Makapuku Forum

NBCPL | FULLTIME

TANZANIA PRISONS 1-3 SIMBA
[emoji460]️ Said Ntibazonkiza 86’ [Pen]
[emoji460]️ John Bocco 45+1’
[emoji460]️ Clatous Chama 34’

[emoji460]️ Edwin Balua 12’
 
SportsXtra | @amrikiembatz

“Prisons waliuanza mchezo vizuri na kuwafanya Simba wasifurahie mchezo kwa dakika 20 za kwanza, lakini baada ya kupata goli nadhani ile nidhamu ya kuwaheshimu Simba ilianza kupotea. Kila mchezaji akawa anajihisi anaweza kufanya kitu kingine cha ziada.”

“Kuna mpango ambao Prisons waliingia nao kuutekeleza na walifanikiwa baada ya kupata goli kila mchezaji akaanza kuhisi Simba ni wepesi na anaweza kufanya anachoweza. Na hapo ndipo madaraja ya wachezaji yakaanza kuamua nini kitafanyika.”

“Kwa hiyo Prisons baada ya kupata goli utaratibu na mpango wa mwalimu ukawa haufuatwi kama walivyoingia kwa kuwaheshimu na kuonekana wapo imara sana.”
 
SportsXtra | @mastertindwa

“Ushindi na alama tatu ambazo Simba wamezipata dhidi ya Tanzania Prisons ni muhimu sana, zitawafanya watulie licha ya kwamba hakukuwa na vurugu wala ugomvi lakini kulikuwa na maneno na minong’ono kutoka kwa mashabiki kwamba inapata ushindi lakini haichezi vizuri.”

“Timu ambazo zinaonekana zinacheza vizuri Yanga ina alama tisa (9), Azam FC ina alama 10, Simba ina alama 12 na kuongoza Ligi kwa hiyo matokeo haya yatatuliza munkari wa mashabiki.”

“Sasa hivi Simba wataelekeza nguvu zao zote kwenye michezo inayofuta hususan dhidi ya Singida Fountain Gate [Ligi Kuu] na Al Ahly [African Football League] kuona watapataje matokeo ya ushindi.”

“Kama Simba isingepata alama tatu leo, yangesemwa maneno mengi sana lakini hayo yote hayana nafasi kwa sababu yanamezwa na ushindi.”
 
MATOKEO : 𝐅𝐔𝐋𝐋 𝐓𝐈𝐌𝐄

LIVERPOOL 2-0 UNION ST.GILLOISE
[emoji460]️ 45" Gravenberch
[emoji460]️ 90+1" Jota

ASTON VILLA 1-0 ZRINJSKI MOSTAR
[emoji460]️ 90" McGinn

AS ROMA 4-0 SERVETTE
[emoji460]️ 22" Lukaku
[emoji460]️ 46" Belotti
[emoji460]️ 52" Pellegrini
[emoji460]️ 56" Belotti

MOLDE 1-2 BAYER LEVERKUSEN
[emoji460]️ 87" Breivik

[emoji460]️ 14" Frimpong
[emoji460]️ 18" Tella

VILLARREAL 1-0 RENNES
[emoji460]️ 36" Sorloth
 
Farhan Jr

Kocha wa Simba sijui sababu zake ni nini kutompa nafasi HUSSEIN ABEL mbele ya Ayoub Lakredi, no doubt huyu ni Kipa wa maana tu na anaweza kufanya vitu vingi langoni tofauti na Kaka mkubwa pale, nadhani hii game ya leo anafaa kuanza, anafaa kupewa milingoti, he can perform better.

Moja kati ya Makipa Wazawa waliofanya kazi kubwa sana msimu uliopita kwa wanaotazama mechi tofauti na Simba na Yanga, nje na hapo ni ngumu kuelewana.

 
Farhan Jr

CHAMA'S FIRST LAW OF MOTION

If a body is at rest or moving at a constant speed in a straight line, it will remain at rest or keep moving in a straight line at constant speed unless it is acted upon by CLATOUS CHAMA

You are all experiencing greatness! Welcome to this MAGICAL 17 WORLD! Leo Kijana wangu anaamua yeye Simba icheze vipi na Prisons wakabe vipi na sio vinginevyo[emoji3]

 
Farhan Jr

SIMBA, wenyewe wanapaita Mbeya ni Green City lakini Simba wamepabadili na kuwa Red City! Wanapaita Sokoine lakini Simba wanapaita BUNJU B, mechi nyingine tena na alama nyingine tena tatu! Panaitwa Mbeya wengine wanaacha alama tatu, lakini Mnyama amerudi kambani mara tatu, ni football zaidi ya uchawi wa afu tatu.

SHOMARI KAPOMBE, mitaa ilikuwa inaimba apumzike! Leo kwenye siku nyingine ya sababu million kwanini ni Beki bora wa pembeni nchini, waambie sauti zao ziwe juu kama kelele za maneno yao, ukisikia We Zombie ujue ni Dangote, ukisikia nioneshe njia basi ni Show me the Way, Dani Alves wa Matombo, Morogoro.

CLATOUS CHAMA, the orchestra! Burudani baada ya Sikinde ya Shaban Dede, Baba ya football kama Msondo Ngoma Baba ya muziki, watoza ushuru ni TRA, wadahili vyuo ni TCU, bodi ya mikopo ni HESLB, lakini NECTA ya Viungo wote nchini ni CLATOUS CHAMA, hii ndio marking scheme ya mpira wa miguu nchini, wote wanamtazama kama Role Model, thats it.

EDWIN BALUA, Tanzania Prisons Cheat code! Stop that Homeboy, stop that! Unawakumbusha Mawakala kuwa Morogoro ina vipaji, waliposema ukuta ni wa Jeriko you screamed “Hold my beer” faulo moja ya maana Ally Salum aliruka kama Air Tanzania lakini anga la juu sio letu, mbavu ni zake na kifo kingekuwa halali yake, stop that Homeboy! Mguu bora zaidi wa kushoto ndani ya Sokoine leo hii.

JOHN BOCCO, Mfungwa mzoefu kwenye gereza la Sokoine, kila mwaka akihukumiwa anafahamu namna ya kutoroka, The Football El Chapo! Anabeba ngada ya mpira na anavuta sembe ya soka kuliko kuvuta subira, Captain alisema “I hear you” lakini wakumbushe watoto Form is temporary but class is permanent, fanya uwezalo ila Farhan hawezi kuwa Shaffih Dauda, note that.

WACHAMBUZI, leo Clatous Chama kwenye free role, anazunguka uwanja mzima kuliko Snura na kiuno chake, anaona kuliko Afande Sele na Darubini kali! Siku nyingine tena na homework nyingine tena, the greatest ever to do it! Vintage beyond forgery kwa sauti ya Peter Drury, the walking work of art.

 
Mchezaji wangu bora wa muda wote, NEYMAR JR aliibeba PSG mgongoni mwake mpaka fainali ya UEFA 2020, kwenye kiwango bora kabisa cha maisha yake na nadhani mtakumbuka nani alipoteza nafasi nyingi kwenye ile fainali mpaka Bayern akabeba taji.

Fundi halisi wa mpira ambaye dunia ina agenda nao the real football Artists kwakuwa hufundishwi academy kuwa Neymar, hufundishwi academy kucheza kama yeye bali unazaliwa nao na mitaa ya upako ardhi tukufu ya Brazil inakubariki.

PSG bila Mchezaji mkubwa kama Neymar ambaye anaweza kuifanya mechi kuwa vyovyote kwa namna yoyote huwezi kushinda big games, niambieni mechi ipi kubwa ambayo Neymar hajaperform! Kuanzia kombe la mabara, UEFA mpaka Copa America vs Argentina.

The greatest ever to do it! Nikitulia nitakuja na mpango wa siri na The New Football Order kutoka maabara moja nchini Marekani, nikitulia tu.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…