Makapuku Forum

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema kitendo cha Serikali kukusudia kuanza kuwatoza kodi wafanyabiashara wanaoweka matangazo madogomadogo mitandaoni kusaka wateja ni kuwarudisha nyuma kiuchumi.

Mbowe ametoa kauli hiyo ikiwa ni miezi michache imepita tangu Serikali kutangaza kufanya mabadiliko ya sheria ya kodi ili kuruhusu kukusanya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya asilima mbili hata kwa kampuni zisizo na ofisi nchini.

Kampuni zinazotoa huduma za kidijitali nazo zitaguswa na utaratibu huo utakapoanza kutekelezwa.

Kulingana na tangazo hilo lililotolewa na Serikali Julai mwaka huu, kodi hizo zitaiwezesha Serikali kukusanya zaidi ya Sh4.8 bilioni kwa mwaka.

Jana akitumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram na X (zamani Twitter), Mbowe alisema kwa mtu aliyejielimisha kuhusu mapinduzi ya nne ya viwanda duniani, ataelewa kuwa mabadiliko haya yanaanza na biashara ndogo zinazoanza mitandaoni na hukomaa na kuingia kwenye mifumo rasmi baadaye.

 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita imewaamuru wafanyabiashara wanane waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi, kuilipa Serikali fidia ya Sh923.8 milioni huku ikiamuru kutaifishwa pia kwa mali zao na Sh103.9 milioni.

Hii ni baada ya mahakama kuwatia hatiani kwa makosa matatu ya kuongoza genge la uhalifu, utakatishaji fedha na kuisababishia Serikali hasara, baada ya kuingia makubaliano na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na kukiri makosa yao.

Hukumu hiyo imetolewa jana Novemba 15, 2023 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Johari Kijuwile baada ya kuwatia hatiani kwa makosa hayo ambapo mbali na kuwaamuru kuilipa serikali fidia, pia wametakiwa kutotenda kosa lolote la jinai ndani ya miezi 12.

Makosa hayo walidaiwa kuyatenda katika siku tofauti kati ya Februari Mosi,2018 na Juni Mosi 2023 kwa kufanya biashara ya kuuza dhahabu kilo 2,348 zenye thamani ya Sh345.9 bilioni bila kuwa na leseni.
 
Shirikisho la Kimataifa la Historia ya mpira wa miguu na takwimu Duniani (IFFHS) limeitangaza Yanga kuwa ni Klabu namba nne kwa ubora Afrika na Simba SC namba 12.

Takwimu hizi ni kwa kipindi cha kati ya September 01, 2022 hadi Augst 31, 2023, huku vilabu namba moja ni Al Ahly ya Misri na Wydad Casablanca ya Morocco.
 
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo amesema wameanza mchakato wa kudhibiti matumizi ya shisha ili yeyote atakayeuza awe na kibali na iuzwe kwenye maeneo maalum badala ya kila Mtu kuuza, hii ni baada ya kubaini Wauza shisha wanaichanganya na bangi na unga na kuathiri Watumiaji kwa kupata kansa ya koo na madhara mengine.

Akiongea Jijini Dar es salaam, Lyimo amesema “Shisha tunaifanyia kazi na mchakato upo ili kuidhibiti, yeyote atakayeuza shisha atakuwa na kibali na maeneo maalum sio kila Mtu ataweza kuiuza, wanaochanganya bangi na Heroin kwenye shisha hawatoweza maana itakuwa maeneo machache na tutapima mara kwa mara kuhakikisha hilo halifanyiki”

“Matumizi ya shisha na uchanganyaji wa dawa za kulevya ukiendelea madhara yake ni makubwa sana, tumeshuhudia Watumia shisha wengine wana kansa ya koo, wanavimba makoo, wengine wana kansa ya utumbo mfumo wa hewa ina madhara makubwa ukienda Hospitali za kansa mtakutana nao”

“Watanzania msitumie vitu vya kuiga, mbaya zaidi wanaodanganywa zaidi ni Wadada ukienda klabu kubwakubwa Wadada ndio wanatumia kwa wingi, wengine Mtu kama anampenda Mdada anamsumbuasumbua wanatumia shisha wanamuwekea dawa za kulevya kule mwisho wa siku anaondoka nae tayari ameshaambukizwa magonjwa n.k, lakini pia Mdada akichanganyiwa shisha na dawa za kulevya mwisho anachukuliwa na Mtu ambaye hajawa na mahaba nae”
 
Ditrick Muogofi (43) amehukumiwa kunyogwa hadi kufa kutokana na kosa la mauaji aliyoyatekeleza katika Kijiji cha Itulike Kata ya Ramadhani Mjini Njombe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Mahamod Hassan Banga ametoa taarifa kuhusu hukumu hiyo ya kesi ya mauaji No 53 ya mwaka 2023, wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya oparasheni mbalimbali za Polisi Njombe kwa kipindi cha kuanzia September 1 mpaka October 31,2023 ambapo pia amesema katika kipindi hicho Alex Simon Gwavi (65) alihukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la kumbaka Mtoto wake wa kike huko Mundindi katika Wilaya ya Ludewa.

"Ditrick Muogofi huyu alihukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la mauaji huko katika Kijiji cha Itulike, Ramadhani Njombe lakini kuna Mtu anaitwa Alex Simon alihukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la kumbaka Binti yake katika Kijiji cha Mundindi wilayani Ludewa kwa kesi namba 44 ya mwaka 2023"
 
Serikali Mkoani Kigoma imeunda Tume ya Watu sita kuchunguza chanzo cha kifo cha Enock Elias Mkazi wa Katoro Mkoani Geita ambaye alikamatwa na Askari wa Uhamiaji Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma na kupotea kisha mwili wake Kuokotwa katika Kijiji cha Chilambo kilichopo katika Wilaya hiyo ya Kakonko.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko, amesema Tume hiyo itafanya kazi kwa siku saba na kuwasilisha matokeo yake ili Serikali ichukue hatua kwa Watu watakaobainika kuhusika na kifo cha marehemu.

Mwili wa marehemu ulitambuliwa na Ndugu na kisha kuzikwa katika Kijiji cha Ilabilo Katanga Wilayani Kakonko huku Ndugu hao wakiitaka Serikali kutoa maelezo ya sababu za Ndugu yao kufikwa na umauti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…