Makapuku Forum

Makapuku Forum

Magazeti ya leo October 20, 2023.
Screenshot_20231020_061405_Opera%20Mini.jpg
 
AFRICAN FOOTBALL LEAGUE
.
[emoji1241] SIMBA SC [emoji739] AL AHLY [emoji1093]
[emoji354] 18:00
[emoji2522] Benjamin Mkapa
.
Leo dunia ya soka itahamia Tanzania katika Uwanja wa Benjamin Mkapa. Ni katika uzinduzi wa michuano mipya ya African Football League ambapo pamoja na shamrashamra za ufunguzi wake, kutapigwa mechi ya kiume kati ya Simba na Al Ahly kutoka Misri.
.
Simba imekuwa timu tishio kwa siku za hivi karibuni, ikiwa imefanya makubwa kwenye soka la Afrika, iliitangaza kuwa timu ya saba kwa ubora baada ya kufika robo fainali mara tatu mfululizo ya Ligi ya Mabingwa na mara moja Kombe la Shrikisho.
.
Simba wamekuwa bora wanapocheza na Ahly Kwa Mkapa, wakiwa wamekutana nao mara nne na kupata ushindi wa asilimia 100, yaani walishinda michezo yote na huu utakuwa mchezo wa tano wanakutana.
.
Kila la kheri @simbasctanzania
Screenshot_20231020_075442_Instagram.jpg
 
STAA wa Al Ittihad, Karim Benzema amekanusha vikali taarifa zinazosambaa kwamba yeye ni miongoni mwa watu wanaounga mkono magaidi.
.
Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa [emoji632] alidai Benzema ana uhusiano na kundi la kigaidi la Muslim Brotherhood. Kauli za kwamba Benzema anashirikiana na kundi hilo la kigaidi iliibuka baada ya staa huyo kuweka wazi hisia zake kupitia mitandao ya kijamii juu ya mgogoro unaoendelea baina ya Palestina na Israel.
.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Benzema aliandika: “Maombi yetu yote kwa watu wa Gaza na waathirika wote wa mabomu yanayorushwa katika eneo hilo ambayo hayawasamehi wanawake ama watoto.” Baada ya kauli yake hii Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa, Gerald Darmanin alipofanya mahojiano na CNews channel alisema:
.
“Benzema ana uhusiano na Kundi la Muslim Brotherhood.” Mbali ya kusema hayo taarifa zinadai baadhi ya viongozi wanataka staa huyo apokonywe uraia wa Ufaransa huku kukiwa na ripoti pia anaweza kupokonywa hadi Tuzo ya FIFA Ballod D’or ambayo alishinda mwaka jana ikiwa atakutwa kweli na hatia ya kushirikiana na kundi hilo.
.
Kundi hili linatambulika kuwa ni kundi la kigaidi ndani ya Saudi Arabia na nchi nyingine jumla sita. Kwa mujibu wa Le Parisien, Mwanasheria wa Benzema amesema kwamba wapo kwenye mchakato wa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mwanasiasa huyo kwa sababu kauli zake zimemharibia jina lake na heshima. “Tumepanga kufungua mashtaka dhidi ya waziri, kwa kuzingatia sheria ya kutoataarifa za uongo juu ya mtu au kutoa lugha zisizofaa juu ya mtu kwa sababu Benzema hana uhusiano wowote na kundi hili.”
.
Hii sio mara ya kwanza kwa Benzema kuhusishwa kushirikiana na Wahuni, iliwahi kutokea hivyo mwaka 2021, ambapo alikutwa na hatia ya kushirikiana na kikundi cha wahuni kumtapeli mchezaji mwenzake Mathieu Valbuena.
.
Valbuena alitishiwa kwamba atoe pesa ama kikundi hicho cha wahuni kisambaze video zake za faragha alizochukuliwa na Benzema ndio alikuwa amesimama mstari wa mbele kumtaka Valbuena akilipe kikundi hicho ili mambo yaishe jambo lililozua hisia tofauti kwa staa huyo na baada ya uchunguzi kufanyika Benzema akakutwa na hatia ambapo alitakiwa alipe faini ya dola 84,000!
Screenshot_20231020_075556_Instagram.jpg
 
[emoji599] OFFICIAL: Klabu ya Yanga imetozwa faini ya Sh 2,000,000 kwa kosa la mashabiki wake kurusha chupa za maji kiwanjani baada ya timu ya Ihefu kufunga bao la pili, pia kwa kosa la maofisa wa benchi la ufundi wa Yanga kuonekana wakipinga maamuzi na kumzonga mwamuzi wa akiba.
.
Naye Afisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe ametozwa faini ya Sh 1,000,000 kwa kosa la kumkejeli na kumdhalilisha mwamuzi Malogo.
Screenshot_20231020_075822_Instagram.jpg
 
SAMUEL ETOO — Ni jina lingine kubwa duniani lililowahi kukanyaga Uwanja wa Mkapa. Hakuna asiyemfahamu rais huyu wa sasa wa Shirikisho la Soka [emoji1062] Cameroon (Fecafoot) baada ya kustaafu soka. Amepita timu nyingi kubwa zikiwamo Real Madrid, Barcelona, Chelsea na Everton na kutengenza jina na ujio wake Tanzania ilikuwa ni moja ya vivutio kwa watazamaji.
.
Cameroon ilicheza mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Tanzania Juni 2008 ikiwa ni mwaka mmoja tangu ufunguliwe uwanja huo mwaka 2007. Kwenye mchezo huo timu hizo zilitoka suluhu na aliambatana na mastaa wengine wa nchi hiyo na waliotamba duniani kama Jean Makoun, Stephane Mbia, Pierre Webo, Alex Song, Rigobert Song, Andre Bikey, Allan Nkong na wengine.

……………..
Screenshot_20231020_075919_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom