Makapuku Forum

Kinachoendelea Gaza: Majeshi ya Israel yameingia hospitali kubwa.

Mashuhuda wanadai kwamba tayari wanajeshi wa Israel wameingia katika hospitali ya Al Shifa.

Al Shifa ndio hospitali kubwa zaidi huko Gaza. Waziri wa Afya amesema kwamba katika hospitali hiyo kuna zaidi ya watu 2000 wakiwemo wagonjwa 650 na wafanyakazi 500 hivi, wengine wakiwa raia wa kawaida.

Mashuhuda wanadai wameona vifaru vya Israel na zaidi ya makomando 100 wakiingia hospitalini hapo kupitia idara ya magonjwa ya dharura.

Marekani imetahadharisha kwamba haipendi kuona hospitali hiyo ikipigwa kwa makombora wala kurushiana risasi kwa sababu idadi kubwa ya watu walioko hapo hawana hatia na hawawezi kujitetea.

Wakati hayo yanatokea, jana wafanyakazi katika hospitali hiyo walifanikiwa kuzika zaidi ya watu 170 katika kaburi la pamoja kwa sababu maiti nyingi zilikuwa zimeanza kuharibika na nyingine kuliwa na mbwa.

Israel pamoja na Marekani zinasema kwamba wanamgambo wa Hamas wanatumia hospitali hiyo kama kambi yao, hata hivyo Hamas wamekuwa wakikanusha madai hayo...!
 
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo amewataka Watanzania wote kujiepusha kuhamasisha matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo bangi kwa kutumia mavazi, maneno na hata mitandaoni wakiwemo wale ambao comment zao mitandaoni na mitaani huonesha kutetea dawa hizo ambapo amesema atakayefanya hivyo atapimwa na akibainika anatumia dawa hatua zitachukuliwa.

Akiongea Jijini Dar es salaam, Lyimo amesema “Maabara yetu ya kisasa ikikamilika tu tutashughulika na wote yaani Mtu akihamasisha tu matumizi ya dawa za kulevya tunamkamata tunaenda kumpima tukikuta anatumia dawa za kulevya tunampeleka Mahakamani”

“Nitoe wito kwa Wananchi wote ambao kwa nafasi yoyote waliyonayo wanatumia kuhamasisha dawa za kulevya tuwaombe waache, kuanzia sasa hivi wale wote watakaokuwa wanahamasisha ikiwemo kwa mavazi, maneno na kwa kutumia majukwaa yao tutachukua hatua ikiwemo kuwapima ili kuhakikisha kama na wao wanatumia na tukikuta wanatumia sheria itachukua mkondo wake, maana huwezi tu kutetea kitu ambacho hautumii”

“Baada ya kutoa taarifa kwamba ukivuta bangi ubongo ukiharibika unawaza kuwaza visivyoonekana, nimeona Kituo kimoja cha Habari wanaanza kujadili na kusema kama tunaona visivyojulikana mbona Mimi ninatumia sijaviona hivyo vitu!?, sasa huyo Mwandishi wa Habari tutamtafuta ili tumpime kama kweli anatumia dawa za kulevya tuweze kumchukulia hatua kwasababu amejitangaza mwenye kuwa anatumia huo ni uhamasishaji wa matumizi ya dawa za kulevya”

“Huwa tunaenda Mikoani kuteketeza bangi, juzi kuna Kuna Mtu (Mbunge) akasema Bungeni kwamba sisi kazi yetu ni kupiga picha tu na selfie tukiwa tunateketeza bangi, ni kwakuwa tu Mbunge huyu kasemea haya Bungeni na wana kinga angesema nje ya Bunge tungempima na yeye ili kujiridisha kama na yeye ni Mtumiaji au laah”
 
Hisia mchanganyiko za wakazi wa bonde la Mto Msimbazi kufuatia tamko la Serikali kuwa watalipwa fidia ya ardhi ya Sh4 milioni kwa kila mwenye eneo, imeibuka huku wengine wakiunga mkono uamuzi huo, na wengine wakiupinga.

Awali kulikuwa na malalamiko ya wakazi hao baada ya kuonekana kuwa watafidiwa nyumba zao na si vinginevyo.

Kassim Said amehoji iweje wananchi wa Loliondo wao walilipwa vizuri na kujengewa hadi nyumba lakini wao wanaokaa mjini wanapewa kiasi hicho kidogo cha fedha?

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…