Kiungo fundi wa soka anayekipiga Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amekiri wakati anajiunga na timu hiyo alikuwa chibonge, lakini kwa sasa amejitahidi kupambana hadi kukata zaidi ya kilo sita na kujiona mwepesi na kuanza kurejesha makali aliyokuwa nayo enzi akiitumikia Yanga.
.
Kiungo huyo alisema awali alipojiunga Azam alikuwa na uzito wa kilo 75, lakini baada ya kupigishwa tizi la maana kwa sasa amebaki na kilo 69 na kujiona mwepesi na kurejea kwenye ule utamu uliompa mashabiki akiwa na Yanga aliyoichezea misimu minne.
.
Fei alisema wakati anaanza kucheza alipata wakati mgumu sana, kwani alikuwa kibonge ila anamshukuru sana kocha kwani alimsaidia mno na kumrejeshea katika hali ya kuwa fiti. “Timu ilinipatia mkufunzi maalum wa kunifundisha mazoezi binafsi yalinisaidia kurudi katika hali, kwani nilikaa nje karibu miezi minne bila kucheza na kwa bahati nimepunguza uzito na sasa nimeanza kurejea katika makali niliyokuwa nayo Yanga,” alisema Fei Toto.
WAKATI makocha wengine wakikuna vichwa jinsi ya kuwatumia wachezaji, hali ni tofauti kwa Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi kwani licha ya kukabidhiwa kikosi msimu huu tayari asilimia 99 ya nyota wote 26 wamecheza michuano mbalimbali huku Dickson Job na Kouassi Yao wakifunika.
.
Yanga imecheza mechi tisa kwenye mashindano mbalimbali ikiwa ni pamoja na mchezo mmoja wa wiki ya Mwananchi ambao ulikuwa maalumu kwa ajili ya kutambulisha kikosi cha msimu huu. Katika mechi tisa, timu hiyo imefunga mabao 23 ikiruhusu nyavu zake kutikiswa mara moja.
.
Ushindi wa Yanga katika mechi zote hizo umechangiwa na kikosi chote kutokana na kocha Gamondi kutoa nafasi kwa kila mchezaji, huku kipa Abuutwalib Mshery akiwa ni pekee aliyekosa nafasi ya kucheza kutokana na kutoka kuuguza majeraha.
Zandani kutoka Simba kuwa Uongozi umeamua kumsuka staa Luis Miquisson ambaye ameanza kunoga kikosini amepewa ndinga kali ya kisasa, amehamishwa nyumba aliyokuwa amefikia pamoja na kukabidhiwa kwa mtaalamu spesho wa viungo kumnoa ili aendelee kumuweka fiti zaidi ya alipofikia sasa.
.
Habari zinasema kwamba Simba wamepania kuonyesha ukubwa na utofauti na mtani wao, Yanga, kupitia mashindano ya African Football League kwani tayari watani hao wote wako kwenye uwezekano mkubwa wa kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
.
Habari za uhakika zinasema kwamba tayari Luis yuko na mtaalamu huyo mwenye uzoefu mkubwa jijini Dar es Salaam na mbali na kufanya naye programu za kawaida kwenye timu huenda mbali zaidi baada ya muda wa kawaida na atakuwa naye mpaka wiki ya tatu ya Oktoba.
.
Arena express imejiridhisha kwamba Luis amekabidhiwa ndinga ya kisasa aina ya Crown New Model ya mwaka 2023 ambayo inakadiriwa thamani yake ni zaidi ya Sh100 milioni na tayari juzi na jana ameonekana nayo kwenye matizi kule Bunju.
.
Mbali na ndinga amehamishiwa kwenye nyumba ya kifahari maeneo ya Mbezi Beach Africana ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya mkataba wa pande zote na vilevile kuhakikisha anatuliza akili uwanjani na kurejesha makali yake kwa klabu msimu huu.
[emoji599] Moja ya vigezo vya CAF kwa nchi kuwa mwenyeji wa Afcon ni uwepo wa viwanja sita ambapo viwili viwe na uwezo wa kuchukua kila kimoja watu 40,000 na vingine viwili kila kimoja kiikichukua watu 20,000 na pia viwanja viwili kila moja kikiwa na uwezo wa kuchukua watu 15,000.
.
Hii ni kumaanisha kwa nchi tatu za Afrika Mashariki, kila moja lazima iwe na viwanja viwili vyenye hadhi ya kimataifa ingawa kwa Tanzania hilo halina shida kutokana na uwepo wa Uwanja wa Mkapa, Uwanja wa Amaan Zanzibar, Uwanja wa Azam Complex na marekebisho kidogo kwenye viwanja vya CCM Kirumba Mwanza, Sheikh Amri Abeid Arusha na vingine vingi.
Watu 52 wamefariki dunia baada ya kutokea kwa bomu na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa leo Ijumaa, Septemba 29, 2023 katika Mkoa wa Kusini Magharibi wa Balochistan nchini Pakistan.
Mlipuko umetokea wakati watu wakiwa wamekusanyika kusherehekea kumbukizi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W).
Serikali ya Pakistan kupitia Jeshi la Polisi imesema bomu hilo ni shambulio la kujitoa mhanga lililolenga mkusanyiko huo wa kidini na tayari maofisa wametangaza hali ya hatari huku majeruhi wakipelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu.
Matatizo ya moyo yanaongezeka kwa asilimia 25 hadi 30 kwa watu wanaofanyiwa uchunguzi wa afya na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo wanakutwa na matatizo hayo.
Hayo yamebainishwa leo Ijumaa Septemba 29, 2023 na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dk Angela Muhozya wakati akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam yakiwa na kaulimbiu ya tumia moyo wako kulinda moyo wako.