Baada ya Jean Baleke kupasia kamba mara tatu βhat-trickβ dhidi ya Coastal Union, amefikisha magoli matano [5] na kuongoza kwenye orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu ya NBC 2023|24.
Baleke amempita Feitoto ambaye alikuwa anaongoza akiwa na magoli matatu ambayo aliyafunga kwenye mzunguko wa kwanza wa Ligi Azam FC ilipocheza dhidi ya Tabora United mchezo ambao haukuchezwa kwa dakika zote 90 baada ya kumalizwa kwa sababu za kikanuni.
MAGOLI MATANO YA JEAN BALEKE
[emoji460]οΈ[emoji460]οΈ[emoji460]οΈ vs Coastal Union
[emoji460]οΈ vs Dodoma Jiji FC
[emoji460]οΈ vs Mtibwa Sugar
Ikiwa Ligi ya NBC imechezwa kwa mizunguko mitatu, tayari wachezaji wawili wameshaondoka na mipira ya Bodi ya Ligi [Feitoto na Baleke] baada ya kila mmoja kufunga hat-trick!