Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetabiri uwepo wa mvua kubwa katika mikoa 14 ya Tanzania bara na visiwani kuanzia Aprili 12 mwaka huu.
Utabiri huo umetolewa leo April 10,2024 na TMA, mvua zinategemewa kunyesha kwenye maeneo ya Mkoa wa Dar es salaam, Tanga, Morogoro, Pwani Lindi, Mtwara, Rukwa, Iringa, Mbeya, Songwe, Njombe, Ruvuma na visiwa vya Unguja na Pemba.
“Athari zinazotegemewa ni mafuriko na kuathirika kwa shughuli za kiuchumi katika maeneo hayo,”imeandikwa kwenye taarifa hiyo.
Aprili 13, TMA imesema mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Morogoro, Pwani, Lindi na Mtwara pamoja na Unguja na Pemba zitashuhudia mvua kubwa.
Baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Iringa, Njombe na Ruvuma yanapaswa kuchukua tahadhari kwani mvua kubwa inatarajiwa kunyesha.
Siku ya Aprili 14, Mkoa wa Dar es salaam, Tanga, Morogoro, Pwani Lindi na Mtwara na visiwa vya Unguja na Pemba zitashuhudia mva kubwa huku adhari zitakazotokea zikitajwa kuwa ni mafuriko na shughuli za kiuchumi kuathirika.