Makapuku Forum

🟨 KADI ZA REKODI
KULIKUWA na kadi za njano 44 zilizoonyeshwa kwenye Ligi Kuu England juzi Jumamosi na hivyo kuwekwa kwa rekodi mpya ya kutolewa kadi nyingi zaidi za njano ndani moja siku kwenye historia ya ligi hiyo ikivunjwa rekodi ya Agosti 22, 1998 ambako kulikuwa na kadi za njano 43 zilizoonyeshwa kwa siku hiyo.
 
Nyota wa Al Nassr, Cristiano Ronaldo ameripotiwa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Juventus ambayo haijamlipa mshahara wake wakati wa janga la Covid-19 mwaka 2020.
.
Straika huyo wa kimataifa wa Ureno anataka kulipwa Pauni 17.15 milioni kiasi ambacho aliahidiwa na klabu hiyo lakini klabu hiyo haikumlipa mshahara wake baada ya kukubali mishahara yao kusisitishwa hadi janga litakapokwisha.
.
Wachezaji wa Juventus walikubali kusitisha mishahara yao ya miezi minne kuanzia Machi 2020 hadi Aprili 2021 kutokana na klabu hiyo kuwa na matatizo ya kiuchumi katika kipindi hicho cha janga la Covid-19.
.
Sasa, Ronaldo ameamua kukumbushia na kutaka alipwe pesa zake na ameomba nyaraka husika kutoka kwa ofisi mwendesha mashtaka wa jijini Turin kwa mujibu wa Gazeti la Gazzetta Dello Sport la Italia.
 
Ushindi wa magoli mawili walioupata Yanga dhidi ya Al Merrikh unawaweka sehemu nzuri ya kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ambayo Yanga haijafika kwa muda mrefu [zaidi ya miaka 20].

Al Merrikh kutokucheza Khartoum, Sudan tayari ilikuwa ni faida ya kwanza kwao, waliowahi kufika Khartoum kwenye mechi za Al Merrikh watanielewa vizuri.

Kwa hiyo Yanga wamepata faida ya kucheza mechi ya ugenini kwenye ‘neutral ground’ lakini mashabiki wa Yanga wakaujaza uwanja na kuifanya Yanga kuonekana ipo nyumbani.

Faida nyingine kwa Yanga ni Al Merrikh kukosa mechi nyingi za ushindani kwa sababu Ligi ya Sudan imesimama kwa muda mrefu maana yake wachezaji wa Al Merrikh hawapati mechi fitness.

Sina hofu mechi ya marudiano Al Merrikh watapigwa tena Azam Complex na tutaishuhudia Yanga ikiikata ile kiu ya muda mrefu ya kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
 
Mechi za UEFA Champions League zinarejea tena wiki hii, bila shaka watanzania wengi wanasubiri kwa hamu mechi ya Shakhtar Donetsk dhidi ya FC Porto ili waweze kumshuhudia kijana wao Novatus Dismas.

Novatus mara baada ya kumaliza mchakato wa kujiunga na Shakhtar alijiunga na Taifa Stars kwa kuwa ilikuwa ni wiki ya mechi za kimataifa. Stars ilikuwa na mchezo wa kufuzu AFCON 2023 dhidi ya Algeria.

Mechi ya kwanza tangu ajiunge na timu hiyo ilikuwa juma lililopita ambapo alikuwa sehemu ya wachezaji wa akiba lakini hakufanikiwa kuoata nafasi ya kucheza mchezo huo.

Kwa hiyo tusubiri kuona kijana mwingine mtanzania akiingia kwenye rekodi za kucheza UEFA Champions League ambayo ni michuano mikubwa ngazi ya klabu katika bara la Ulaya.

Kumbukumbu zinaonesha kuwa Kassim Manara na Mbwana Samatta ndio watanzania waliowahi kucheza UEFA Champions League, kama Novatus atacheza basi atakuwa mtanzania wa tatu.
 
Messi ameongeza msisimko wa Ligi ya Marekani, mechi ambazo Inter Miami inacheza viwanja vinajaa! Ma-star wa Marekani ambao hawakuwa na utamaduni wa kwenda uwanjani siku hizi wanaenda na sababu kubwa ni Messi.

David Beckham amefanikiwa sana kibiashara baada ya kumsajili Messi.
 
Kwa uwekezaji ambao Simba wamefanya msimu huu [usajili, maboresho ya benchi la ufundi, pre-season] kama watashindwa kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, itakuwa ni hasara kubwa sana kwao.

Kwa hiyo wanatakiwa wafuzu hatua ya makundi halafu mambo mengine baada ya hapo yataji-set yenyewe. Hata wakishindwa kuendelea kutoka kwenye makundi kuna namna viongozi wakiongea na wanachama wanaweza kuwaelewa.

Wakitolewa kwenye hatua hii itabidi waitishe Mkutano Mkuu wa wanachama wawaambie bajeti ya usajili halafu timu imeshindwa kufuzu hatua ya makundi. Halafu viongozi wajitathmini au kujiuzulu kabisa nafasi zao kwa hasara walioisababishia klabu.

- Alex Luambano | #HiliGame
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…