Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20230901_072733_Opera%20Mini.jpg
 
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limetangaza kuwachukulia hatua ikiwemo kuwapiga faini hadi ya shilingi milioni tano Madereva na Abiria watakaojisaidia maarufu kama ‘kuchimba dawa" kwenye maeneo yasiyo rasmi baada ya mwezi mmoja wa kutoa elimu.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dr. Samuel Gwamaka ambaye ameziomba Halmashauri na Wajasiriamali kutumia changamoto hiyo kama fursa ya ujenzi wa vyoo ili kuepuka uchafuzi wa mazingira.

"Tutaoa hii elimu kwa muda wa mwezi mmoja na baada ya mwezi mmoja tutaanza kuchukua hatua tutakapokuta kwamba kuna basi lipo porini Watu wanachimba dawa tutatoa motisha kwa yule ambaye atakuwa anatutumia picha, wewe piga picha namba za hilo basi, piga picha ya ushahidi angalau Watu wanachimba dawa halafu tuletee sisi kama Baraza huyo mwenye Basi tutashughulika naye kwanza kwa kumpiga faini isiyopungua milioni tano”.

“Pia inaweza kuhusisha kwa kumnyang'anya leseni ya kuendesha Mabasi lakini adhabu zinaweza kwenda kwa pamoja kwahiyo kuanzia Oktoba 2, 2023 hatutegemei kuona basi linachimba dawa” ——— Dr. Gwamaka.
Screenshot_20230901_073829_Instagram.jpg
 
Tanzania kupitia Wizara ya Afya imewasilisha ombi kwa Waziri wa Afya wa Botswana, Dkt. Edwin Dikolot la kusaidia Nchi hiyo katika kuimarisha upatikanaji wa dawa, Waziri wa Afya Tanzania, Ummy Mwalimu akiwa Botswana amewasilisha hilo leo August 31, 2023 wakati wakijadiliana masuala ya upatikanaji wa dawa katika Nchi hiyo ya Botswana.

“Nimewasilisha ombi kwa Waziri wa Afya wa Botswana Mhe Dkt. Edwin Dikolot la kutaka Tanzania iweze kuisaidia Nchi hii katika kuimarisha upatikanaji wa dawa, Tanzania ina uzoefu wa kutosha katika ununuzi wa dawa ambapo imeingia mikataba na Wazalishaji wakubwa wa dawa Duniani wapatao 233”

“Kupiti mfumo huu Tanzania inaweza kununua aina za dawa tofauti 2209, Tanzania pia imepewa dhamana ya ununuzi wa dawa wa pamoja kwa Nchi mbili ambazo ni Commoro na Seychells, mpango huu ulifanikisha kupunguza gharama ya ununuzi wa dawa kwa 53% kwakuzingatia Azimio la SADC kwamba Bohari ya dawa ya Tanzania isaidie Nchi Wanachama katika upatikanaji wa dawa”

Kwa upande wake Waziri wa Afya wa Botswana Mhe, Dkt. Edwin Dikolot amemshukuru Waziri wa Afya Tanzania , Ummy Mwalimu kwa kuleta wazo hili na akaelekeza Taasisi ya dawa ya Botswana kuanza mazungumzo na Bohari Kuu ya Dawa ya Tanzania.
Screenshot_20230901_073925_Instagram.jpg
 
Waziri Mkuu, mstaafu Jaji Joseph Warioba ameeleza wasiwasi wake kuhusu hatua ya Serikali ya kutaka kuanza kutoa elimu ya Katiba Mpya kwa miaka mitatu, akisema ni muda mrefu kwa mchakato huo.

“Tumefikia mahali kama kuna utashi wa kisiasa, tunaweza kuamua juu ya haya mabadiliko, inanipa wasiwasi, ni kama tunataka kuanza upya mchakato huu. Unaona mijadala hii ya Katiba inavyoingilia shughuli zetu za maendeleo, nadhani imefika wakati tufanye uamuzi,” amesema Jaji Warioba.

Jaji Warioba ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, ameeleza hayo Ijumaa Agosti 31, 2023 katika mahojiano wa Azam TV yaliyofanyika nyumbani kwake wilayani Kinondoni, mkoani Dar es Salaam.

Juzi aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro, alisema watatoa elimu ya mabadiliko ya katiba kwa miaka mitatu, akisema kwamba utafiti walioufanya umeonekana kuwa zaidi ya asilimia 50 ya Watanzania hawaifahamu Katiba na hata wengine hawajawahi kuiona.

Kauli hiyo, Dk Ndumbaro iliwaibua wadau mbalimbali wakiwemo Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) na Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), waliokosoa hatua hiyo, wakisema inalenga kuchelewesha mchakatao huo.

Katika maelezo yake, Jaji Warioba amesema wakati akiwa mwenyekiti wa tume hiyo, wananchi walishiriki na walitoa elimu ya kutosha kuhusu Katiba Mpya, akisema walisambaza nakala za Katiba za Tanzania na Zanzibar.

Mbali na hilo, walifanya machapisho kueleza yaliyo katika Katiba na kusambamba katika maeneo mbalimbali ikiwemo vijijini, akisema kwa namna yanayoendelea hivi sasa huwezi kusema wananchi hawana elimu kuhusu mchakato huo.

“Kwa jinsi walivyoipanga sioni kama wanaweza kutoa mwanga zaidi kuliko walionao hivi sasa, Kamati ya Mukandala (Profesa Rwekiza), imechukua maoni ya kutosha na wananchi wanajua. Mimi natafsiri Serikali ingesema hatuwezi kupata Katiba Mpya sasa hivi, waseme mapema kuliko hivi,” amesema na kuongeza;
Screenshot_20230901_074851_Instagram.jpg
 
Ikulu ya White House ya Marekani, imesema kuwa Russia inaendelea na mazungumzo ya siri na Korea Kaskazini ili kupata risasi na nyenzo nyingine za kivita dhidi ya Ukraine.

Mtandao wa BBC umeripoti kuwa msemaji wa usalama wa taifa hilo, John Kirby, amesema kuwa pamoja na vifaa vya kijeshi, Moscow inaweza pia kuingia katika mikataba ya kununua malighafi ili kuipatia sekta yake ya ulinzi.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield alizikosoa Russia na Korea Kaskazini.

“Katika harakati zake za kutafuta silaha hizi, Russia itakiuka maazimio ya Baraza la Usalama, yakiwemo yale ambayo Urusi yenyewe iliyapigia kura.

Mkataba wowote wa silaha kama huo utakuwa ukiukaji mkubwa wa azimio la Baraza la Usalama lililopitishwa kwa kauli moja baada ya majaribio ya nyuklia ya Korea Kaskazini na kurusha makombora ya balestiki," Linda Thomas-Greenfield amesema.

Screenshot_20230901_075009_Instagram.jpg
 
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ameungana na watu mbalimbali kuomboleza vifo vya zaidi ya watu 70, vilivyotokana na kuungua kwa jengo la ghorofa tano jijini Johannesburg, akisema kuwa ni janga kubwa.

Ikiwa ndiyo tamko lake la kwanza kulitoa hadharani kufuatia tukio hilo la moto, mtandao wa BBC umemnukuu Rais huyo akiwa katika ziara jimbo la Eastern Cape akisema: "Tunaungana na watu waliopoteza wapendwa wao katika na janga hili."

BBC imeeleza kuwa kati ya waliofariki, wamo watoto saba, miongoni mwao, yumo mtoto wa mwaka mmoja.

Ramaphosa ameendelea kusema: “Tukio hili linatutaka sote kuwaombea walionusurika ili wapate utulivu wa kimwili na kisaikolojia, nina matumaini kwamba uchunguzi kuhusu moto huo utawezesha jamii na mamlaka kuzuia kutokea tena kwa janga kama hilo.”

Screenshot_20230901_075145_Instagram.jpg
 
Nchi za Rwanda na Cameroon zimefanya mabadiliko katika vikosi vya usalama na kijeshi.

Jana Jumatano Rais wa Cameroon Paul Biya mwenye umri wa miaka 90 alifanya mabadiliko makubwa katika wizara ya ulinzi ya nchi hiyo.

Miongoni mwa nyadhifa alizozifanyia mabadiliko ni pamoja na mjumbe wa kiti cha Urais anayeshughulikia ulinzi, wafanyakazi wa jeshi la anga, jeshi la wanamaji na polisi.

Biya aliyeingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka wa 1982, ni miongoni mwa marais waliokaa madarakani muda mrefu zaidi barani Afrika.

Nako nchini Rwanda, Rais Paul Kagame amewateua majenerali wapya pamoja na kuwapandisha vyeo vya kanali maofisa wapya vijana. Mbali na hayo Kagame aliidhinisha kustaafu kwa maofisa 83 wakuu wa kijeshi.

Kagame mwenye umri wa miaka 65 amekuwa madarakani tangu mwaka 2000 akiwa miongoni mwa marais waliokaa muda mrefu.

Mnamo 2015, katiba ya Rwanda ilibadilishwa ili kumruhusu Kagame kubaki rais hadi 2034.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Cable, maamuzi ya Kagame na Biya kubadilisha wanajeshi wao yanakuja siku chache baada ya wanajeshi kunyakua mamlaka nchini Gabon.
Screenshot_20230901_075248_Instagram.jpg
 
[emoji599] Saa zinakimbia sana. Muda wa hukumu nao unakaribia. Leo saa 6:00 usiku, dirisha la usajili litakuwa linafungwa pale nchini England.
.
Mambo ni mengi na timu nyingi bado zipo kwenye harakati za kujenga vikosi vyao hususani Mashetani Wekundu Manchester United wenyewe watakuwa na kazi ya kuhakikisha wanakamilisha usajili wa beki wa kushoto ama kiungo mkabaji. Kikosi hiki ambacho kipo chini ya Erik Ten Hag kina changamoto ya eneo la beki wa kushoto baada ya kuumia kwa Luke Shaw na Tyrell Malacia.
.
United iko mbioni kumsajili beki Sergio Reguilon kutoka Tottenham kwa mkopo wa ili akacheze eneo hili ama inaweza ikawachukua Rico Henry wa Brentford. Kwenye upande wa kiungo United ipo kwenye hatua za mwisho kumsajili staa wa Fiorentina, Sofyan Amrabat.
.
United pia inaweza kutangaza kukamilisha uhamisho wa golikipa wa Fenerbahce, Altay Bayindir ambaye ataenda kuwa mbadala wa Andre Onana.
Screenshot_20230901_075347_Instagram.jpg
 
HATIMAYE kinda wa Barcelona, Ansu Fati amejiunga na Brighton kwa mkopo wa msimu mzima bila ya kipengele cha kununuliwa huku akiwa amebakiza mkataba wa miaka minne.
.
Brighton ambayo itashiriki michuano ya Europa League msimu huu, Uhamisho huo umeshtua mashabiki kufuatia kauli ya Rais wa Barcelona, Joan Larpota aliyesisitiza kwamba kinda huyo hataondoka msimu huu.
.
Fati amelazimika kuondoka kutokana kukosa namba ya kudumu kikosi cha kwanza. Fati anaamini kwamba kocha wa Barcelona, Xavi alimpotezea na alidhihirisha baada ya kuingizwa katika dakika ya 79 katika mchezo wa ufunguzi wa LaLiga dhidi Getafe mwezi uliopita.
.
Fati aliichezea Barcelona kwa mara yake ya kwanza mwaka 2019 akiwa na umri wa miaka 16 na kuweka rekodi LaLiga ya kuwa mfungaji kinda zaidi alipofunga bao dhidi ya Real Betis.Pia aliweka rekodi ya kuwa mfungaji mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya Ligi ya Mabingwa Ulaya alipofunga dhidi ya Inter Milan mwaka 2020.
Screenshot_20230901_075440_Instagram.jpg
 
JINI

Premier League Player of the Season.
Premier League Young Player of the Season.
Man City Player of the Season.
FWA Footballer of the Year.
PFA Players’ Player of the Year.
UEFA Men’s Player of the Year.

Mnahesabu hizi ?
Screenshot_20230901_080322_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom