya kupokea malipo ya kuchuna ngozi mifugo, ndipo ukatokea mgogoro uliosababisha achomwe mara mbili kifuani na mwenzake huyo kwa kutumia kisu alichokuwa akikitumia kuchunia ngozi.

Alisema Abubakar alipoteza maisha muda mfupi alipokuwa akipelekwa hospitali kwa matibabu na polisi wanamshikilia mtuhumiwa kwa taratibu nyingine za kisheria.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Kivukoni, Gidion Alli aliwataka vijana kuepuka hasira zinazosababisha kuchukua sheria mkononi na kusababisha vifo au majeraha.

Jirani wa marehemu, Judith Mathias alisema tukio hilo linashangaza kwa kuwa ni kijana asiye na mgogoro na watu. "Hili tukio la kikatili linapaswa kukemewa na watu wote, pia nawaomba vijana wajifunze kuwa na subira.
Screenshot_20230831_181010_Instagram.jpg
 
Watu 19, wakiwamo askari polisi sita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa tuhuma za kujeruhi na kusababisha vifo vya watu wawili katika purukushani kati yao na wasafirishaji mkaa eneo la Kiluvya.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia juzi, wakati polisi hao walipokuwa wakiwazuia watu waliokuwa wakitumia bodaboda kusafirisha mkaa kinyume cha sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Agosti 29, 2023, kamanda wa polisi wa kanda hiyo, Jumanne Muliro alisema mbali na askari sita, wamo wengine 11 wa Kampuni ya Ulinzi Pasco LTD na maofisa wawili wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).

Tukio hilo limetokea ikiwa imepita miezi kumi tangu Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge kumweleza Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango hatua mbalimbali zinazochukuliwa na mkoa huo katika kuwadhibiti wasafirishaji mkaa ili kuondoa changamoto ya upungufu wa maji kwenye Bonde la Mto Ruvu unaosababishwa na shughuli za kibinadamu.

Jana, kamanda Muliro alisema juzi saa nane usiku wakati maofisa hao walipokuwa katika shughuli zao za kikazi zinazotokana na misitu, walikutana na watu 30 wakiwa na pikipiki wamebeba mkaa.

“Wakawasimamisha wakakaidi, ikaanza purukushani kubwa katika eneo lile, baadhi ya watu hao walilazimishwa kusimama lakini waliacha pikipiki zao wakakimbia na baadaye baadhi yao walirudi na kuwarushia mawe maofisa hao,” alisema kamanda Muliro.

“Baada ya kundi lile kurudi, wale maofisa walikuwa na silaha wakafyataua risasi ambazo baadaye uchunguzi ulibaini watu wawili walijeruhiwa na wakapoteza maisha wakiwa wamepelekwa hospitali ya Mloganzila.”

Alisema miili ya watu wawili ambao wamepoteza maisha kutokana na purukushani hizo majina hayajatambulika na ipo Hospitali ya Mloganzila kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Screenshot_20230831_181057_Instagram.jpg
 
Mahakama Kuu imewaachia huru washtakiwa wanne, waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka ya kumuua Mchungaji wa Kanisa la Pentecoste Assemblies of God Tanzania (PAGT), Wilaya ya Chato, Mathayo Kachilamwaka.

Mauaji hayo yalidaiwa kutokana na mgogoro wa haki ya kuchinja kati ya waumini wa dini ya Kikristo na Waislamu (ikiaminika kuwa wakichinja Waislamu Wakristo wanaweza kula hiyo nyama, lakini wakichinja Wakristo, Waislamu hawawezi kula) na kundi la watu wanaodaiwa ni Waislamu, walikuwa wakipinga kufunguliwa kwa bucha mahsusi kwa waumini wa Kikristo.

Siku ya tukio ilidaiwa kabla ya kufunguliwa kwa bucha hilo, waumini Wakristo walifanya mkutano wa injili Uwanja wa CCM Katoro, Chato na kutangaza watachinja nyama yao na kuiuza kwenye bucha maalumu.

Akitoa hukumu hiyo juzi, Jaji Kamana Stanley wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, alisema upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha shtaka la mauaji ya kukusudia dhidi ya washtakiwa na kuwaachia huru.

Walioachiliwa huru ni Abdulhamid Maarifa au Kishiga, Yusuph Matama au Abuu Hairat, Siraji Lumila na Khalid Sadick ambao walikuwa wanakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya kukusudia ya mchungaji huyo yaliyotokea Februari 11, 2013.

“Upande wa mashtaka una wajibu wa kuthibitisha kesi pasipo kuacha mashaka. Zaidi Kanuni ya asili katika sheria ya jinai kwamba mshtakiwa hawezi kutiwa hatiani kwa sababu ya udhaifu wa utetezi wake,” amesema Jaji Kamana.

Screenshot_20230831_181152_Instagram.jpg
 
Mfanyabiashara wa madini aliyetambuliwa kwa jina la Festo Marwa (55) na mtoto wake John Marwa wameuawa kikatili kwa kupigwa kichwani na kitu kizito chenye ncha kali.

Marwa na mwanawe ambao ni wakazi wa Kunduchi jijini Dar es Salaam, wamekutwa na umauti wakiwa katika kitongoji cha Mkerema Kijiji cha Lilondo, Halmashauri ya Wilaya ya Madaba mkoani Ruvuma.

Akitoa taarifa ya mauaji hayo jana Jumatano Agosti 30, 2023, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, ACP Marco Chilyaakati amesema John (mtoto) amekutwa na jeraha kubwa kichwani na uchunguzi wa awali unaonyesha kapigwa na kitu kizito chenye ncha kali kilichosababisha ubongo kutoka nje.

“Baada ya mauaji hayo, wauaji hao waliichukua miili yao na kuiweka kwenye gari la Marwa ambalo ni Jeep kisha wakalisukuma gari hilo hadi kwenye korongo,” alidai kamanda huyo.

Amedai lengo la kulisukumia gari hilo korongoni ni kutaka ionekane kuwa walipata ajali.

Hata hivyo, Kamanda Chilyaakati amesema makachelo walipolikagua gari hilo halikuwa limepata ajali.

“Baada ya kufanya utafiti tumefanikiwa kumkamata dereva aliyekuwa akiliendesha lile gari aliyetuambia kuwa baada ya tukio wenzake walimsindikiza hadi kituo cha mafuta kusudi aende polisi akatoe taarifa kwamba kapata ajali,” alidai kamanda Chilyaakati.

Amedai ili kupoteza ushahidi, dereva huyo alipigwa na kitu chenye ncha kali mguuni ili naye aonekana kapata majeraha kwenye ajali hiyo ya kutengeneza.

Anadai baada ya kumhoji alimtaja mtuhumiwa mwingine ambaye naye ametiwa mbaroni akihusishwa na tukio hilo.

Screenshot_20230831_181247_Instagram.jpg
 
Mfanyabiashara wa madini aliyetambuliwa kwa jina la Festo Marwa (55) na mtoto wake John Marwa wameuawa kikatili kwa kupigwa kichwani na kitu kizito chenye ncha kali.

Marwa na mwanawe ambao ni wakazi wa Kunduchi jijini Dar es Salaam, wamekutwa na umauti wakiwa katika kitongoji cha Mkerema Kijiji cha Lilondo, Halmashauri ya Wilaya ya Madaba mkoani Ruvuma.

Akitoa taarifa ya mauaji hayo jana Jumatano Agosti 30, 2023, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, ACP Marco Chilyaakati amesema John (mtoto) amekutwa na jeraha kubwa kichwani na uchunguzi wa awali unaonyesha kapigwa na kitu kizito chenye ncha kali kilichosababisha ubongo kutoka nje.

“Baada ya mauaji hayo, wauaji hao waliichukua miili yao na kuiweka kwenye gari la Marwa ambalo ni Jeep kisha wakalisukuma gari hilo hadi kwenye korongo,” alidai kamanda huyo.

Amedai lengo la kulisukumia gari hilo korongoni ni kutaka ionekane kuwa walipata ajali.

Hata hivyo, Kamanda Chilyaakati amesema makachelo walipolikagua gari hilo halikuwa limepata ajali.

“Baada ya kufanya utafiti tumefanikiwa kumkamata dereva aliyekuwa akiliendesha lile gari aliyetuambia kuwa baada ya tukio wenzake walimsindikiza hadi kituo cha mafuta kusudi aende polisi akatoe taarifa kwamba kapata ajali,” alidai kamanda Chilyaakati.

Amedai ili kupoteza ushahidi, dereva huyo alipigwa na kitu chenye ncha kali mguuni ili naye aonekana kapata majeraha kwenye ajali hiyo ya kutengeneza.

Anadai baada ya kumhoji alimtaja mtuhumiwa mwingine ambaye naye ametiwa mbaroni akihusishwa na tukio hilo.

View attachment 2734691
Huu ukatili mkubwa sana wa kukatisha maisha ya watu
 
Back
Top Bottom