Wakili wa Miriam Mrita katika kesi ya mauaji ya Aneth Msuya, Peter Kibatala amesema Mahakama Kuu imekubaliana nao kwamba upande wa mashitaka wameshindwa kuthibitisha mashikata dhidi ya washtakiwa wote wawili hivyo kuwaachia huru.
Kibatala amesema watu wa Arusha wakae tayari kumpokea dada yao anayewaletea.
Kibatala ametoa kauli hiyo leo Februari 23, 2024 baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Saalam kuwaachia huru mjane wa Bilionea Msuya, Miriam Mrita na mwenzake Revocatus Muyella waliokuwa wakikabiliwa na shitaka moja la mauaji ya Aneth Msuya.
#BREAKING: Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam imemuacha huru Mke wa Marehemu Bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na Mfanyabiashara Revocatus Everist baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha makosa dhidi yao.
Wawili hao walifikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza February 23 ya mwaka 2017 wakikabiliwa na kesi ya jinai namba 103 wakituhumiwa kumuua mdogo wa Bilionea Msuya, Aneth Msuya kwa kumchinja Kigamboni, May 26, 2016.
“Baada ya kujiridhisha pasina kuacha shaka, Mahakaa hii inawaachia huru wawili hawa kutokana na upande wa mashtaka kutothibitisha makosa dhidi yao,”
“Kuhusu gari Land Rover lililotolewa Mahakamani kama kielelezo sio sehemu ya familia hiyo, gari litataifishwa na Serikali”
Fundi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Jackson Mkami aliyeongoza kikosi cha uokoaji cha Shirika hilo kwenye tukio la moto ulioteketeza Lounge maarufu ya starehe ( Kitambaa Cheupe ) Tabata Barakuda Dar es salaam leo, amesema chanzo cha moto huo ni Mafundi wa kuchomelea vyuma waliokua wakifanya kazi eneo hilo.
“Kuna Mdada alikua counter akasema Mafundi walikua wanachomea kwahiyo ni moja kwa moja inakuja dhahiri kwamba uchomeaji aidha umeleta hitilafu yoyote ndio sababu ya kuungua kwa hili jengo” - Mkami.
Pamoja na kwamba Mkurugenzi wa Kitambaa Cheupe hakutaka kuongea sana kwa leo na kuahidi kutoa taarifa rasmi hapo baadae, kiu ya wengi ilikua ni kutaka kujua kama kuna Mtu amejeruhiwa au amepoteza maisha kitu ambacho amekiri hakuna aliyeumia wala kupoteza maisha lakini kiu ya pili ni kitu ambacho hajakizungumzia kwa leo ambacho ilikua ni kiu ya wengi kutaka kufahamu kama Kampuni yake ilikata BIMA kwa ajili ya biashara hiyo.
Tukio hili limetokea ikiwa ni siku moja tu imepita toka ‘Mfariji’ Benki ya NMB ianzishe kampeni yake kubwa kupitia CloudsFM ikihamasisha Watanzania kukata BIMA tofautitofauti katika Matawi mbalimbali ya Benki hiyo yaliyotapakaa Nchi nzima zikiwemo BIMA za biashara ili kutengeneza mazingira ya kulipwa pale majanga yanapotokea kama hivi.