Makapuku Forum

[emoji187] Najua kwamba Simba na Yanga wanaombeana mabaya. Sijui ilianzia lini lakini kwa umri wangu chuki kubwa zaidi iliendelezwa katika lile pambano la fainali za CAF mwaka 1993. Simba dhidi ya Stella Abidjan. Mgeni rasmi alikuwa Mzee Rukhsa. Mwenyezi Mungu amrehemu. Kabla ya mechi nchi nzima ilikuwa imesisitiziwa kwamba tunapaswa kuwa wazalendo kwa sababu Simba walikuwa wanakaribia kutuletea kombe la kwanza kubwa nchini.
.
Mfumo wa tiketi ulikuwa huu huu kwahiyo hakukuwa na namna ya kuweza kuwazuia YANGA kuingia uwanjani. Ujumbe tu kutoka kwa Rais na watu wazito ni kwamba Yanga walipaswa Kuishangilia Simba. Walipokuja uwanjani hawakuishangilia Simba wala Stella lakini Boli Zozo alipoifungia Stella bao la pili na kufanya matokeo kuwa 2-0 ndipo Yanga walipolipuka na kuimba kwa furaha wakisema “uzalendo umetushinda”.[emoji23]
.
Kuanzia hapo kila kitu kimekuwa wazi. Hakuna unafiki tena. Na umekuwa mwendo wa visasi kiasi kwamba katika dunia hii ya utandawazi watu wamekuwa wakivaa hadi jezi za timu pinzani. Si zinauzwa nchini na watu wanalipa kodi kuziingiza? Hakuna tunachoweza kuzuia kwa sasa. Afadhali tungezuia huko mwanzoni kwa kukemea mambo kadhaa. Na sasa nadhani imekuwa kama chachu tu kwa timu zetu kufanya vizuri.
.
Ukiwafunga Mamelodi unawafunga mdomo Mamelodi na Simba. Ukiwafunga Al Ahly unawaziba midomo Al Ahly na Yanga. Ni kazi ngumu lakini lazima wachezaji wetu waifanye. Hakuna namna kwa sababu hakuna tunachoweza kubadili kama Dk. Ndumbaro alivyosema na baadaye kutolewa taarifa rasmi kwamba “alitania tu.” Acha mashabiki waende uwanjani kushangilia wapinzani. Kitakachowanyamazisha ni ubora tu wa timu ya nyumbani.
.
Unadhani Yanga walifurahi kuona Simba wanakwenda robo fainali mara nne mfululizo? Ubora wa Simba ya Jose Luis Miquissone yule na wahuni wenzake uliwalazimisha. Baadaye wenyewe walichoka kwenda kushangilia wapinzani wa Simba. Ni hadithi ya Yanga kufika fainali za Shirikisho. Watu walioumia zaidi duniani ni Simba lakini hawakuwa na la kufanya. Ubora wa Yanga na kina akina Aziz Ki uliwalazimisha. Huu ndio ukweli halisi. Ukweli ambao lazima usemwe.

— Edo Kumwembe [via Jicho la Mwewe]
 
Kamati ya Uchunguzi Nchini Urusi imeagiza kukamatwa kwa Washtakiwa wengine watatu wa Familia moja (Baba na Watoto wake wawili) ambao tayari wamefikishwa Mahakamani na kujumuishwa kwenye kesi ya shambulizi la kigaidi lililoua zaidi ya Watu 130 Crocus City Hall Nchini humo wakidaiwa kuhusika kwa kuwasaidia Magaidi hao kwenye masuala mbalimbali ikiwemo kupanga mipango ya shambulizi na kuwauzia gari jeupe ambalo walitumia kufika Crocus Hall na kuwaua Watu kisha wakalitumia gari hilo kujaribu kutoroka.

Washtakiwa hao ni Islomov Isroil Ibrahimovich (62) na Watoto wake Islomov Aminchon Isroilovich (33) na Islomov Dilovar Isroilovich ambao wote wamesomea mashtaka na kupelekwa mahabusu hadi May 22,2024 watakaporudi tena Mahakamani.

Kwa mujibu wa uchunguzi, Mshtakiwa wa tatu wa mauaji kati ya wanne waliofikishwa Mahakamani jana usiku ambaye anaitwa Shamsidin Fariduni (25) alimshawishi Aminchon Isroilovich (33) na kufanikiwa kumuingiza kwenye kundi lao la kihalifu kipindi cha mwezi January mwaka huu na baadaye akamuingiza kwenye kundi Dilovar March 11,2024.

Itakumbukwa usiku wa kuamkia leo Wanaume wanne waliohusika moja kwa moja na kuua Watu kwenye shambulizi hilo wakifikishwa Mahakamani wakikabiliwa na kesi ya ugaidi ambapo wamefikishwa Mahakamani hapo wakiwa na majeraha na muonekano dhaifu unaodaiwa kusababishwa na nguvu iliyotumika kuwadhibiti wakati wa kuwakamata na adhabu ya kuteswa ili wataje waliowatuma na genge lao lote.

Washtakiwa hao wametambuliwa kwa majina ambapo Mshtakiwa wa kwanza anaitwa Dalerdzhon Mirzoyev (32), wa pili Saidakrami Murodali Rachabalizoda (30), wa tatu Shamsidin Fariduni (25) na wanne ni Kijana mdogo Muhammadsobir Fayzov mwenye umri wa miaka 19 ambaye amefikishwa Mahakamani akisukumwa kwenye kiti cha Wagonjwa huku akionekana kuwa mahututi ambapo wote wamerejeshwa rumande hadi May 22,2024.
 
Shunie chukua fomu na wewe gombea mwakani tukuchague makapuku wote, ukiingia madarakani unatupa vitengo nyeti vyote tunavikamata
 
Rapa na mfanyabiashara wa Marekani, Diddy, ameuza hisa zake zote za kampuni yake ya ‘Revolt TV’ kwa mtu asiyejulikana, baada ya uvamizi wa nyumba zake huko Los Angeles na Miami jana Jumatatu. Uvamizi huo ulikuwa sehemu ya msako mkali uliofanywa na polisi kuhusiana na uchunguzi wa kesi za unyanyasaji wa kingono zinazomkabili rapa huyo.

Mwaka jana, Diddy alijiuzulu uenyekiti wa kituo hicho cha habari ili kulinda uwekezaji wa kampuni zinazotangaza kupitia ‘Revolt’, ikiwa ni pamoja na Kampuni ya Kuunda Magari ya Cadillac na Mtandao wa Huduma za Simu wa AT&T.

Diddy amekuwa akikabiliwa na kashfa na kesi zinazohusu unyanyasaji wa kingono, ikiwa ni pamoja na kesi dhidi ya aliyekuwa mpenzi wake, mwimbaji wa R&B, Cassie, tangu mwaka 2023.
 
Serikali ya Urusi imekataa ofa ya Polisi wa kimataifa (Interpol) ya kuwasaidia kufanya uchunguzi kujua Wahusika Wakuu wa shambulizi lililoua Watu zaidi ya 130 Crocus City Hall Nchini humo.

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema Urusi itafanya uchunguzi yenyewe kwakuwa wameshazoea na wanazijua vizuri mbinu za Nchi za Magharibi na namna wanavyofanya upendeleo kwenye maswala ya uchunguzi.

“Sikumbuki kama Interpol walijitolea kutusaidia uchunguzi wa shambulizi la bomba la mafuta la Nord Stream (ambao ulikata njia kuu ya usafirishaji wa gesi kutoka Urusi hadi Ulaya ) ingawa tuliliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kwahiyo hatutaki msaada wa uchunguzi wao kwenye shambulizi hili ili walete upendeleo wao” ——— Sergei.
 
Mwanaume aitwaye Alisher Kasimov Raia wa Kyrgyztan na Baba wa Watoto wanne, amefikishwa Mahakamani leo March 26,2024 Nchini Urusi kwa tuhuma za kuwapangishia nyumba Magaidi waliohusika katika shambulizi la kigaidi lililoua zaidi ya Watu 130 Nchini humo ambapo kukamatwa kwake kunafanya idadi ya Watuhumiwa wa ugaidi waliokamatwa hadi sasa kufikia wanane.

Kasimov amesema hajui lolote kuhusu shambulizi hilo akisema yeye alimpangisha Gaidi mmoja kama Wapangaji wengine tu na hakuwa anajua kwamba ni Gaidi “Mimi niliweka matangazo ya apartment yangu kwenye mtandao wa Avito na nikapata Mteja wala sikujua kuwa anahusika na ugaidi na sikujua kama
ataitumia apartment kupanga mipango ya ugaidi”

Baada ya kusomewa mashtaka yake Kasimov amepelekwa rumande hadi atakaporejea tena Mahakamani May 22,2024 pamoja na Washtakiwa wengine saba wakiwemo wanne waliohusika na mauaji moja kwa moja huku wengine watatu (Baba na Wanae wawili) wakidaiwa kuwauzia gari Magaidi hao.
 
Mahakama ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma imemuhukumu kifungo cha miaka 20 jela Kijana Mussa Ally Makandaje (32), Mkazi na Kijiji cha Msinjili Wilaya ya Tunduru baada ya kupatikana na hatia katika kosa la kukutwa na vipande 14 vya nyama ya mnyama aina ya pofu.

Akisoma hukumu hiyo ya kesi ya jinai Na.18 ya mwaka 2023, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Lilian Haule amenukuliwa akisema “Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa pasipo kuacha shaka yoyote”.

Imeelezwa kuwa Mtuhumiwa alitenda kosa hilo August 10 2023 na kufikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza August 25 2023.

Pofu ni Mnyama Jamii ya swala anayepatikana katika mbuga mbalimbali za Tanzania na anatajwa kuwa na mwili mkubwa kuliko wote katika Jamii hiyo ya swala, sifa nyingine ni sura nzuri pamoja na utamu wa nyama yake uliyoifanya kuwa moja ya nyama zinazopendwa sana katika uwindaji.
 
Rais Samia Suluhu Hassan ameielekeza Wizara ya Maji kupitia Mamlaka za Maji kuondoa faini kwa kipindi cha mwezi mmoja kwa Wateja wake ili waanze kulipia kidogokidogo sehemu ya madeni yao halisi na kuagiza pia warejeshewe huduma ya maji wakati wakiendelea kupunguza madeni.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameyasema haya leo March 26,2024 Dodoma kwenye kikao kazi na Viongozi wa Watendaji wa Sekta ya Maji ikiwa ni pamoja na Menejimenti ya Wizara ya Maji, Wakurugenzi Watendaji wa Mamlaka zote za maji pamoja na Mameneja wa RUWASA kwa lengo la kuendelea kukumbushana na kuelezana kwa msisitizo wajibu wa Sekta katika kufanikisha utendaji kazi, utoaji huduma na utekelezaji wa miradi ya maji inayoendelea hapa Nchini.

“Tunatoa mwezi mmoja Mwananchi ambaye umekatiwa maji kwasababu ya faini umechelewa kulipa na umekatiwa maji, faini tunasamehe kwa mwezi mmoja kupitia maelekezo ya Mh. Rais, sasa chelewachelewa utamkuta Mwana sio wako, hata kama una kideni kikubwa niwaombe Watendaji wekeni utaratibu ili Mtu awe anapunguza kidogokidogo huku anapata huduma”

Aweso amewataka pia Watendaji wote wa Mamlaka za Maji na Bodi zake kuwa kipimo cha ufanisi katika kazi kitakua katika maeneo ya kudhibiti upotevu wa maji pamoja na kutochelewesha maunganisho mapya kwa Mteja mwenye kutaka huduma ya Maji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…