Makapuku Forum

Makapuku Forum

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limetangaza kuwachukulia hatua ikiwemo kuwapiga faini hadi ya shilingi milioni tano Madereva na Abiria watakaojisaidia maarufu kama ‘kuchimba dawa" kwenye maeneo yasiyo rasmi baada ya mwezi mmoja wa kutoa elimu.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dr. Samuel Gwamaka ambaye ameziomba Halmashauri na Wajasiriamali kutumia changamoto hiyo kama fursa ya ujenzi wa vyoo ili kuepuka uchafuzi wa mazingira.

"Tutaoa hii elimu kwa muda wa mwezi mmoja na baada ya mwezi mmoja tutaanza kuchukua hatua tutakapokuta kwamba kuna basi lipo porini Watu wanachimba dawa tutatoa motisha kwa yule ambaye atakuwa anatutumia picha, wewe piga picha namba za hilo basi, piga picha ya ushahidi angalau Watu wanachimba dawa halafu tuletee sisi kama Baraza huyo mwenye Basi tutashughulika naye kwanza kwa kumpiga faini isiyopungua milioni tano”.

“Pia inaweza kuhusisha kwa kumnyang'anya leseni ya kuendesha Mabasi lakini adhabu zinaweza kwenda kwa pamoja kwahiyo kuanzia Oktoba 2, 2023 hatutegemei kuona basi linachimba dawa” ——— Dr. Gwamaka.View attachment 2735265
Ila huo ni uonevu mkubwa kabisa. Au Atoto una maoni gani?
 
Screenshot_20230901_084639_Instagram%20Lite.jpg
 
Back
Top Bottom