Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 154,929
- 459,607
Rais wa Rwanda, Paul Kagame amemteua aliyekuwa Ofisa Mkuu wa Jeshi, Jenerali James Kabarebe nchini humo kuwa Waziri wa Nchi kwa Ushirikiano wa Kikanda licha ya kwamba anashutumiwa kufanya kazi kwa karibu na kundi la waasi la DR Congo.
Jenerali Kabarebe ambaye kwa miongo kadhaa amekuwa mshirika wa karibu wa Rais Kagame, alistaafu jeshi mwezi uliopita.
Wataalamu wa Umoja wa Mataifa walichapisha ripoti mwezi Juni wakimtuhumu Jenerali Kabarebe kuwa na jukumu kubwa katika kuratibu operesheni za kundi la waasi la M23 mashariki mwa DR Congo huku Rwanda ikikanusha uvumi huo.