Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mahakama ya Wilaya ya Mufindi imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela, Sostenes Vakuka baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kubaka.

Vakuka (32), mkazi wa kijiji cha Ihowanza, Kata ya Malangali ametiwa hatiani kwa kumbaka mwanamke mwenye miaka 20, ambaye ni mke wa mtu.

Hukumu hiyo imetolewa jana Desemba 6, 2023 na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mufindi, Edward Uphoro.

Katika kesi hiyo, ilidaiwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Februari 25, 2023 saa moja usiku katika Kijiji cha Ihowanza akiwa nyumbani kwa mwanamke huyo ambapo alimuingilia kinguvu bila ridhaa yake, huku akimuuliza ni nani amemruhusu kuishi katika nyumba hiyo.

Siku ya tukio inaelezwa mume wa mwanamke huyo alikuwa amekwenda dukani kununua mahitaji.

Screenshot_20231207_134529_Instagram.jpg
 
Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema Wizara hiyo imetoa lita 14,500 za petroli na dizeli kwa ajili ya kusaidia na kurahisisha shughuli zinazoendelea Hanang Wilaya ya Katesh mkoani Manyara kulikokumbwa na janga la maporomoko ya matope.

Kapinga amesema hayo leo Desemba 7, 2023 akimuwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko baada ya kuwasili katika eneo hilo ili kuona uharibifu wa miundombinu ya sekta anayoisimamia ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa magizo Rais Samia Suluhu Hassan aliyatoa kwa viongozi wote.

Amesema mafuta hayo yaliotolewa ni kwa ajili ya mitambo na magari yanayotumika katika kuondoa matope na magogo katika eneo hilo.

Screenshot_20231207_134705_Instagram.jpg
 
Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) imetoa orodha ya timu tatu bora zinazowania tuzo ya klabu bora ya mwaka 2023 ambazo ni Al Ahly ya Misri, Wydad ya Morocco na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini

Katika kipengele hicho zilianza timu 10 ikiwemo Yanga ya Tanzania na ikapenya katika mchujo wa tano bora na leo katika tatu bora imeshindwa kupenya.

Tuzo hizo zitatolewa Desemba 11 jijini Marrakech nchini Morocco.
Screenshot_20231207_134918_Instagram.jpg
 
Kocha wa Simba, Abdelhak Benchikha ameingia katika orodha ya makocha watatu wanaowania tuzo za CAF 2023 ambazo zitafanyika Jumatatu Desemba 11, mwaka huu.

Benchikha anachuana na Walid Regraui wa timu ya Taifa ya Morocco na Alidu Cisse wa Senegal.
Screenshot_20231207_135033_Instagram.jpg
 
Waziri wa Uhamiaji nchini Uingereza, Robert Jenrick amejiuzulu jana Jumanne kwa madai sheria ya dharura ya Serikali ya Rwanda kuwa haijitoshelezi.

Katika barua yake ya kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak, waziri huyo amesema waziri mkuu ameelekea kwenye msimamo wake kuhusu kutokubaliana na sheria hiyo ya dharura.

"Hata hivyo, sikubaliani na sheria inayopendekezwa kwa sasa kupitia Bunge, kwani siamini kwamba inatupa fursa nzuri zaidi ya kufanikiwa," amesema Jenrick.

Amesema umakini zaidi ulihitajika kumaliza changamoto za kisheria ambazo zinaweza kukwamisha mpango huo wa Serikali ya Uingereza na Rwanda.

Muswada huo uliozinduliwa hivi karibuni na umeweka wazi kwamba Rwanda kuwa ni nchi salama kwa wanaotafuta hifadhi.

Screenshot_20231207_135146_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom