Makapuku Forum

Makapuku Forum

Madereva wa pikipiki maarufu kama Bodaboda wakiwa kwenye foleni leo Jumanne Septemba 5, 2023 katika kituo cha mafuta wilayani Handeni mkoani Tanga wakisubiri huduma kutokana na uhaba wa mafuta.
Screenshot_20230905_151726_Instagram.jpg
 
Mahakama ya Wilaya ya Mufindi, imemhukumu Mbogo Tinda (45), Mkazi wa Kijiji cha Ihoanza Tarafa ya Malangali, wilayani hapa, kutumia kifungo cha miaka 20 gerezani, baada ya kumtia hatiani kwa makosa mawili.
Makosa hayo ni lile la kukutwa na nyara za Serikali (nyama ya tandala – kudu, yenye uzito wa kilo 32), lakini pia kujihusisha nyara za Serikali bila kuwa na kibali.

Hukumu hiyo imetolewa jana September 4, 2023; na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Benedict Nkomola, ambapo imedaiwa mshtakiwa huyo alipatikana na nyama ya tandala yenye thamani ya Sh7, 859, 136 milioni.

Akisoma shtaka hilo, hakimu huyo amesema mnamo August 26, 2023 katika Kijiji cha Idope, Kata ya Ihoanza, wilayani hapa, mshtakiwa huyo alikutwa na nyama ya Tandala ambayo alikuwa anaiuza bila kuwa na uhalali wa kufanya shughuli hiyo.

Inadaiwa kuwa mshtakiwa alinunua na kuuza nyama ya tandala kilo 32, yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha ambayo ni mali Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kuwa na vibali au leseni ya kuuza nyama hiyo.

Pia hakimu huyo amesema kosa hilo ni kinyume na kifungu namba 86(1) (2) (a) na kifungu (3) cha sheria ya uhifadhi wa wanyapori sura 283 rejeo la Mwaka 2022, ikisomwa pamoja na aya ya 14 Jedwari la kwanza la vifungu vya 57(1), na 60 (1) (2) vya sheria ya makosa ya uhujumu uchumi na makosa ya kupangwa, sura 200 rejeo la Mwaka 2022.

Aidha katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 11, 2023; mshtakiwa alikiri kutenda makosa hayo, ndipo mahakama ikamtia hatiani na kumhukumu kwenda jela miaka 20 kwa kosa la kwanza na pili ambapo adhabu hizo zitaenda sambamba.
Screenshot_20230905_151912_Instagram.jpg
 
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amesema kazi iliyo mbele yake ni kuhakikisha huduma ya nishati inawafikia wananchi wote na kwamba pamoja na kazi nzuri iliyofanyika ya kuimarisha sekta ya nishati, bado kuna nafasi ya kufanya ili nishati ya uhakika ipatikane.

“Kama watu hawapati umeme, kama watu hawapati nishati wanayoihitaji, hata tukivaa suti za namna gani tunakuwa hatuna maana na tutakuwa tunasemwa kila siku, kiu yangu ni kuona tunafanya kazi kwa viwango ili huduma ya nishati iwafikie wananchi wote,” alisema Dk Biteko.

Dk Biteko alisema hayo jana Jumatatu, Septemba 4, 2023 baada ya kupokewa rasmi na menejimenti na watumishi wa Wizara ya Nishati katika Ofisi za wizara hiyo zilizopo jijini Dodoma baada ya kuapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan kushika nyadhifa hizo.

Alitumia fursa hiyo kumpongeza aliyekuwa Waziri wa Nishati, January Makamba (ambaye sasa ni Waziri wa Mambo ya Nje) kwa juhudi alizofanya kuendeleza sekta hiyo na kuahidi utekelezaji wa miradi mbalimbali ya nishati ili nchi kuwa na nishati ya uhakika.

Pia, Dk Biteko aliongozana na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ambaye naye ameteuliwa na kuapishwa kuchukua nafasi ya Stephen Byabato aliyehamishiwa Wizara ya Mambo ya Nje akishughulikia masuala ya Afrika Mashariki.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba aliwapongeza Dk Biteko na Judith kwa kuteuliwa kwao na kuwakaribisha viongozi hao katika Wizara ya Nishati na kueleza wafanyakazi watatoa ushirikiano kwa viongozi hao ili kuweza kutekeleza majukumu yao kazi kwa ufanisi mkubwa.

Screenshot_20230905_152110_Instagram.jpg
 
Licha ya kuonekana wenye afya njema, Elikana na Eliudi Mwakyusa (10) maisha yao baada ya kutenganishwa hayajawahi kuwa sawa kwao kutokana na kushindwa kuzuia haja kubwa na ndogo.

Pacha hao wanashindwa kuzuia kwa kuwa hawaihisi pindi wanapotaka kujisaidia, changamoto hiyo inawanyima kujiamini na kushiriki masomo vizuri kama watoto wengine.

Pacha hawa waliozaliwa Februari 20, 2013 wakiwa wameungana huku wakitumia njia moja kujisaidia, walitenganishwa kwa mafanikio makubwa nchini India na sasa ni wavulana wakubwa wanaosoma darasa la tatu katika Shule ya Msingi Lubele wilayani Kyela, Mkoa wa Mbeya.

Kutokana na changamoto waliyonayo, mara kadhaa Elikana na Eliudi hulazimika kuacha masomo darasani na kurudi nyumbani baada ya kujisaidia, kwani licha ya kuvishwa pampers haja kubwa hutoa harufu inayowafanya wenzao wawatenge.
Screenshot_20230905_152443_Instagram.jpg
 
Rais wa China Xi Jinping huenda hatashiriki mkutano unahusisha nchi 20 tajiri duniani (G20) huku tetesi zikitaja mgogoro wa nchi hiyo na India inayoandaa mkutano huo kuwa sababu.

Kilele cha mkutano huo unaokutanisha nchi mashuhuri duniani kitafanyika wiki ijayo nchini India.
Endapo Rais Xi Jinping hatahudhuria basi uwezekano wa kukutana na mpinzani wake kiuchuni Rais wa Marekani, Joe Biden utakuwa mdogo.

Taarifa za ndani zinasema China itawakilishwa na Waziri Mkuu wake, Li Qiang huko jijini New Delhi kuanzia Septemba 9 hadi 10 mwaka huu.

Rais Xi mara ya mwisho alikutana na Biden katika mkutano wa kilele wa G20 huko Bali, Indonesia Novemba mwaka jana.
"Natumai atahudhuria," Biden aliwaambia waandishi wa habari Alhamisi Washington alivyoulizwa kuhusu ushiriki wa Xi Jinping.

Rais wa Urusi Vladimir Putin tayari amesema hatasafiri kwenda New Delhi na badala yake atamtuma Waziri wa Mambo ya Nje, Sergei Lavrov kwenda kumuwakilisha.
Screenshot_20230905_152611_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom