Makapuku Forum

Takwimu mpya za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zinaonyesa ongezeko la asilimia 5 katika wastani wa kipato cha Mtanzania kwa mwaka ikichangiwa na kukua kwa uchumi wa kanda ya Dar es Salaam, kanda ya ziwa na kanda ya kaskazini.

Katika ripoti ya BoT ya ufanisi wa uchumi katika kila kanda iliyotolewa Oktoba 5 mwaka huu inaonyesha kuwa wastani wa kipato cha Mtanzania (GDP per Capita) mmoja mmoja kimeongezeka kutoa wastani wa Sh2.70 milioni hadi Sh2.84 milioni.

Wastani wa kipato cha wakazi wa Dar es Salaam kimeongezeka zaidi kuliko maeneo mengine ya nchi kutoka Sh4.81 milioni hadi Sh5.39 milioni mwaka 2022 sawa na ukuaji wa asilimia 12, hivyo ilikinganishwa na mwaka uliopita kila mkazi wa Dar es Salaam aliongeza Sh500, 000 katika mapato yake ya mwaka.
 
Hamis Said (37) mkazi wa Mtaa wa Nkokoto, Kata ya Igunga Mjini mkoani Tabora amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumpa ujauzito mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 16 (jina limehifadhiwa) anayesoma kidato cha pili.

Mwendesha mashtaka wa Ofisi ya Mkuu wa Mashitaka Wilaya ya Igunga, Albanus Ndunguru ameiambia mahakama mbele ya Hakimu wa Wilaya, Edda Kahindi leo Jumatano Oktoba 11, 2023 kuwa mshtakiwa huyo anashtakiwa kwa makosa mawili la kufanya mapenzi na binti yake wa kumzaa na kumpa ujauzito.

Baada ya kumsomea mashtaka yake, Ndunguru aliieleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuiomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kuanza kusikilizwa kwa hoja za awali.

Baada ya mshtakiwa kusomewa mashitaka hayo mawili alikana kutenda makosa hayo ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 20, 2023 na mshitakiwa amepelekwa mahabusu baada ya kukosa mdhamini aliyetakiwa kusaini dhamana ya Sh2 milioni.

 
Zikiwa zimesalia siku tisa kuelekea ufunguzi wa mashindano ya ‘African Football League’ katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo Simba itafungua pazia hilo dhidi ya Al Ahly, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Iman Kajula amesema mechi hiyo pia itahudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Gianni Infantino.

Pia Kajula amesema Infantino atakuwa sambamba na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Patrice Motsepe.

"Rais wa Fifa atakuwepo, Rais wa CAF atakuwepo na marais wa vyama vya soka vya maeneo mengine, hivyo inahusisha vyombo vingi za Serikali," amesema Kajula.
 
Awamu ya kwanza ya wanajeshi wa Ufaransa wapatao 1,500 wameondoka nchini Niger baada mamlaka ya kijeshi iliyochukua madaraka ya nchi hiyo mwezi Julai, kuwaamuru Wafaransa hao kuo#tunaliwezeshataifa.

Mamlaka katika Mji Mkuu wa Niamey imesema kuwa askari hao wameanza kuondoka katika ngome zao nchini humo, wakiwa wanaenda “uelekeo wa Chad,” huku kikosi chao cha kwanza kikisindikizwa na wanajeshi wa Niger.

Kwa mujibu wa mtandao wa Aljazeera, jana Jumanne Oktoba 10, 2023, magari ya wazi pamoja na yale yenye vifaa vya kuzuia vilipuzi, yalionekana yakiwa yamewabeba wanajeshi hao wa Ufaransa, yakipita njia za vumbi na kuondoa katika mji huo wa Niamey.

Katika taarifa ilisomwa kwenye luninga ya taifa, utawala wa kijeshi nchini humo, umewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa msafara huo, ambapo wamesema, utahusisha askari 1, 500 watakao ondoka kwa njia ya barabara kuelekea Chad, ambayo ni safari ya mamia ya kilometa, huku ikiwalazimu kupita maeneo yenye hatari.

“Leo vikosi vilivyokuwa Ouallam, vimeondoka katika ngome yao, haya ni maandalizi ya kuondoka kwa awamu ya kwanza ya askari watakaotumia njia ya barabara kuelekea Chad, wakisindikizwa na vikosi vyetu vya ulinzi na usalama,” Jeshi la Niger limesema.

Mbali na wanajeshi hao watakaondoka kwa njia ya barabara, “ndege tatu maalum” zimesajiliwa katika uwanja wa ndege wa Niamey, kati ya hizo, mbili ni kwa ajili ya kuviondoa “vikosi maalum” na moja ni maalum kwa ajili ya “vifaa.”
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa ufafanuzi juu ya taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu malalamiko ya Emmanuel Gadi kuwa TRA imetengeneza mfumo wa kuingiza mizigo nchini nje ya mfumo halali wa Serikali kinyume na Sheria ya Forodha.

Taarifa iliyotolewa na Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata imesema “Tunapenda kuufahamisha umma na jamii kwa ujumla kuwa, Mamlaka haina mfumo wowote mwingine inaouendesha wa kuingiza mizigo nchini nje ya mfumo wa Forodha wa TANCIS ambao unatumika kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACCMA).

“Emmanuel Gadi alifikisha malalamiko yake kwa njia ya barua tarehe 27 Februari, 2023 akidai kupewa uthibitisho na TRA wa kuingiza mzigo wa vifurushi 471 vya “Toner Cartridges” kupitia kampuni ya Tosh Logistics Ltd, TRA ilifanya uchunguzi wa kutosha na kuthibitisha kwamba, hapakuwa na mzigo wowote ulioingizwa nchini kwa jina la Wintech Tanzania Ltd wa vifurushi 471 vya “Toner Cartridges” kupitia kadhia yenye namba TZDL-22-1382193 ya tarehe 18 Agosti 2022 kama anavyodai.

“Hivyo, TRA ilimjibu Mhusika kupitia barua yenye kumbukumbu namba CF 8/92/01 ya tarehe 25 Julai 2023 ikimjulisha kuwa, kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa “House Bill of Lading” na kutoonekana kwa mzigo huo kwenye kadhia iliyowasilishwa na kampuni ya Tosh Logistics Ltd, TRA isingeweza kuthibitisha kuingizwa kwa mzigo huo nchini, kupitia taarifa yake aliyoitoa kwenye vyombo vya habari tumebaini kuwepo viashiria vya ukwepaji kodi kwani ni dhahiri kuwa mzigo huu uliingizwa kwa njia za magendo, TRA inamtaka mlalamikaji kuwasilisha nyaraka na uthibitisho wa kampuni yake kuingiza mzigo huo nchini mara moja ili hatua stahiki zichukuliwe”
 
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, katika matamshi yake makali tangu kuanza kwa mzozo kati ya Palestina na Israel, ametoa wito wa kuachiliwa kwa Mateka wote waliochukuliwa na wanamgambo wa Hamas na kusema Israel ina haki ya kujilinda.

Mtandao wa @DW_Kiswahili umeripoti kuwa akiongea mwishoni mwa hadhara yake ya kila wiki kwa maelfu ya Watu katika uwanja wa St. Peter, Papa Francis ameelezea pia wasiwasi wake juu ya kuzingirwa kwa Israel na Gaza.

"Ninaendelea kufuatilia, kwa uchungu na wasiwasi kile kinachotokea Israel na Palestina, Watu wengi sana wameuawa na wengine kujeruhiwa, naziombea Familia zilizoshuhudia siku ya sikukuu ikigeuka kuwa siku ya maombolezo na ninaomba kwamba Mateka waachiliwe mara moja”

"Ni haki ya wale wanaoshambuliwa kujilinda, lakini nina wasiwasi mkubwa na mzingiro mzima wa Wapalestina wanaoishi Gaza, ambako pia kumekuwa na wahasiriwa wengi wasio na hatia”

Jeshi la Israel limefanya mashambulizi ya ndege usiku kucha katika viunga vya ukanda wa Gaza, huku vita vyake dhidi ya kundi la Hamas vikiingia siku ya tano leo Jumatano na zaidi ya Watu 2,200 wameuawa katika vita hivyo kwa pande zote huku vifo vikihisiwa kuongezeka.
 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa (UVVCM), Comrade Mohammed Ali Kawaida ameiomba Serikali kuharakisha mchakato wa kuboresha na kurejesha mikopo ya Vijana 4% zilizokuwa zinatolewa kupitia Halmashauri zote nchini ili Vijana wanufaike kwa kupata pesa ambazo watazitumia kujiinua kiuchumi.

Kawaida ameyasema hayo wakati akiongea kwa niaba ya Vijana wote nchini katika Uzinduzi wa Wiki ya Vijana Mkoani Manyara.

"Tunaomba Wizara husika iharakishe mchakato wa maboresho ya namna bora ya kutoa mikopo ya 4% za Halmashauri ili Vijana waendeleale kunufaika na kujikwamua kiuchumi”

"Kipekee nimpongeze sana Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anazozifanya kukuza uchumi wa Nchi yetu lakini pia kwa kuendelea kuwaamini Vijana katika maeneo mbalimbali ya Uongozi na kututafutia fursa za kuweza kujikwamua kiuchumi"
 
Serikali kupitia Wizara ya Afya imeitaka Jamii kuwekeza zaidi katika afya ya akili kipindi hiki ili kusaidia kukomesha ukiukwaji wa Haki za Binadamu ikiwemo unyanyapaa ambazo Watu wenye changamoto za afya ya akili wanaendelea kukumbana nazo siku hadi siku ambapo amesema matumizi ya pombe yaliyokithiri yanaleta changamoto kubwa ya uraibu na magonjwa ya akili.

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema hayo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Afya ya Akili Duniani yaliyofanyika Dodoma kitaifa ambapo Kaulimbiu ya mwaka huu 2023 ni 'Afya ya akili ni Haki kwa Binadamu wote’.

“Lengo kuu la maadhimisho haya ni kujenga na kuongeza ufahamu wa Wananchi juu ya madhara yatokanayo na matumizi ya pombe yaliyokithiri pamoja na kutafakari hali halisi na mwelekeo wa udhibiti wa matumizi haya Kitaifa na Kimataifa, kama tujuavyo matumizi ya pombe yanaleta changamoto kubwa ya uraibu na magonjwa ya akili”

“Tushikamane kwa pamoja na sio kuwatenga na kuwanyanyapaa Watu wenye changamoto ya afya ya akili, tatizo la afya ya akili ni la kila mmoja, unapomnyooshea mwenzako kidole kuwa ana tatizo la afya ya akili vidole vinne vinakuelekea wewe, kutokuotesha mti nyumbani kwako ni tatizo la afya ya akili, unaenda kwa Mtu nyumbani kwake ameweka tiles lakini huoni hata mti mmoja, nalo ni tatizo la afya ya akili"
 
Kuelekea mchezo wa ufunguzi wa African Football League ambao utachezwa October 20, 2023 kati ya Simba SC dhidi ya Al Ahly ya Misri katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC Ahmed Ally @ahmedally_ ametangaza viingilio na utaratibu wa Mashabiki katika mchezo huo ambapo hakutakuwa na tiketi za VIP A kama ilivyozoeleka.

Viingilio.
VIP B: 40,000
VIP C: 30,000
Machungwa: 10,000
Mzunguuko 7000
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…