Makapuku Forum

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Jeshi la Kujenga Taifa, Askari mgambo pamoja na Vyombo vingine vya dola, imefanya operesheni maalum Mkoani Mara hususani katika Kanda maalum ya Tarime Rorya kwenye Bonde la Mto Mara.

Operesheni hii, iliyofanyika kuanzia October 02 hadi 08, imefanikisha uteketezaji wa jumla ya hekari 807 za mashamba ya bangi, ukamataji wa gunia 507 za bangi kavu iliyo tayari kusafirishwa, gunia 50 za mbegu za bangi pamoja na kuteketeza viwanda viwili vidogo vilivyokuwa vikitumika kuchakata na kufunga bangi kabla ya kusafirishwa ambapo Watuhumiwa 11 wanashikiliwa kuhusika na dawa hizo.

Akiongea katika tukio hilo, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amesema, wakazi wa eneo hilo wamelifanya Bonde la Mto Mara kama eneo maalum kwa ajili ya kilimo cha bangi na kujimilikisha kwa kutoruhusu Mtu yeyote asiye mkazi kuingia kwenye Bonde kama sehemu ya kuficha uharifu wao na wametishia kumdhuru yoyote atakayeingia ndani ya Bonde hilo bila ridhaa yao “Wamediriki hadi kufunga ofisi ya kijiji wakimtuhumu Mtenda wa kijiji cha Nkerege kutounga mkono kilimo cha bangi”

‘‘Sisi kama Mamlaka tutafanya operesheni endelevu katika maeneo haya kuhakikisha kilimo cha bangi kinaisha, Bonde hili lina rutuba nyingi na linakubali mazao ya aina zote, hivyo tumekubaliana na RC wa Mara kuwa na mikakati ya kusimamia Bonde ili kumaliza kilimo cha bangi na kutafutwa kwa shughuli nyingine ambayo itakuwa rafiki’’
 
Shirika la Bima la Taifa (NIC) leo limeingia mkataba wa miaka mitatu na Yanga SC kwa ajili ya kutoa tuzo ya Mchezaji bora wa mwezi wa Yanga (NIC Player Of The Month).

Mkataba huo wa miaka mitatu wenye thamani ya Tsh milioni 900 umesainiwa leo na Rais wa Yanga Eng. Hersi Said na Mkurugenzi wa NIC, Dr Elirehema Doriye mbele ya Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam.

“Hii ni nafasi kubwa kwa Wachezaji wa Yanga kuonesha uwezo wao ili mwisho wa mwezi waweze kutunukiwa tuzo ya Mchezaji bora wa mwezi”
 
Klabu ya Barcelona imepitia kipindi kigumu kiasi cha baadhi ya wachezaji kuwa wanaidai klabu hiyo yenye heshima kubwa Ulaya na nchini Hispania .

Taarifa kumuhusu Gerard Poque ni kwamba amesamehe mshahara wake kiasi cha €20m aliokuwa akiidai Barcelona

Hadi sasa ndio mchezaji pekee ambaye amefanya hivyo kati ya wachezaji wote wanaoidai Klabu
 
“Barcelona ni klabu bora na ni moja ya klabu kubwa zaidi duniani, nimekuwa nikiwafuatilia tangu nikiwa mtoto na nimekuwa nikipenda jinsi wanavyocheza “

“Tuna kocha anayejua aina hii ya soka, nilikuwa nampenda sana nilipokuwa mdogo hata safu ya kiungo iliyokuwa inanivutia ni ya Busquest, Xavi na iniesta”

Ikay Gundogan akielezea maisha ndani ya Barcelona chini ya Kocha Xavi Hernandez
 
Kuhusu mchezaji kamili anatakiwa kuwaje Kiungo wa Barcelona , Pedri amesema ;

" Mchezaji kamili anatakiwa kuwa na Kasi kama ya Kylian Mbappe, Mguu wa kushoto kama wa Messi, Mguu wa kulia kama wa Iniesta, Uwezo wa kupiga Chenga kama Ronaldinho, Uongozi kama wa Puyol na usahihi wa kupiga pasi kama Xavi Hernandez na Mashuti kama ya Messi"

 
Baada ya ushindi wake wa kwanza msimu huu dhidi ya Mtibwa Sugar, Kocha wa Tanzania Prisons Fred Felix Minziro amesema bado anaendelea kufanya marekebisho kwenye kikosi chake ili kupunguza makosa ambayo mara kadhaa yamewafanya waadhibiwe.

"Ligi ni ngumu na ina ushindani mkubwa. Kutengeneza timu si kazi rahisi, inahitaji muda kwa sababu kuna wakati wachezaji wanafanya makosa yanayojirudiarudia lakini sisi kama makocha hatuchoki tunaendelea kurekebisha makosa hadi timu itakaa sawa."

"Tutaendelea kupambana mwisho wa siku angalau tuweze kusogea nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi. Tutaendelea kujiimarisha kwenye eneo la ulinzi kuhakikisha hatufanyi makosa ya kizembe kwa sababu ukifanya makosa ya kizembe siku zote unaadhibiwa."
 
“Tunatazamia kutoka mikoa mbalimbali kufika kwenye mechi hii [Simba vs Al Ahly], ndio maana jana tulikuwa na mazungumzo na @airtanzania_atcl ili kupata punguzo la bei ya tiketi kwa mashabiki watakao safari kutoka mikoani.”

“Pia tutakuja na ofa kutoka kwa watu wenye vyombo vya usafiri [mabasi], kwa hiyo watu wenye vyombo vya usafiri ambao wangependa kuwa sehemu ya kampeni hii ya kusafirisha mashabiki wawasiliane nasi ili wawe sehemu ya kampeni hii kusafirisha mashabiki kutoka mikoani.”

“Lengo letu ni uwanja kujaa watu 60,000. Tunatarajia tiketi zitauzwa kwa haraka kwa hiyo tiketi zitatangazwa watu wanunue kwa haraka sababu tunatarajia kutakuwa na watu wengi kutoka nje ya Dar.”

- Imani Kajula, Mtendaji Mkuu Simba.
 
Serikali imeahidi kushughulikia changamoto ya umeme iliyopo nchini kwa kasi kubwa ili tatizo hilo liweze kuisha katika kipindi kifupi kuanzia sasa.

Hayo yameelezwa leo Oktoba 11, 2023 na Naibu Waziri Mkuu, Dk Doto Biteko katika mkutano mkuu maalum wa jimbo la Chalinze wa kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM (2020-2025) wilaya ya Chalinze mkoa wa Pwani.

Dk Biteko amesema katika kipindi cha miezi sita inayokuja ukosefu wa umeme nchini utaisha baada ya Serikali kuweka mikakati madhubuti ya kumaliza tatizo hilo nchini. Amesema watendaji wanafanya kazi ili Watanzania wapate umeme wa kutosha.
 
"Tumekuwa na sababu kadhaa ambazo zimetajwa na Ewura ambazo ni kupanda kwa gharama za mafuta sokoni, uagizaji mafuta, changamoto ya dola, kushuka thamani ya shilingi na sera za kikodi, uchambuzi wetu umeonyesha sababu hizi si za kweli.

Sera za kikodi na kuondolewa ruzuku ya Serikali na upungufu wa dola na kushuka thamani ya shilingi hizi ni sababu za kweli ambazo zimepelekea mafuta kupanda, yapo mambo ambayo yakifanyiwa kazi husaidia kupunguza, eneo la kwanza ambalo tuna mapendekezo ni hili la dola, ni kupunguza uagizaji wa bidhaa nje ya nchi," Msemaji wa sekta ya Nishati ACT-Wazalendo, Isihaka Mchinjita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…