Makapuku Forum

Watu tisa wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa kwenye ajali iliyohusisha magari mawili wilayani Bagamoyo Mkoa Pwani jana Machi 10, 2024 jioni.

Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge amesema taarifa za awali zinaonyesha kuwa dereva wa lori alikuwa anayapita magari yaliyokuwa mbele yake kwenye eneo lisiloruhusiwa, ndipo alipogongana uso kwa uso na basi dogo aina ya Toyota Coaster.

"Ajali imetokea eneo la Kiromo Bagamoyo Mkoa wa Pwani na dereva wa lori aliyekuwa akitokea Bagamoyo kwenda Dar es Salaam alikuwa anayapita magari kwenye eneo lisiloruhusiwa, ndipo akagongana uso kwa uso na gari ya abiria aina ya Toyota Coaster iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda Bagamoyo," amesema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo amesema kuwa kati ya waliopoteza maisha, saba ni wanaume na wawili ni wanawake.

"Majeruhi watatu wamefikishwa Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo kwa ajili ya matibabu," amesema.

 
Ikiwa ni ndani ya saa 24 toka Mwimbaji Staa wa Bongofleva Alikiba azindue Redio yake Jijini Dar es salaam, Mfanyabiashara Nguli wa Media Tanzania @JosephKusaga ambaye pia ni Mwanzilishi wa Clouds Media, amempongeza Staa huyo kwa hatua hiyo kubwa aliyopiga na kumwambia mlango wake uko wazi wakati wowote.

Katika Instagram page yake ambayo hupost mara chache, Mkongwe huyu amemuandikia Alikiba maneno yafuatayo ———> “Hongera sana Alikiba kwa uzinduzi wa kituo chako kipya cha redio! [emoji343]@CrownFMTZ katika dunia ya media inayobadilika kila wakati, inahitaji ujasiri, ubunifu, na ushirikiano mkubwa na jamii ili kuacha alama na ni wazi kwamba Ali anajiandaa kutuletea kitu cha pekee sana hewani”

“Nikiwa na zaidi ya miaka 25 katika tasnia ya media, nimeshuhudia matunda ya ushirikiano na faida za kuheshimu na kujifunza kutoka kwa wale walio jenga njia, kwa Vijana wote wenye ndoto kubwa huko nje, kumbukeni kwamba unyenyekevu, heshima, na umoja ndio chanzo cha mafanikio ya kudumu. [emoji93]”

“ @officialalikiba , jua mlango wangu daima uko wazi kwako. Iwe ni kwa ushauri, ushirikiano, au tu mazungumzo kuhusu mustakabali wa media, niko hapa kusaidia safari yako kwa kila hatua. Pamoja, tunaweza kupeleka tasnia ya media kwenye viwango vipya! [emoji573]” ——— amemalizia Kusaga.

Joseph Kusaga ambaye kwa miaka kadhaa sasa Dubai imekua sehemu ya makazi yake baada ya kufungua biashara ya Media kwenye Umoja wa Falme za Kiarabu, anaheshimika kwa kufungulia dunia ya ajira kwa Vijana wengi kupitia vitu mbalimbali alivyovianzisha ikiwemo Clouds Media Tanzania, Clouds Rwanda, Iguchi FM Burundi ( Clouds Burundi), Tamasha la FIESTA na miradi mingine mbalimbali nje ya Media.
 
Chama tawala Nchini Rwanda cha Rwandan Patriotic Front (RPF) kimemteua Kiongozi wa Chama hicho ambaye pia ni Rais wa Nchi hiyo paulkagame, kugombea tena Urais kwenye Uchaguzi unaofanyika July mwaka huu ambapo akishinda itakuwa ni awamu yake ya nne kuiongoza Rwanda kama Rais.

Kagame amekiongoza Chama hicho tangu mwaka 1998 (miaka 26) na mwaka jana mwezi April kilimchagua aendelee kuhudumu kama Mwenyekiti wake.

Muda mfupi baada ya kupitishwa kuwa Mgombea Kagame usiku wa kuamkia leo, Kagame amenukuliwa akisema “Tunafahamu Nchi ilikotoka, nathamini mchango wenu na imani yenu kwangu siku zote, mzigo mlionipa nimekubali kuubeba lakini narudia kusema tena, nataka Mtu wa kunitua huu mzigo na watakaoubeba wapo miongoni mwenu”

Rais Kagame ambaye October 23 mwaka huu atatimiza umri wa miaka 67, ameliongoza Taifa hili la Afrika Mashariki kwa miaka 24 sasa kuanzia April 2000 ambapo mwaka 2015 zilifanyika kura za maoni ambazo ziliondoa ukomo wa mihula miwili ya kikatiba kwa Marais wa Nchi hiyo ambapo uchaguzi uliofuata wa mwaka 2017 Rais Kagame alishinda kwa asilimia 98.8%.
 
Mwanamke mmoja aitwae Daines Mwashambo (30) Mkazi wa Kijiji cha Mashese, Mbeya Vijijini anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuua Watoto wake wawili kwa kuwanywesha sumu ya kuulia magugu shambani aina ya “Pare Force”.

Polisi wamesema Daines alifanya tukio hilo akiwa nyumbani kwake lakini vifo vya Watoto hao vilitokea muda mfupi baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya.

Kamanda wa Polisi Mbeya SACP- Benjamini Kuzaga amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni msongo wa mawazo uliotokana na Daines kutuhumiwa na Serikali ya Kijiji hicho kufanya udokozi na wizi kwa kuingia katika nyumba za Watu.

Imeelezwa kuwa baada ya kuwanywesha sumu Watoto wake, Mtuhumiwa naye alikunywa sumu lakini akawaiwa kabla haijamuua ambapo kwasasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya chini ya ulinzi wa Polisi.
 
Ukraine imekataa pendekezo la Papa Francis la kufanya mazungumzo na Urusi ili kumaliza mapigano yaliyodumu kwa zaidi ya miaka miwili ikisema Kyiv haitajisalimisha kamwe.

Papa Francis amesema kutokana na hali kuzidi kuwa mbaya kwa pande zote “mtu anapaswa kuonyesha ujasiri wa kusalimu amri kwa kuinua bendera nyeupe na kujadiliana.”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…