Makapuku Forum

Makapuku Forum

"Kwakuwa tunakwenda kufanya jambo kubwa la kushiriki African Football League tukaona tuje na kitu kikubwa ambacho kitakuwa fahari kwa mashabiki wa Simba.

Leo ni siku ya uzinduzi wa jezi ambayo itatumika tarehe 20 Oktoba, 2023. Jezi zetu ni bora sana."- Mkurugenzi wa Sandaland Fashion Wear, Yusufu Omari.
Screenshot_20231012_133120_Instagram.jpg
 
"Leo ni uzinduzi wa jezi maalumu za AFL. Sandaland wameona tunavyokwenda kwenye sikukuu Wanasimba wasiende na jezi ya zamani, waende na jezi yenye hadhi. Watu wanatuonea donge sasa tunakwenda kuwaumiza tukiwa na jezi mpya."- Ahmed Ally. #AFL #WenyeNchi #NguvuMoja
Screenshot_20231012_133227_Instagram.jpg
 
"Tupo imara, kila Mwanasimba atekeleze majukumu ili tufikie malengo yetu na kufikia hatua nzuri. Sandaland amekuwa mfano mzuri wa kazi anayofanya, mdhamini mkuu M-Bet, makampuni ya Mo na wadhamini wengine wote."- Mwenyekiti wa klabu, Murtaza Mangungu. #AFL #WenyeNchi #NguvuMoja
Screenshot_20231012_133551_Instagram.jpg
 
"Tunaamini mwaka huu Wanasimba wameridhika na hata tukipita mtaani tunaona namna wamependeza na jezi zetu. Hongera Sandaland."

"Nafurahi kuwambia baada ya uzinduzi wa jezi hii, jezi zitaanza kupatikana kwenye maduka ya Sandaland. Leo wataanza kupendeza. Nawaomba Wanasimba wanunue na wavae hata wageni wakifika wajue nchi hii ni Simba."

"Tupo African Football League, tumewaacha wengine mbali. Muda ukifika pumba na mchele hujitenga."

"FIFA wameleta mashindano haya kwetu kwa kuangalia namna tunajaza uwanja itakuwa ni aibu uwanja usijae, nawaomba mnunue kwa wingi. Nataka kuona siku hiyo uwanja unatapika."

"Nashukuru serikali inayoongozwa na Rais wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kufanya marekebisho ya uwanja ule na kutumika kwa ufunguzi wa AFL. Wengine watautumia lakini sababu ya marekebisho ni Mnyama."- Mwenyekiti wa Bodi, @salim_tryagain. #AFL #WenyeNchi #NguvuMoja
Screenshot_20231012_133647_Instagram.jpg
 
"Tunaamini mwaka huu Wanasimba wameridhika na hata tukipita mtaani tunaona namna wamependeza na jezi zetu. Hongera Sandaland."

"Nafurahi kuwambia baada ya uzinduzi wa jezi hii, jezi zitaanza kupatikana kwenye maduka ya Sandaland. Leo wataanza kupendeza. Nawaomba Wanasimba wanunue na wavae hata wageni wakifika wajue nchi hii ni Simba."

"Tupo African Football League, tumewaacha wengine mbali. Muda ukifika pumba na mchele hujitenga."

"FIFA wameleta mashindano haya kwetu kwa kuangalia namna tunajaza uwanja itakuwa ni aibu uwanja usijae, nawaomba mnunue kwa wingi. Nataka kuona siku hiyo uwanja unatapika."

"Nashukuru serikali inayoongozwa na Rais wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kufanya marekebisho ya uwanja ule na kutumika kwa ufunguzi wa AFL. Wengine watautumia lakini sababu ya marekebisho ni Mnyama."- Mwenyekiti wa Bodi, @salim_tryagain. #AFL #WenyeNchi #NguvuMojaView attachment 2779864
Twende kwa Mkapa
 
Wataalam wa afya kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando (BMC) ya jijini Mwanza wametaja kuvaa miwani ya kusomea bila ushauri wala uthibitisho wa kitaalam na matumizi ya vipodozi vilivyoima muda wake kuwa miongoni mwa mambo 10 yanayochangia matatizo ya macho kwa watu wengi nchini.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Macho Duniani yaliyofanyika hospitaini hapo jana Oktoba 12, 2023, Mkurugenzi Mkuu wa BMC, Dk Fabian Massaga ametaja matumizi ya kompyuta bila tahadhari, uvutaji wa sigara na kutobadilisha mara kwa mara brashi za kusafishia uso kwa akina mama kuwa sababu nyingine zinazosababisha matatizo ya macho.

“Kutokula vyakula bora vinavyosaidia kurutubisha afya ya macho, kutofanya mazoezi na kutokuwa na utamaduni wa kupima macho mara kwa mara ni sababu nyingine inayosababisha matatizo ya macho,’’ amesema Dk Massaga

Mtaalam huyo ametaja mfumo wa maisha usiowapa watoto fursa ya kucheza ili kusaidia macho yao kuona mbali pia husababisha madhara kwa macho.

‘’Wazazi wawape fursa watoto wao kucheza nje kuwezesha macho yao kuona mbali badala ya kushinda ndani wakichezea simu na kutazama runinga,’’ ameshauri.

Screenshot_20231013_081742_Instagram.jpg
 
Kamati kutathmini ufanisi na utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imeshauri majukumu ya wizara hiyo kuhamishiwa kwa muda Ofisi ya Rais ili iweze kujengwa kikamilifu.

Mbali na kuhamishiwa ofisi hiyo katika kipindi cha mpito, pia wameshauri kubadilishwa kwa jina lake na kuwa Wizara ya Ushirikiano wa Kimataifa ikiwa ni hatua ya kuakisi azma ya Serikali ya kutumia diplomasia ya uchumi katika kujenga ushirikiano wa kimataifa.

Kamati hiyo iliyozinduliwa Machi 31, 2023; imetoa mapendekezo hayo wakati ikiwasilisha ripoti yake leo tarehe 12 Oktoba, 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Akisoma mapendekezo hayo, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Balozi Hassan Yahya amesema historia inaonyesha kuwa ujenzi wa wizara hiyo katika miaka ya awali, ulihitaji kuwa na wizara yenye hadhi maalumu ikiwa ni pamoja na kuhamishiwa au kuatamiwa chini ya mamlaka.

“Hatua hiyo iliiwezesha nchi kuwa na Wizara ya Mambo ya Nje madhubuti yenye maofisa wenye weledi na uwezo wa kusimamia ufanisi na maslahi ya nchi kimataifa,” amesema balozi Yahya.

Amesema wanadiplomasia mahiri kama Dk Salim Ahmed Salim ni miongoni mwa waliotokana na mfumo huo ambao ulijenga wanadiplomasia wa nchi hii.

Amesema kuhamishiwa kwa wizara hiyo chini ya ofisi ya Rais ni hatua ya mpito kunatokana na mabadiliko makubwa yanatotokea duniani na changamoto ambazo wizara hiyo imepitia huku akieleza kuwa kufanya hivyo kutaipa nafasi Serikali kuijenga upya na kuiimarisha kama ilivyokuwa miaka ya 1960 na 1970.

Screenshot_20231013_081849_Instagram.jpg
 
Shirikisho la Soka Afrika (CAF ) leo limepanga Makundi sita yenye Timu nne zitakazoshiriki michuano ya AFCON 2023 nchini Ivory Coast kuanzia January 13 2024.

Tanzania imepangwa Kundi F na Mataifa ya Morocco, Congo DR pamoja na Zambia na mechi zao zitachezwa katika Mji wa San-Pedro nchini Ivory Coast ambapo ni umbali wa Kilometa 337 kwa gari kutokea mji Mkuu wa nchi hiyo Abidjan.
Screenshot_20231013_082024_Instagram.jpg
 
Mtangazaji Mkongwe wa zamani wa BBC, Salim Kikeke @salim_kikeke amefikia makubaliano ya kufanya kazi na Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA).

Kikeke sasa atafanya kazi kama Mshauri wa Masuala ya Habari na Uhusiano wa ZIPA.

Kikeke amesema “Nimerejea Tanzania ili kusaidia Taifa langu kwa hali na mali, hii ni fursa ya kipekee kupata nafasi ya kuhusishwa kwenye sera ya Uchumi wa bluu ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dr Hussein Mwinyi”

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Salim Kikeke aliondoka BBC kwa hiari yake April 2023 na kuamua kurejea Tanzania baada ya kuitumikia BBC kwa miaka 20, alianza Mei 2003 na kuondoka April 2023.

Salim Kikeke sasa atafanya kazi kwa ukaribu na CEO wa ZIPA Shariff Shariff katika kuitangaza Zanzibar Kitaifa na Kimataifa.
Screenshot_20231013_082115_Instagram.jpg
 
Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila kwa mara nyingine kwa mafaniko makubwa kwa kushirikiana na Korea International Foundational for Health Care na Africa Future Foundation imefanya upandikizaji wa figo kwa Wagonjwa wanne (Wakiwemo watatu waliovaa barakoa pichani) ambao figo zao zimeshindwa kufanya kazi.

Upandikizaji huo ni wa kipekee nchini kwa kuwa umetumia utaalamu wa kisasa Duniani ambapo figo imevunwa kutoka kwa Mchangiaji kwa kutumia njia ya matundu madogo (Hand assisted Laparoscopic Donor Nephrectomy).

Akizungumzia upandikizaji huo katika hafla ya kuwaaga waliopandikizwa figo, Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi amesema utaalamu uliotumika kuvuna figo kwa kutumia matundu unafanyika Mloganzila pekee kwa Hospitali za Umma nchini na Afrika Mashariki na Kati.

“Kwa kutumia njia ya matundu mchangiaji anakuwa na kovu dogo, anakaa Hospitali kwa muda mfupi takribaini siku mbili hadi tatu kitu ambacho kinasaidia kupunguza gharama kwa Hospitali na Mchangiaji pia”

Prof. Janabi ameishukuru Serikali kwa uwekezaji ilioufanya ambapo amefafanua kuwa Mloganzila kuna vyumba vya upasuaji vya kisasa na vyumba vya uangalizi maalumu vyenye mashine na vifaa vya kisasa na pia kuna wataalamu bingwa na bobezi waliojengewa uwezo na Serikali katika nyanja tofauti tofauti.
Screenshot_20231013_082241_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom