Makapuku Forum

Serikali imetangaza nafasi za kazi kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii 8,900 watakaokwenda kutekeleza afua jumuishi za afya, lishe na ustawi wa jamii katika ngazi ya vitongoji na vijiji.

Tangazo limelotolewa leo Jumamosi Aprili 6, 2024 na Wizara ya Afya kwa ushirikiano na Ofisi ya Rais Tamisemi likieleza kuwa, hivi sasa Serikali inatekeleza mpango jumuishi wa wahudumu wa afya wa ngazi ya jamii nchini.

Kupitia mpango huo, Serikali imeweka utaratibu wa kuwapata wahudumu wenye sifa zilizowekwa kutoa mafunzo na kuwatumia wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika utekelezaji wa afua hizo.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, awamu ya kwanza ya mpango huo utaanza kwenye mikoa 10 na halmashauri mbili kwa kila mkoa.

Mikoa itakayonufaika ni Geita wahudumu 920, Kagera (878), Kigoma (1094), Lindi (1724), Mbeya (836), Njombe (746), Pwani (480), Songwe (774), Tabora (966) na Tanga (482).

 
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa kuanzia leo Jumamosi, Aprili 6 hadi 9, 2024 ukionesha uwepo wa mvua kubwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Pwani, Lindi, Mtwara, Tanga na visiwa vya Unguja na Pemba.

Mbali na hiyo, mikoa mingine inayotarajiwa kunyesha mvua kubwa ni Kagera, Geita, Mwanza, Mara, Simiyu, Shinyanga na Kigoma.

Kutokana na mvua hizo kubwa mfululizo, TMA imeonesha uwezekano wa kutokea athari kwa makazi kuzungukwa na maji, na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi huku ikiwataka wananchi kuzingatia na kujiandaa kwa hali hiyo.

 
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetabiri uwepo wa mvua kubwa katika mikoa 14 ya Tanzania bara na visiwani kuanzia Aprili 12 mwaka huu.

Utabiri huo umetolewa leo April 10,2024 na TMA, mvua zinategemewa kunyesha kwenye maeneo ya Mkoa wa Dar es salaam, Tanga, Morogoro, Pwani Lindi, Mtwara, Rukwa, Iringa, Mbeya, Songwe, Njombe, Ruvuma na visiwa vya Unguja na Pemba.

“Athari zinazotegemewa ni mafuriko na kuathirika kwa shughuli za kiuchumi katika maeneo hayo,”imeandikwa kwenye taarifa hiyo.

Aprili 13, TMA imesema mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Morogoro, Pwani, Lindi na Mtwara pamoja na Unguja na Pemba zitashuhudia mvua kubwa.

Baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Iringa, Njombe na Ruvuma yanapaswa kuchukua tahadhari kwani mvua kubwa inatarajiwa kunyesha.

Siku ya Aprili 14, Mkoa wa Dar es salaam, Tanga, Morogoro, Pwani Lindi na Mtwara na visiwa vya Unguja na Pemba zitashuhudia mva kubwa huku adhari zitakazotokea zikitajwa kuwa ni mafuriko na shughuli za kiuchumi kuathirika.

 
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema jina la Tume ya Uchaguzi (NEC) litabadilika Ijumaa Aprili 12, 2024 na kuwa Tume Huru ya Uchaguzi.

Katika taarifa iliyotolewa leo katika mitandao ya kijamii ya ofisi hiyo imesema:

“Tunapenda kuvitaarifu vyombo vyote vya habari kwamba, kufuatia tangazo la Serikali namba 225 la Machi 29, 2024 Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi namba 2 ya mwaka 2024, itaanza kutumika rasmi Aprili 12, 2024.

“Hivyo, kuanzia Aprili 12, 2024 jina la Tume litabadilika na litakuwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi au kwa kiingereza Independent National Electoral Commission,”imesema taarifa hiyo.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…