Hivi itakuwaje siku moja, umekaa zako, mara huyo mwanao wa miaka mitatu anayeitwa Junior anaanza kukwambia, mama unajua mimi zamani nilikuwa naitwa John.
Nilikuwa napenda sana kucheza mpira. Rafiki yangu alikuwa anaitwa Vincent, yeye alikuwa mchokozi sana. Nyumba yetu iliungua moto mimi nilikuwa nimelala nikafia humo.
Nimemiss sana wazazi wangu wa zamani, lini utanipeleka niwaone.. katika hali hiyo utafanyaje.Eti utafanyaje..!? Ikitokea hivyo hautakuwa mwenyewe. Kuanzia mwanzoni mwa miaka 1960, Chuo Kikuu cha Virginia huko Marekani kimekuwa kikifuatilia na kurekodi matukio ya namna hiyo.
Mpaka sasa Chuo hicho kimekusanya taarifa za zaidi ya watoto 2,200 ambao wanakumbuka matukio ya maisha ya zamani.
Katika matukio mengi, watoto ambao wanakumbuka matukio yaliyotokea miaka mingi nyuma, wengi wanatoa taarifa sahihi ambazo wataalamu wanapozifuatilia wanakuta kweli mtu wa namna hiyo alikuwepo na hata namna alivyofariki ni kama alivyokuwa anaeleza yule mtoto.
Bado wataalam hawajajua vizuri ni nini kinachosababisha hali hii itokee kwa baadhi ya watoto, kwa sababu huwa inatokea hata kwenye watoto kutoka katika familia ambazo hazina imani ya umwilisho(reincarnation).
Wataalam wanashauri inapotokea hali kama hiyo usimchokonoe zaidi mwanao ili kueleza kwa sababu hiyo inaweza kusababisha mtoto kutoa majibu ya kutunga.
Na kama itatokea ana sisitiza anataka umpeleke kwa wazazi wake wa zamani, mwambie hayo yalikuwa mambo ya zamani yameisha pita...vipi ikikutokea utafanyaje utakwenda kutambika au utakanyaga mafuta na kukemea mapepo....!?